Mkuu
laurentie hongera kwa kuwahamasisha raia kuhusu kuzikamatia fulsa zilizopo shamba!
Mimi ni mkulima mzoefu wa mazao karibu yote ya bustani.
Nimesoma na kujionea picha zako ulizo bandika hapa;
Zipo kasoro nyingi sana nimeziona kwenye hili bandiko. Ningependa kuweka masahihisho ya jumla iwe kama tahadhari kwa wale waliovutiwa na huu uzi hatmae kuja kufanya kazi.
1) Ipo kasoro kwenye upandaji wa hizo tikiti. Umepanda kienyeji sana. Upandaji wako utaathiri huo mmea kipindi cha umwagiliaji maji hasa kwa hiyo hybrid(zebra)
2) kuna mapungufu katika uainishaji wa gharama za uendeshaji. Kwanini huwi realistic kuchambua hatua kwa hatua mpaka mavuno.
Nk nk nk
Nikipata muda, ntatoa mchanganuo wa upandaji, cost na kipato halisi kwa ekari moja ya tikiti ili kuwarahisishia watakaovutika kuingia kwenye sekta hii na hatmae wajue mbivu na mbichi kuhusu kilimo.