NMB wamekataa kupokea taarifa ya kuzuia miamala baada ya kadi ya benk kuibiwa matokeo yake wahalifu wamefanikiwa kutoa pesa

I
Kama wangekubali kufanya uliyotaka kufanya binafsi ningewashangaa sana na kuona hawana weledi wa kazi.
Wao walikuwa na hakika gani kama wewe au huyo ndugu yako kaibiwa??
Ingekua busala zaid km ofisa bank angetumia sim kumpigia mteja husika kutokana na kuibuka mtu kati kuhusu Account yake.
Kama simu ni miongoni mwa vilopotea basi wangemshauri kuenda tawi lililo kalbu naye kwa mlolongo uleule (Impitie)
 
Mkuu, kuna taratibu za kufuata kwa mtu ambaye ni mgonjwa au amefariki. Linapokuja suala la kisheria, ubinadamu huwa unakaa pembeni.
Ukiwa siku umelazwa ndiyo utajua kwanini huwezi kiuondoka kwenye drip uende bank badala yake utatuma mtu wa karibu
Bank ni miongoni mwa sekta ambazo ziko very limited kwenye kutumia ubunifu au akili ya kuzaliwa kwenye kutekeleza majukumu yake. Mfano leo hii wewe unaweza enda bank, ndani kuchukua pesa, Jamaa anatakiwa a verify sura yako na signature, sura inakuwa yako kabisa, ila ukiyumbisha signature kidogo tuu... hakuna namna utapata pesa zako...
Kuna sheria na taratibu kila mahali. Lakini kuna akili ya kazi (kujiongeza).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
By the way, scenario yako inaibua maswali mengi sana.

1. Unadhani kama wewe ungekuwa ofisa wa bank, ungefanya maamuzi kwa kutegemea habari za kuambiwa na mtu ambaye hana hata blood stream relationship na mtu aliyeibiwa!??

2. Simu nyingi za vijana siku hizi zina password kila kona, hao wezi waliwezaje ku unlock simu na kuzipata hizo passowrd za account yake!? Na zilisaviwaje!??

3. Kijana wako aliwezaje kuchukua simu na kukupigia wewe bila kuwaza kuwapigia watu wa bank, ambapo baada ya maswali kadhaa basi card yake ingekuwa blocked!?

4. Unadhani kitendo cha maofisa wa bank kushindwa kufanya kile ulichotaka ni uzembe!?? Anold,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee watake radhi NMB kuwarushia tuhuma ambazo si za kwao. Uzembe umeufanya wewe na kijana wako, muda ambao kijana wako amekupigia simu kukueleza yaliyo mkuta basi angetumia huo muda kuiblock kadi yake kupitia nmb mobile..au angepiga simu mwenyewe au angeenda benki mwenyewe au angeweza hata kuhamisha salio lote na kuliweka kwenye simu nk. Benki wako sahihi kukataa japo ni kweli kuna mambo busara inapaswa kutumika lakini si katika hali kama hiyo. Siku hizi watu wanamambo mengi ni rahisi sana kumhujumu mtu kwa namna yoyote kwa njia kama hiyo ya kufunga akaunti yake nk. Usiwalaumu benki walaumu wezi labda kwa kuiba tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashauri uongozi wa NMB waangalie baadhi ya taratibu ambazo hazina msingi katika usalama wa hela za wateja. Hakukuwa na sababu yeyote ya kupuuza taarifa za awali ilitakiwa kukubali taarifa na kuzifanyia kazi. Hili jambo kwa kweli limenisikitisha sana maana endapo mwenye akauti yupo hospitali au amekufa n.k itakuwaje? hizi ni kanuni mbovu kwenye usalama wa fedha za watu, sasa mmekataa na pesa zimeibwa kipi bora?
Wapeleke mahakamani watakulipa tu,toka lini kufungia miamala kukaleta athari kwa benki na mteja
Us kuna benki ukizoea kutoa hela temeke tu, ukienda mwenge unaweza ukakosa pesa wanajua niga kesha fanya yake
 
Hizi ni sheria za kijinga kwa sababu
1. Kuzuia akaunti isitumike kwa muda haina madhara yoyote
2. Hata kama ataketoa taarifa ni mwizi mwenyewe ili mradi tu akaunti haitatoa pesa litasimiasha akaunti hiyo kutumiwa isivyo
3. Kusubiri mwenye akaunti aende ni upuuzi wa kiwango cha flyover kwa sababu huenda ametekwa au yuko mazingira hatarishi na hawezi kufika .

