Njoo tulime tikiti ujikomboe

Inaendelea...
8)Gharama ya spray tank sh 40,000/=

9)Gharama ya mbolea.
Kupandia, DAP sh 70,000 mfuko1 na kukuzia CAN sh70,000 Booster kopo2 za 1litre@12000=sh24000 TOTAL=164,000/-
8) Gharama ya vibarua +ulimaji haitazidi sh150000 mpaka kuvuna.
9)Upandaji na makisio ya matunda mazuri kwa ekari moja.
Eneo la ekari1 ina 4000sqm
Hivyo idadi ya mashimo ni 4000sqm/(2m*1m)=2000.
Idadi ya mashina kkt ekari1 kama utapanda punje2 kila shimo 2000*2=4000.
Ukifanikiwa kutunza matunda mawili makubwa katika kila shina, ekari1 utapata matunda 4000*2=8000.
Kadilio la chini kabisa la bei ya tikiti shambani ni sh1000.
TOTAL YIELD; 1000*8000= SH 8000,000/=
Fuatilia vipengele vyote vya gharama kisha DEDUCT toka kwenye total yeald utapata RETURN ya hii project.
Nyongeza;
Epuka kuspray viuatilifu mida ya asubuhi ili kujenga urafiki na nyuki ambao ndo wahusika wakuu ktk uchavishaji.
Usimwagilie maji usiku kuepuka kulowanisha majani ya tikiti yatashindwa kukauka mapema.

Karibuni kwa maswali.
cc Lizarazu etc
Mkuu mchanganuo mzuri sana..

Ina maana haya maandalizi yote na gharama zake ni kwa heka moja tu?
.
Na vipi mtu anaetaka kufanya cultivation ya nusu heka tu vipi gharama zake zinakadiriwa kuwa kma shingap hivi kwa uzoefu wako?
 
Hichi kilimo cha tikiti kinavutia sana ngoja nijipange vizuri nami niwekeze huko, kazi za kuajiriwa inakuwa kama mtumwa ebo. Hata wanawake tunaweza bwana kukamata jembe

sasa wewe angela ulivyojikobeka hiyo mimekapu utaweza kushika jembe kweli????
 
Naam mkuu ni jambo la heri sana kuona kuna mtu aliyetayari kwa ushirikiano ninao hitaji... kikubwa ni kuwa honesty na kutanguliza utu ukiishinda roho ya tamaa. Siku zote biashara nzuri ambayo hata Mungu ana ibariki ni inayofanyika for equally mutual benefits.

Kama nilivyoweka kwenye mabandiko yangu ya awali, binafsi sina tatizo ni utayari tu wa muhusika. Hivyo fanya unione kwa inbox kwa ajiri ya mawasiliano yenye ukaribu zaidi.
Tupo pamoja mkuu. Kuhusu uaminifu ondoa shaka kabisa make unaenda kufanya kazi na mtu aliyekuwa na utayari wa maksudi na committed one mwenye family na uelewa mtambuka wa kile afanyacho.
Nakuja inbox mkuu...
 
Mkuu mchanganuo mzuri sana..

Ina maana haya maandalizi yote na gharama zake ni kwa heka moja tu?
.
Na vipi mtu anaetaka kufanya cultivation ya nusu heka tu vipi gharama zake zinakadiriwa kuwa kma shingap hivi kwa uzoefu wako?
Maelezo haya nimeyatoa kwa ujumla. Nimeainisha gharama zote ili iwe rahisi kueleweka na kujua mahitaji na vitu vyote kabla hujaingia shamba.
Huu ni uchambuzi unaokata kiu yote na kupunguza queu ya frequently asked questions.
Ukitimiza mahitaji mhimu i.e waterpump and all utilities, gharama nyingine obviously zitapungua zenyewe i.e mafuta, mbegu, nguvukazi, viuatilifu etc.
Kwa nusu eka gharama zitapungua as minimumly as required.
 
Poa mkuu nimekuelewa
 
Tatzo la kuzaliwa na kukulia buguruni kimboka,unakuwa unacopy element zile zile za dada zako pale buguruni shelii-koffi olomide wee

pole, the way you attack the point reflects your level, si kosa lako, pengine umekulia mazingira hayo na ndio maisha unayoishi to this moment
 
Maelezo haya nimeyatoa kwa ujumla. Nimeainisha gharama zote ili iwe rahisi kueleweka na kujua mahitaji na vitu vyote kabla hujaingia shamba.
Huu ni uchambuzi unaokata kiu yote na kupunguza queu ya frequently asked questions.
Ukitimiza mahitaji mhimu i.e waterpump and all utilities, gharama nyingine obviously zitapungua zenyewe i.e mafuta, mbegu, nguvukazi, viuatilifu etc.
Kwa nusu eka gharama zitapungua as minimumly as required.
Kuna maelekezo nimesoma kuwa unachimba shimo la futi 2*2 then unaweka mbegu 5 hadi 6 kwa shimo na distance ya shimo hadi shimo ni futi 12 kwa pande zote,hii imekaaje mkuu?
 
Kuna maelekezo nimesoma kuwa unachimba shimo la futi 2*2 then unaweka mbegu 5 hadi 6 kwa shimo na distance ya shimo hadi shimo ni futi 12 kwa pande zote,hii imekaaje mkuu?
Umetumia kilevi gani mkuu?!
Kamuulize aliyeandika hayo maelezo atakuwa na ufafanuzi wa kutosha.
Hili sio jukwaa la mizaha, kama huna cha kuchangia, pita kimya tu kuliko kujaza ukurasa kwenye thread ambayo wengine wangepata taarifa mhimu mapema kadri ya uhitaji wao.
 
Soma taratibu uelewe mkuu...
 
Umetumia kilevi gani mkuu?!
Kamuulize aliyeandika hayo maelezo atakuwa na ufafanuzi wa kutosha.
Hili sio jukwaa la mizaha, kama huna cha kuchangia, pita kimya tu kuliko kujaza ukurasa kwenye thread ambayo wengine wangepata taarifa mhimu mapema kadri ya uhitaji wao.
Am here 2 learn mkuu,kama kuna unalojua nieleweshe! Read this Watermelon
 
Sihitaji kuelewa chochote mkuu maelezo yangu nimeshabainisha. Sasa kama hicho unachoomba kueleweshwa kipo ndani ya maelezo yangu, basi kichukue kama kilivyo.
Nilihitaji kupata mawazo yako kama mkulima mzoefu wa zao hili na sio kubishana na wewe! Sometimes its good 2 learn new things/technics!
 
Sihitaji kuelewa chochote mkuu maelezo yangu nimeshabainisha. Sasa kama hicho unachoomba kueleweshwa kipo ndani ya maelezo yangu, basi kichukue kama kilivyo.

Mkuu wewe unalima hasaa sehemu gani kwa haoa dar es Saalam au mashamba yanapatikana hasaa wapi??maana nataka nianze kwanza na hekari 3 nione matokeo yake....
 
Sihitaji kuelewa chochote mkuu maelezo yangu nimeshabainisha. Sasa kama hicho unachoomba kueleweshwa kipo ndani ya maelezo yangu, basi kichukue kama kilivyo.

Mkuu nimesoma maelezo yako kuna vitu nimenote down. haya ni maswali yangu ambayo nimebaki nayo baada ya kusoma point na maelezo yako.

1. Umesema unaweza mwagilia mche kwa siku tatu kwa wiki na matikiti yakawa mazuri mwisho wa siku. Je unaweza ainisha mche mmoja wa tikiti unatakiwa upate maji kiasi gani kwa wastani kwa siku (katika hizo siku 3 kwa wiki ulizoainisha).?

2. Kuna post moja umemjibu mtoa mada kuwa baada ya siku 56 unaweza acha kumwagilia tikiti ili liweze imarika vyema. Hapo hapo katika maelezo yako umesema baada ya siku 75 hutakiwi kumwagilia kwa ajili kuepusha tikiti kupasuka kutokana na kuzidiwa maji. Je kati ya hayo lipi ni sahihi.?

3. Unaweza kutuainishia mchanganuo wa upuliziaji dawa na mbolea.? kwamba lini ama baada ya siku ngapi kipi kifanyike ( Hapa ni katika case ya kupulizia dawa na mbolea ).?

4. Katika yooote niliyopata kupiga stori na wadau ambao wamelima tikiti. Wote kwa nyakati tofauti wamenitahadharisha na mvua kubwa katika kipindi cha cha siku 10 za mwisho. Kwamba ikitokea matikiti yamepigwa na mvua katika wiki ya mwisho, basi kuna uwezekano mkubwa matikiti yakaharibika. Je hii ni kweli kutokana na uzoefu wako.?

Shukrani
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom