INTROVERT MAN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2019
- 993
- 1,337
HI THERE, MAISHA YANGU
Mahusiano, Muziki, Depression, hustles, & Happiness.
Habari wakuu wa jamiiforums,
Heshima kwenu.
Kuna msemo mmoja wa Kiingereza unasema " if a street performer make you stop walking, you owe him a buck"
Basi kupitia hadithi za ukweli nilizozisoma humu basi nami ninawiwa kuileta yangu kwani uhalisia wa maisha waliyopitia baadhi ya walioleta story zao humu kama mzee Akili Sina , Analyse, UMUGHAKA na wengineo wameni inspire na mimi nilete story yangu. Sababu kuu ya kuandika ni kwamba napenda kuandika sana na hao wanaJF wananidai coz nimejifunza vitu vingi toka kwao.
Nikisema nimepitia labda maisha magumu nitakuwa nakufuru. Nimepitia mambo ya kawaida ila natoa maangalizo mapema lakini binafsi nimepitia mitihani iliyokuwa migumu kulingana na umri wangu na pia issue ya kuhandle kitu ambacho ndio unaface kwa mara ya kwanza katika life. Hii ni kwa kila mtu hapa duniani. Kinachokuja ku matter hapa ni kwamba kiwango cha maumivu experienced by brain ni sawa hata kama ni mapito ni tofauti.. Nasema hivi mapema kwani isije ikafika huko kwenye comment yakaanza mashindano ya shida oh wewe umepata tabu gani? sisi ndio tumeptia shida. Ok kama mimi kula andazi moja asubuhi kwangu ni tabu afu kwako ni bless haina noma kumbuka kuna wengine breakfast ni draft za madikodiko.
Classes zipo hadi mbinguni so duniani tu haziepukiki. Kuna malaika wakuu na malaika wa kawaida. Kuna malaika wako jehanamu wanageuza watu waungue vizuri. . Kuna wengine wanazunguka katika kiti cha enzi.
Hivyo tu.
Msitishwe na nilivoandika heading hapo kuna neno muziki mkajua mimi ni mwanamuziki hapana. Me ni napenda muziki kuusikiliza sana. Hata hii stori nimeweza kuandika vizuri kutokana na kupata nostalgic memories kutokana na nyimbo fulani fulani hivi.
UZI HUU NIMEANDIKA KWA NOTE BOOK YA SIMU SO MSIJARI NI UMEKAMILIKA FROM A TO Z. YOU HAVE NOT TO WORRY. NITAKUWA NA PANDISHA KIPANDE KILA JIONI. ni mwendo wa kupaste tu. Au mods mnasemaje??.
TAFADHALI KAMA UTAUNGANISHA DOTS NA UKANIJUA BASI FANYA UVUNGE KIMYA KIMYA KAMA UMEKUTANA NA JESHI LA VIBWENGO. UVUNGE KABISA.
Here we go.
1. BAADA YA KUMALIZA FORM FOUR NA KWENDA ADVANCE.
Nilivomaliza form four basi nilirejea nyumbani kwa mama angu ambae anaishi nje kiasi chake toka kwenye mji fulani. Sababu ya kurudi kule ni kwamba kulikuwa na fursa ya kazi kwa kijana mdogo kama mimi kufanya manual labour kwenye mashamba ya zao fulani la kibiashara.
Nilirudi kwa mama tokea shule iliyokuwa mjini. Nilirudi kilazima japo sikupenda kurudi kule nilitamani kukaa kwa ndugu yangu mjini.
Kilichofanya nirudi kule ni msiba wa bamdogo aliyefariki 26/December so tulivozika wanafamilia wakanipiga pin nisirudi. Aiseee nilichukia sana. Lakini nashukuru Mungu ni kwamba kurudi kule kijijini ni ilikuwa baraka kubwa sana kwangu. Kulifanya nikakua kiakili kiasi chake.
Basi msiba ukaisha. Basi mama ambaye ni mjane na anaishi peke ake kutokana na kuwa watoto wote tumetawanyika kusaka maisha na sisi huku wa mwishoni ndio tunasoma basi alishukuru me kuwepo pale kama mtoto wa kiume kusaidia majukumu mengine ya home hata kumuondolea upweke.
Mama akasisitiza nikaombe kazi kwenye kampuni kubwa ya kilimo ambayo iko karibu na kijiji. Kishingo upande nikakubali. Nikaomba msaada wa watu jinsi ya kujiandaa na vitu gani yaani passport na kitambulisho chochote. Mama alinipa elfu tano kwa ajili ya kupiga paspoti size. (Kijijini ni gharama kubwa).
