NMB wamekataa kupokea taarifa ya kuzuia miamala baada ya kadi ya benk kuibiwa matokeo yake wahalifu wamefanikiwa kutoa pesa

dogo kaibiwa akashimdwa enda benki mwenyewe aya sawa akakupa taarifa ukashindwa mshauri alatoe taarifa benki kuzuia miamala
Aya nayo ngumu ukashindwa ww kwenda ili ufosi king

sawa ukamwambia jirani akajikongoga akaenda akapata hayo majibu, akakupa taarifa ukashindwa enda tena wala kumtuma muhusika aende unakaa kusubiri yatokee ya kutokea ulaumu

nmb walikuwa sawa ww ndo mzembe
Huyo dogo hajajengewa msingi wa kujitegemea na ukute kutokana na hilo ndio maana hata kaporwa maana kama kwenda bank tu mpaka asaidiwe sishangai hata kuporwa hilo begi.

Mbona bank wapo faster hata ukipiga simu mwenyewe tu wanaifunga kikubwa wanakuuliza maswali ikiwa pamoja na nambari yako ya simu na akaunti na kama umepiga kwa namba husika faster.
 
Unajua ni vema ukatumia akili ingalau kidogo ili kujibu, taarifa za awali ni muhimu kama uhalifu unatokea, mtu aliyetumwa kutoa taarifa alikuwa na vitambulisho, alikuwa namba za mmiliki wa kadi kikubwa ni kujiridhisha, kwa hiyo kutoa taarifa za kuzuia uhalifu usifanyike dhambi? ndiyo maana afisa wa kwanza alikubali baada ya kujua uharaka na umumu.
Huo sio utaratibu mkuu usilazimishe alitakiwa aende mwenyewe tena mara tu baada ya kuibiwa na kama haitoshi hata kama mngemsaidia kwa kuazima simu na kupiga huduma kwa wateja wangemuuliza maswali mawili matatu kama namba ya akaunti na detail zingine kama namba ya simu na wangeizuia kwa muda ila wangemwambia afike ofisini pia.

Pia kupitia kwenye simu janja aka smartphone kuna option ya kuandika email kwenda NMB bank hivyo kupitia email address yake ambayo ameiandika wakati anafungua akaunti angeweza kutuma email kwa kutumia simu yako alafu angewapandia hewani.
 
Hivi sheria hazitakiwi kupinda hata kidogo?
Unaweza kupindisha sheria sehemu yenye Opportunity na sio Threat!!! Kwa mfano, benki zote duniani zina the so-called KYC; yaani Know Your Customer!! Ndo pale kabla ya kufungua akaunti utaambiwa upeleke a valid ID Card, recent Photos and probably na barua! Nchi zingine watakuambia upeleke proof of address.

Now here is a thing! Assume nipo pale Kaunta ya CDRB, saa moja au mbili kabla ya benki kufungwa, unaingia pale ukiwa na 200M na unataka kufungua akaunti! Nakuuliza ID; huna! Barua; huna! Picha; huna! Nakuuliza umetoa wapi pesa, unajibu ni mgao wako wa urithi na umeamua kuleta pesa benki kwa sababu usingependa kukaa na pesa nyingi ndani!

Je, nitakuacha uondoke na pesa wakati benki ina-struggle kupata deposits za kutosha?!!! The answer is NOW WAY, siwezi kukuacha uondoke nayo kwa sababu nikikuacha uondoke nayo si ajabu hutarudi nayo tena hapo benki!!! Kwa mazingira kama hayo nitakufungulia akaunti kwa masharti ya kuhifadhi pesa yako lakini HUTARUHUSIWA kuichukuwa hadi utakapoleta viambatanisho vinavyotakiwa na benki!!

Hapo nitakuwa nimepinda sheria lakini kwa sababu kuna fursa nimeiona!! Lakini mtu anaibuka from nowhere na kutaka akaunti fulani iwe blocked nami nimuamini kisa tu ana akaunti namba; NO WAY!
 
Mleta mada natamani nifanye biashara ya ushirika na wewe, halafu tufungue Joint Account!! Siku kadi ikiwa kwenye mikono yangu, naibiwa begi na simu halafu nakupigia simu kwamba nimeibiwa begi na kadi yetu ilikuwa kwenye begi!!

But wait, machale si yanaweza kukucheza na kukutuma uende benki kuuliza pesa imetolewa kwenye ATM ipi na hivyo kuomba uoneshwe CCTV Footage za muda ambao transaction imefanyika?! Mbona CD ya hii simulizi inanasa sana kwa upande wangu?! Na kama simulizi yote ni kweli basi huyo kijana wako anastahili kuvikwa taji la wazembe kwa mwezi wa Februari.
 