Mambo ya kujiuliza akaunti ikizuiwa temporaly inaleta madhara gani kinachohitajika wakati wa kutaka kuotumia kutoa pesa utahitajika kuthibitisha pasipo shaka kuwa wewe ni muhusika halali.
Tuache kukariri mambo na kuwa na mazoea tu bila kujiuliza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama wangekubali kufanya uliyotaka kufanya binafsi ningewashangaa sana na kuona hawana weledi wa kazi.
Wao walikuwa na hakika gani kama wewe au huyo ndugu yako kaibiwa??
Maadhali palishakuwa na shaka ingekuwa vyema NMB kuizuia kwanza kisha kuwasiliana na mhusika.
 
Sio NMB peke yake, nadhani ndio utaratibu wa benki zote. Last Year, kaka yangu alifariki kwa tatizo la moyo, sikuwa naye karibu wakati akikumbwa na mauti, but nilipofika na kuomba vitu vyake, sikukuta card yake ya ATM ndani ya wallet yake.

But kwa vile nilikuwa naifahamu account yake, nikaenda kwenye tawi lililo karibu nami la benki ambayo ni STANBIC ile ya pale jirani na PPF tower. Mhudumu alinipokea, but akagoma pia kufunga account kwa madai only kwa amri ya mahakama tu ndio mtu mwengine anaweza kufanya lolote kuhusiana na account ya mtu mwengine.

Hata hivyo nashkuru baada ya kufuatilia mambo ya mirathi, nilikuta mzigo bado upo kwenye account.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo dogo hajajengewa msingi wa kujitegemea na ukute kutokana na hilo ndio maana hata kaporwa maana kama kwenda bank tu mpaka asaidiwe sishangai hata kuporwa hilo begi.

Mbona bank wapo faster hata ukipiga simu mwenyewe tu wanaifunga kikubwa wanakuuliza maswali ikiwa pamoja na nambari yako ya simu na akaunti na kama umepiga kwa namba husika faster.
Nafikiri mzee nd'o alikuwa anamjengea msingi wa kujitegemea kijana wake kwa kumtrust aende benki . Kwa upande mwigine benki walikuwa sahihi , maana wakiruhus mtu mwingine atoe taarifa itakuwa hatari maana tukitofautiana na mwenzangu wa ndoa au watoto wakorofi wanaweza kutumia huo mwanya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maadhali palishakuwa na shaka ingekuwa vyema NMB kuizuia kwanza kisha kuwasiliana na mhusika.
Lilikuwa linawezekana na kwa urahisi Zaidi kama angekwenda muhusika mwenyewe lakini si kwa 3rd person. Who knows, labda aliyeleta taarifa anataka kufanya yake kwenye akaunti lengwa lakini ili afanye hayo yake inabidi akaunti iwe kama haisomi.

Uliza kwenye makampuni ya simu namna ambavyo watu huwa wanapigwa kwenye simu zao kwa kuzi-deactivate kwa muda mfupi tu.

Halafu sitaki kuamini kama aliyeibiwa alishindwa kuwa hata na mawasiliano ya huduma kwa wateja wa bank husika. Yes anaweza kusema namba alikuwa hana, lakini kama mleta mada ameweza kuleta hii mada humu, manake ana smart phone, kwenye google naamini angepata namba na mpaka matawi ya hiyo bank.

Tena namshauri aliyetumwa (kama yupo humu) next time jumba bovu litakuja kumuangukia.
 
I

Ingekua busala zaid km ofisa bank angetumia sim kumpigia mteja husika kutokana na kuibuka mtu kati kuhusu Account yake.
Km cm ni miongoni mwa vilopotea bas wangemshar kuenda tawi lililo kalbu naye kwa mlolongo uleule (Impitie)

Yes inafaa kufanyika hivyo na ni sahihi kabisa kwa ofisa kuconfirm. Lakini ukumbuke kama aliyekwenda pale, kama nimeelewa sawa, si yule aliyeibiwa. Manake kama aliyeibiwa hivyo vitu vyote vikiwamo na simu aliweza kufanya mawasiliano na mleta uzi hapa jamvini na kumuelezea yaliyotokea, kitu gani kilifanya ashindwe kuwasiliana na bank tajwa??

Sina hakika sana na hao wezi wapo smart kiasi gani mpk ndani ya muda mfupi kuweza kupata taarifa za siri za kufanya miamala kwa uharaka ule.
 
Back
Top Bottom