Baada ya kujiandaa basi Jumatatu huyo ya mguu safari ya km mbili mpaka katika ofisi ya hiyo kampuni.
Mdogo mdogo huyo asubuhi mama aliniandalia chai. Nikanywa vizuri nikaondoka. Kipindi hicho nilikuwa namiliki kisimu fulani hivi nokia navigation cha button. Kilikuwa na Internet kupitia opera mini na storage kiasi chake. Hako kasimu kalinisave sana. Basi huku nikitembea nilikuwa nasikiliza wimbo wa post to be wa marion ambao mwaka ule ulikuwa hot sana bila kusahau wa Kid ink show me ft chris brown
Basi nikafika ofisini wakaniandikisha kazi. Uzuri ni ulikuwa msimu wa kuajiri. Niliripoti tarehe 7 mwezi wa kwanza. Wakanipa number yangu kuwa kesho nifike nayo kwa head man katika division niliyopangiwa. Kumbuka kampuni ina division kibao zenye maekari ya kutosha.
Kazi yenyewe ni uvunaji na me sina experience sana dah nikaona hii hatari. Lakini nikakumbuka ya kuwa kuna shamba jipya linatengenezwa yaani ndani ya virgin forest umefumuliwa so wanataka kupanda miche mipya.
Huko ndiko vijana wengi wanapenda na ni kazi ya kulipwa kwa siku yaani 5,400/= ila mshahara kutoka mwisho wa mwezi. Wazee na watu wazima hawapendi huko ila wao wanapenda uvunaji. So kwa kuwa kule kuna vijana afu kuna wanangu wengi wa kijijini kwetu na waliomaliza form four wapo kule basi nikaona hapa ndio penyewe.
Na uzuri ni kuwa hilo shamba jipya ni pua na mdomo na kijijini kwetu kuliko huko division nilikopangiwa na nikikumbuka uvunaji ndio siwezi.
Nikatoka ofisini nikaamua nipitie shamba jipya siku ile ile. Kumbe headman wa shamba jipya ni brother fulani kasoma na sister angu afu ni mwana balaa. Akanisalimia chapu akaniuliza kwa kilugha dogo na wewe kazi utaweza nikasema sana. Nikamuambia nimetoka ofisini ila uvunaji siwezi ndio maana nimekuja huku.
( Kiukweli mimi jembe ninapiga sana hata shule nilikuwa nalima na pia nilikokuwa nakaa mjini tuna mashamba na vinyungu so kulima nilikuwa napiga hatari mpaka leo hii ninaweza).
Basi nikampa namba akairudisha akasema dogo usiogope we njoo nayo kesho usisahau jembe. Nikasema sawa usijari imeisha hiyo '' in Kidagaa voice "
Kesho asubuhi saa kumi na mbili nikaamka nakuta mama kajihimu kanipikia bonge la ubwabwa . Nikawahi mno kazini aka shambani niliwahi kuliko inavyotakiwa. Nikapeleka namba pale wakanisajili. Tukapangiwa ukubwa kila mtu mahali pa kupiga hallow.
Kwenye hilo shamba jipya ni kuwa makatapila na magrader yalikuwa yamefumua na kulima so sisi kazi yetu na majembe ilikuwa ni kupigasha na kusawazisha na kutoa mizizi na vijigogo. Ilikuwa kazi easy sana na mwisho ni saa tano au sita.
Siku ya kwanza nilitoka jasho balaa ila wana wakanisaidia. Uzuri asilimia kubwa ya jamaa zangu wa pale kijijini nao walikuwa wanafanya kazi pia.
Nilipangiwa pagumu wakanisave. Tumbo lilifanya kazi iwe ngumu basi nikajikuta napata tabu. Kumbe nikajua haitakiwi me niwe nakula asbh.
Maisha ya kule shambani yalikuwa vizuri sana tena sana nayamisi kwa kweli. Sikuwa muongeaji sana na kama kawaida yangu. Mama aliniambia huko kazini kuna mengi ukiwa muongeaji manyapara hawapendi kabisa.
Na kampuni inaendeshwa kikoloni kwa sababu ipo hata kabla ya uhuru so kuna kuendeshana fulani hivi.
Kipindi hiko nilikuwa katika mahusiano na mwanamke wangu wa toka shule. Tulikutana shuleni yeye akiwa mgeni pale. