NMB na CRDB

Ndikwega

JF-Expert Member
Feb 1, 2012
5,989
2,000
Ndugu zangu wana JF ukisikia Bank za kipumbuvu katika kuajili wafanyakazi wake ndiyo hizi mbili, kwa mtazamo wangu ni Namba moja.Leo nitaielezea moja nayo ni NMB.

Hawa jamaa Namuomba Mungu Kama vp uongozi wa Highlands Zone walaaniwe na mabaya yawe juu yao. July,2012 walitangaza ajira zao kwa kubandika tangazo kwenye mti hapa ofisi zao Mbalizi Road Mbeya ambapo ndiyo makao makuu ya Highlands zone. Mimi na jamaa yangu tuliandika barua kwa kufuata viwango vya barua za ajira, namimi nina alama nzuri za kufaulu kuliko jamaa yangu katika kila hatua ya shule. Mwenzangu akatangulia kupeleka Maombi ya kazi lakini hukuambatanisha na cheti cha kuzaliwa, mimi nilivyopeleka mpokeaji akaniambia ambatanisha na cheti cha kuzalia, ikabidi nirudi kuchukua na kuambatanisha. Sasa jamaa yangu wala hakuambatanisha,Nadhani Siku ya Kupitia hayo maombi wakampigia simu alete hicho cheti na akaitwa kwenye usaili na kazi akapata, mimi hata kuitwa usili hawakuthubutu.

Swali: Hawa jamaa huwa wanatangaza kazi kwa ajiri ya kufurahia tunavyohangaika kuomba hizo nafasi au ili iwaje?Na ukweli ni kuwa huyo jamaa yangu kaka yake yupo hapa hapo hapo mbeya na anafahamiana na hawa wa NMB na ndiye alifanya mpango mzima.
Nilikuwa najaribu kuwajuza kuwa msione kwanini hamwitwi kwenye usaili na hali huku walitangaza na mliomba wanatuzuga tu hawa. HAKIKA WALAANIWE NA MWENYEZI MUNGU WENYE TABIA HIZI.
 
MMOJA

JF-Expert Member
Aug 30, 2012
441
250

Pole sana ndugu
 
ndomyana

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
4,953
2,000
Mhh makubwa pole sana kijama, nenda rungwe kalime maparachichi au rudi kyela kalime matikiti
 
Ndikwega

JF-Expert Member
Feb 1, 2012
5,989
2,000
Utakomaa vipi ndugu labda unishauri, sina ndugu yangu mwenye nafasi kubwa huko kazini na hali ndiyo kama hii hamna pesa japo rushwa ni dhambi hata vitabu vya Mungu vimeangikwa.
 
King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,794
2,000
Cheti si uwezo baba. Huenda mwenzio alijibu kwa ufasaha maswali yote kushinda wewe na gpa yako. Siku hizi unaangaliwa uwezo na sio vyeti. Umenikumbusha forum flani, facilitators 5, mmoja wa USA, holland, uganda, kenya na mtz 1. Wote wana digrii moja moja ila mtz tu ndo ana phd. Akisimama kupresent mada unataka kuingia chini ya meza kujificha. Hata intern mkenya ana nafuu.
 
kelvinkipeta

Senior Member
Feb 17, 2012
108
195
huo ni ujinga wamajamii mnasapoti ujinga et usipojulikana haupati kazi.tupige vita kwa kuanika upuuzi kama huo kwenye media na hata kwenye mitandao ya kijamii ikiwezekana hata kwa kutaja majina ya wanaofanya ivo ili kuondoa huo ujinga.sasa tunasoma ili iweje....acheni kusapot ujinga,na wewe unaesapot nina uhakika ni kilaza sana wewe.usitumie hii forum kusapot ujinga haikusaidii lolote,tushauriane nini tufanye kukomesha ujinga wa namna hyo.
 
mwila

Member
Oct 17, 2012
38
0
Utakomaa vipi ndugu labda unishauri, sina ndugu yangu mwenye nafasi kubwa huko kazini na hali ndiyo kama hii hamna pesa japo rushwa ni dhambi hata vitabu vya Mungu vimeangikwa.
pole sana ndugu,ila ninyi wenye ma GPA mara nyingi darasan huwa hamna ushirikiano wa wenzenu, na hivi mnajiita vipanga basi bize na daftari bize na vitamu!! Kuna muda wa kujichanganya, muda wakujichanganya watu wanakuona unatengeneza marafiki au kwa kingereza network, sio wewe serious serious na wewe unadhan ukirudi mtaan atakushika nani mkono?? Kazi za benk mara nyingi wanao ajiriwa wanakuwa wanafahamiana either na baadhi ya wafanyakazi ili ku identify vizuri tabia za mtu watakao mwajiri, mara nyingi hizo benki hawakuchukui kama hakuna mtu anayekufahamu, wanaogopa kuibiwa hela mpaka knowledge yao!! Pole usijari, mtumie huyo rafiki yako kuingia hapo, usianze kuonyesha chuki, ajira ngumu sana siku hizi!! One love!!
 
Criterion

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
11,473
2,000
Pole sana kwa kutokuitwa na Bank. Wewe usilani. Endelea kutafuta kazi, siku moja utapata wala usikate tamaa. Kazi inapotangazwa, mara nyingi wanaotuma maombi ni wengi ukizingatia kwamba wenye sifa na wanaohitaji kazi ni wengi. Mwajiri hawezi kuita wote kwa interview. Hivyo hu short list. Na hata wanaofanya interview kama ni wengi zaidi ya nafasi zilizopo hawawezi kuchukuliwa wote. Watachukuliwa kulingana na nafasi zilizopo.

Unapoomba kazi, utegemee lolote. Ila usitukane wala kulaani unapokosa kwa sababu kama huyo mwajiri mtarajiwa amethibitisha kwako kwamba utamaduni wake ni wa chini ya meza, na wewe kama si wa hivyo, hata ungeitwa pengine angekuona hamfanani na angekuacha. Hata bahati akuchukue, pengine kazini mgeshindana kwa tofauti hizo.

Vumilia, endelea kuomba kazi sehemu zingine. Ukipata mshukuru Mungu, na ukikosa pia angalia ulikotoka kwa shukrani na uangalie mbele kwa matumaini. Ila upunguze jazba na hasira ili usiogopeshe waajiri na pia uweze kutunza kazi yako utakapopata.
 
SG8

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
3,926
2,000
Sijaelewa CRDB hapa wameingiaje? Maana kwenye maelezo yako umezungumzia NMB Mbalizi Road...Pengine ndio hapa alipokushinda jamaa yako... Alikuzidi ujanja kwenye interview...alama za kwenye vyeti hazisaidi chochote
 
Donne

Member
Nov 29, 2012
6
20
Watanzania bwana hamna hata jipya! hivi mimileo nataka kutoka kwenye ajira nianze kuwa mkulima hata huko kyela wewe unataka kuajiriwa, Tena uwe banker acha upuuzi huo umepitwa na wakati.kuwa mjasilia mali kaka
 
Syakafwa

Member
Nov 30, 2012
10
0
Ndugu tunatofautiana sana kwa vitu vingi. una gpa nzuri umekosa quality zingine. usisafirie nyota ya mwenzio subiri nawe utapata kampuni linalo-consider zaidi gpa. chamsing ni kutokata tamaa, wote tunatafuta ila tunashukuru mwenzetu akipata coz jam ya majobless inapungua hivo jua siku yako inakaribia.
 
gambagumu

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
1,082
2,000
acha hasira dogo..halafu sio busara kulaani kwani nawe waweza laanika.tulia sio mwisho wa maisha nafasi yako atakupatia Mungu endelea kumwomba acha kutegemea binadamu kwa maana wengi wao wamejaa udhalimu.
 
gambagumu

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
1,082
2,000
kwa taarifa yako tu NMB kuna mtandao unouza kazi na nafasi moja ni tsh1000000 kwa hiyo usishangae.
 
Sunshow

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
1,133
1,500
Siyo vizuri unavyofanya. Hivi huyo rafiki yako akisoma uzi huu atakuchukulia vipi? Inawezekana baadae angeweza kukupa mchongo lakini atakuona hufai. Kuwa na alama nzuri darasani siyo kigezo pekee ndiyo maana kazi nyingine wanataka waliomaliza kidato cha nne au cha sita japo hata mwenye degree angetamani afanye kazi hiyo kulingana na maslahi yake. Kumbuka kupata alama nzuri darasani ni bidii yako mwenyewe LAKINI kazi ni bahati ya mtu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom