NMB wamekataa kupokea taarifa ya kuzuia miamala baada ya kadi ya benk kuibiwa matokeo yake wahalifu wamefanikiwa kutoa pesa

Katika menu ya nmb mkononi *150*66#
Kuna kipengele cha akaunti yangu.. Pale unapata option ya kufungia kadi yako muda wwte na kuifungua muda wwte.. Tujitahidi kuwa wadadisi wa vitu vinavyotuhusu sisi... Hususani mambo muhimu kama hili lako... Sidhani kama huna huduma hiyo ya nmb mkononi maarufu kama nmb mobile
Screenshot_20200228-163033_1582896686468.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
kama uliwa notify hilo katika namna ambayo unawezakufanya reference as ushahid, i think unaweza kuwafungulia mashatka ili kuwa sew and if possible wakulipe.

Tatizo unaweza kuta uli just wapigia cm tu basii no barua no nini..
Pole sanaa mkuu
 
Kwa mnaosema angeenda mwenyewe, lets say muhusika kapigwa hadi kupoteza fahamu, je asubiriwe hadi azinduke? Na huo muda wakutafuta Loss Report wezi watakuwa wanakusubiri?!

Kuna Sheria halafu kuna Hekima na Busara.
Wakamuibia, wakamuacha atafute simu, akatoa taarifa nyumbani, wakahakikisha kila kitu kiko sawa, wakaanza kumpiga akapoteza fahamu!!! Haingii akilini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nywila ilikuwa kwenye simu.
Poleni sana. Kosa la kwanza alilofanya ni kuweka password sehemu moja na kadi. Hili ni kosa kubwa na wakati mtu anapewa kadi huwa anaambiwa kabisa ikariri password ili hata ukipoteza kadi isiangukie kwenye mikono ya wahalifu. Kingine ni kwamba kuna namba ya simu ambayo mtu hupiga anapopoteza kadi ili ifunguwe. Yeye hakuwa na hii namba? Wakati unapewa kadi ni lazima hii namba inakuwepo kwenye zile karatasi. Pia kwenye website ya benki husika ni lazima kuna namba ya mawasilino iwapo kuna emergecy. Hiyo namba ndiyo alitakiwa aiweke kwenye simu na siyo password. Hata hivyo NMB Tanzania walifanya uzembe kwani wangeweza kusaidia kwa kutoa maelekezo ya simu huyo ndugu yako atakayopiga. NMB Tanzania mnaweza kuelezeaje haya malalamiko ya mteja wenu?
 
Kwa kawaida mngemshauri huyo mmiliki wa Akaunti apige simu huduma kwa wateja kisha aombe kadi yake kufungwa.

Angeulizwa maswali ambayo kimsingi angemudu kuyajibu kama salio lililopo, muamala wa mwisho kufanya, nambari ya simu anayotumia kwenye Akaunti n.k. Kisha wangei block bila kuhitaji mtu kwenda Physically.

Kwa kifupi uzembe mliofanya msiurudie tena siku nyingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ungefuata taratibu zao. Benki zote anayetakiwa kutoa taarifa ni mhusika mwenyewe ndio wanafunga
Kuna mazingira mwenye akaunti hawezi toa taarifa... mfano, akifanyiwa jambo hilo huku yupo eneo lisilo na tawi lao inakuwaje..???

Je akifanyiwa uharifu hadi akapoteza kumbukumbu, hilo ulosemalo linawezekanaje..?? Kuwe na namna kutoa taarifa kwa emergence... ni bora kufunga halafu ije ifunguliwe kuliko kugoma kufunga halafu watu wakakomba hela
 
Huo sio utaratibu mkuu usilazimishe alitakiwa aende mwenyewe tena mara tu baada ya kuibiwa na kama haitoshi hata kama mngemsaidia kwa kuazima simu na kupiga huduma kwa wateja wangemuuliza maswali mawili matatu kama namba ya akaunti na detail zingine kama namba ya simu na wangeizuia kwa muda ila wangemwambia afike ofisini pia.

Pia kupitia kwenye simu janja aka smartphone kuna option ya kuandika email kwenda NMB bank hivyo kupitia email address yake ambayo ameiandika wakati anafungua akaunti angeweza kutuma email kwa kutumia simu yako alafu angewapandia hewani.
Njia rahisi na haraka ni kupiga simu. Hii imewekwa kwa sababu njia nyingine zinatumia muda mrefu. Imagine umepoteza kadi usiku na bank zikiwa zimeshafungwa! Utaweza kwenda? eMail itasaidia? Ile namba inafanya kazi masaa 24/7. Huyu mtu wa benki alitakiwa amwongoze kwa kumpa hiyo namba na amwambie cha kufanya.
 
Back
Top Bottom