NMB wamekataa kupokea taarifa ya kuzuia miamala baada ya kadi ya benk kuibiwa matokeo yake wahalifu wamefanikiwa kutoa pesa

Nadhani kanuni zao ni hovyo kabisa. Maana kuzuia miamala isitoke haina madhara kwa Bank na kwa mhusika pia maana ni tukio ka dharura na la muda mfupi ili kuzuia jambo baya lisitokee.
Kama wangekubali kufanya uliyotaka kufanya binafsi ningewashangaa sana na kuona hawana weledi wa kazi.
Wao walikuwa na hakika gani kama wewe au huyo ndugu yako kaibiwa??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
What if mtoa taarifa akitoa taarifa za uongo ili kumkomoa mwenye akaunti ili asifanikishe jambo fulani kama safari,manunuzi au kusababisha usumbufu tu??? Au umeangalia upande mmoja tu?

Namba ya siri ya mwenye kadi wahalifu waliitoa wapi? Anold,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua ni vema ukatumia akili ingalau kidogo ili kujibu, taarifa za awali ni muhimu kama uhalifu unatokea, mtu aliyetumwa kutoa taarifa alikuwa na vitambulisho, alikuwa namba za mmiliki wa kadi kikubwa ni kujiridhisha, kwa hiyo kutoa taarifa za kuzuia uhalifu usifanyike dhambi? ndiyo maana afisa wa kwanza alikubali baada ya kujua uharaka na umumu.
Nawe umetumia akili hapa???
Vipi kama wangefunga kumbe aliyetoa taarifa kaamua tu kusema ifungwe ili kukukomoa si ungelalamika wamefunga akaunti bila idhin yangu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnao mdiss jamaa kua hao wezi wamepataje password its easy kuna maduka sasa iv yanamashine unalipa kwa kuswipe pia manunuzi ya online china ya dolla 100 yanafanyika bila ata password just number ya card na namba flani ipo nyuma ya mastercard ..kodnumber...
So jamaa nachoeleza ni sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
Weee hata bank inaonyesha hukufaham?
Eti bila password yaan hata buku watakutaka nywila

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao wezi walijuaje Password ya kijana wako?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hao sio wezi ni wadai wake, amekopa mahali halafu kulipa analeta miyeyusho anazuga hela zipo kwenye kadi hana cash. Wamemtaitisha wakampora na kadi bila shaka ni Bar hapo hamna namna watu wameenda kujilipa ATM.

Mfunze mwanao "Dawa ya kukopa ni kulipa sio kuleta maneno mengi"
 
Kama wangekubali kufanya uliyotaka kufanya binafsi ningewashangaa sana na kuona hawana weledi wa kazi.
Wao walikuwa na hakika gani kama wewe au huyo ndugu yako kaibiwa??
Acheni upuuzi......ndio maana kuna kitu inaitwa KYC .....bank wanatakiwa wawe na uwezo wa kuwasiliana na mteja wao incase kuna ishu yeyote ya tofauti....wangempigia simu ili kuhakiki taarifa wanazopewa...
 
Simu nayo iliibiwa pamoja na kadi hivyo haikuwa hewani
 
Acheni upuuzi......ndio maana kuna kitu inaitwa KYC .....bank wanatakiwa wawe na uwezo wa kuwasiliana na mteja wao incase kuna ishu yeyote ya tofauti....wangempigia simu ili kuhakiki taarifa wanazopewa...
Upuuzi ni nini?? Upuuzi ni leo wewe ukurupuke kwenda bank tu kwa sababu labda unanifahamu na umeona nikiibiwa na kuwaambia watu wa bank wafunge kadi yangu.
 
Anold, Kwanza poleni. Pili, mwenye kadi hakuwa na pin code? Pin code huiandiki mahali, unatunza kichwani.
 
Unajua ni vema ukatumia akili ingalau kidogo ili kujibu, taarifa za awali ni muhimu kama uhalifu unatokea, mtu aliyetumwa kutoa taarifa alikuwa na vitambulisho, alikuwa namba za mmiliki wa kadi kikubwa ni kujiridhisha, kwa hiyo kutoa taarifa za kuzuia uhalifu usifanyike dhambi? ndiyo maana afisa wa kwanza alikubali baada ya kujua uharaka na umumu.
Benki sio wajinga. Hao wezi wa begi walipataje nywila? Endapo wangekubali kufunga akaunti kwa taarifa yako hata mimi ningeshangaa sana. Anayetakiwa kutoa taarifa ni mwenye kadi na sio vinginevyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiwa siku umelazwa ndiyo utajua kwanini huwezi kiuondoka kwenye drip uende bank badala yake utatuma mtu wa karibu
Ni ujinga ku disclose password. Mwambie kijana wako yeye ni mjinga sana, ameshindwaje kukariri tarakimu nne tu za nywila? Kadi hata uibiwe sasa hivi, sio jambo rahisi kuiba fedha bila password kuwa nayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanamhudumia mtu kulingana na maelezo aliyokwenda nayo, yeye alikwenda kumwakilisha mtu ambae hajapigwa (tena mwakilishi wa mwakilishi maana kijana wake ameibiwa alafu na yeye tena ametuma mtu mwingine kumwakilisha ambae huenda hata maelezo ya msingi ya mwenye akaunti hana kama majina yote matatu, namba ya simu na hata umri, huenda ameulizwa akabaki na kigugumizi)

Pia huhitaji loss report kwa kuwa kinachohitajika ni wewe kuifunga kwa muda ili taratibu zingine zifuate za loss report etc na hata simu inatosha kama wangemsaidia kupiga simu alafu angetoa maelezo kutokana na maswali ambayo wangemuuliza

Hakuna hekima na busara hapo kwa kumsikiliza mtu asiehusika na akaunti, je kama kuna watu wamekuja kufanya figisu kuifunga ili jamaa akienda kuchukua hela akwame labda kuna sehemu anatakiwa baada ya masaa 2 apeleke fedha kwa ajili ya maombi ya tenda flani sasa wapinzani wake wamewahi ili kumfanyia figisu ili ashindwe kupeleka tenda kwa wakati na kupunguza ushindani?

Kuna namba ya simu kwenye card za benki bahati mbaya wananchi hawapendi kuzichukua na kuzi-save yaani ukiibiwa card au kupoteza huhitaji nguvu nyingi zaidi ya simu ambayo ni bure
Well said

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mazingira mwenye akaunti hawezi toa taarifa... mfano, akifanyiwa jambo hilo huku yupo eneo lisilo na tawi lao inakuwaje..???

Je akifanyiwa uharifu hadi akapoteza kumbukumbu, hilo ulosemalo linawezekanaje..?? Kuwe na namna kutoa taarifa kwa emergence... ni bora kufunga halafu ije ifunguliwe kuliko kugoma kufunga halafu watu wakakomba hela
Kwa emergency unatakiwa kupitia polisi mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom