Nimesikitishwa sana na uzembe ambao Maofisa wa NMB- BANK HOUSE wameufanya na kusababisha wezi waliopora begi la kijana wangu pamoja na kadi ya Bank ya NMB wapate mwanya wa kuiba hela kwa kupitia kwenye ATM. Tukio lenyewe ni kuwa jana tarehe 27/02/2020 muda wa asubuhi kijana wangu aliporwa begi ambalo ndani yake kulikuwa na simu pamoja na kadi ya Bank.
Hivyo baada ya kunijulisha uporaji huo mara moja niliwasiliana na mtu ambaye alikuwa karibu na tawi la Bank ya NMB ili aweze kutoa taarifa za awali ili kuzuia wahalifu hao wasiweze kutumia hiyo kadi hiyo. Nilimpata mtu na kaenda moja kwa moja mpaka NMB bank house ambapo alikutana na maofisa ambao mmoja wao alikuwa tayari kusaidia, hata hivyo wakati anaendelea kujaribu kuzuia miamala isifanyike inasemekana alitokea afisa mwingine wa bank na kumueleza Afisa aliyekuwa anaendelea na zoezi la kufunga miamala kuwa hairuhusiwi mtu mwingine kutoa taarifa Bank ya kufunga miamalla isipokuwa mhusika mwenyewe hivyo ikaelekezwa kuwa lazima mwenyewe akatoe taarifa. Jambo hili limesababisha uzembe mkubwa kwani wezi hao wameweza kutoa hela bila wasiwasi wowote.
Nashauri uongozi wa NMB waangalie baadhi ya taratibu ambazo hazina msingi katika usalama wa hela za wateja. Hakukuwa na sababu yeyote ya kupuuza taarifa za awali ilitakiwa kukubali taarifa na kuzifanyia kazi. Hili jambo kwa kweli limenisikitisha sana maana endapo mwenye akauti yupo hospitali au amekufa n.k itakuwaje? hizi ni kanuni mbovu kwenye usalama wa fedha za watu, sasa mmekataa na pesa zimeibwa kipi bora?