Mnao mdiss jamaa kua hao wezi wamepataje password its easy kuna maduka sasa iv yanamashine unalipa kwa kuswipe pia manunuzi ya online china ya dolla 100 yanafanyika bila ata password just number ya card na namba flani ipo nyuma ya mastercard ..kodnumber...
So jamaa nachoeleza ni sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnao mdiss jamaa kua hao wezi wamepataje password its easy kuna maduka sasa iv yanamashine unalipa kwa kuswipe pia manunuzi ya online china ya dolla 100 yanafanyika bila ata password just number ya card na namba flani ipo nyuma ya mastercard ..kodnumber...
So jamaa nachoeleza ni sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio wanamdiss ila ameleta mada kizembe sana na anataka bank wamkubalie kufunga akaunti ambayo sio yake, alichotakiwa aombe msaada ni hatua gani za kuchukua endapo nimeibiwa fedha zangu kwenye ATM japokuwa maelezo yake yanaonyesha huyo dogo mzembe maana begi limeibiwa ambapo ndani kulikuwa na ATM Card na simu ambapo password ya ATM card ilikuwa ndani ya simu ambayo hiyo simu bila shaka ilikuwa haina password alafu anaanza paragraph ya kwanza kwa kuwaita NMB wazembe kumbe uzembe upo kwake na dogo kwa kushindwa kutoa taarifa mapema maana hata kwa simu tu bank wanasikiliza

Kwahiyo hawajatumia hiyo mbinu unayosema ya kutumia zile number zilizopo nyuma ya card pamoja na CVV
 
Kwa mnaosema angeenda mwenyewe, lets say muhusika kapigwa hadi kupoteza fahamu, je asubiriwe hadi azinduke? Na huo muda wakutafuta Loss Report wezi watakuwa wanakusubiri?!

Kuna Sheria halafu kuna Hekima na Busara.
 
Mkuu benki wapo sahihi pole,ungepiga huduma kwa wateja hata bila kufika benki ungesaidiwa

Lakini kwa upande wa benki walipaswa wawe suspicious,mtu anakuja kutoa taarifa ya wizi kuhusu akaunti ya mteja wenu,hata kama hawatablock ilipaswa wamtafute mteja wao maana simu wanazo wamuulize kama ana taarifa hio

Lakini kwa sababu ni wanafanya kwa mazoea wakasababisha mteja wao kaibiwa kizembe.

Unaachaje mtu kama huyu anaondoka kizembe bila kujua lengo lake?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mnaosema angeenda mwenyewe, lets say muhusika kapigwa hadi kupoteza fahamu, je asubiriwe hadi azinduke? Na huo muda wakutafuta Loss Report wezi watakuwa wanakusubiri?!

Kuna Sheria halafu kuna Hekima na Busara.
Wanamhudumia mtu kulingana na maelezo aliyokwenda nayo, yeye alikwenda kumwakilisha mtu ambae hajapigwa (tena mwakilishi wa mwakilishi maana kijana wake ameibiwa alafu na yeye tena ametuma mtu mwingine kumwakilisha ambae huenda hata maelezo ya msingi ya mwenye akaunti hana kama majina yote matatu, namba ya simu na hata umri, huenda ameulizwa akabaki na kigugumizi)

Pia huhitaji loss report kwa kuwa kinachohitajika ni wewe kuifunga kwa muda ili taratibu zingine zifuate za loss report etc na hata simu inatosha kama wangemsaidia kupiga simu alafu angetoa maelezo kutokana na maswali ambayo wangemuuliza

Hakuna hekima na busara hapo kwa kumsikiliza mtu asiehusika na akaunti, je kama kuna watu wamekuja kufanya figisu kuifunga ili jamaa akienda kuchukua hela akwame labda kuna sehemu anatakiwa baada ya masaa 2 apeleke fedha kwa ajili ya maombi ya tenda flani sasa wapinzani wake wamewahi ili kumfanyia figisu ili ashindwe kupeleka tenda kwa wakati na kupunguza ushindani?

Kuna namba ya simu kwenye card za benki bahati mbaya wananchi hawapendi kuzichukua na kuzi-save yaani ukiibiwa card au kupoteza huhitaji nguvu nyingi zaidi ya simu ambayo ni bure
 
Mnao mdiss jamaa kua hao wezi wamepataje password its easy kuna maduka sasa iv yanamashine unalipa kwa kuswipe pia manunuzi ya online china ya dolla 100 yanafanyika bila ata password just number ya card na namba flani ipo nyuma ya mastercard ..kodnumber...
So jamaa nachoeleza ni sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo dogo kacheza muvi nzuri sana hivi ni mwizi gani anapata hadi akili yakujua password ipo kwenye simu hii haijawahi kutokea
 
Back
Top Bottom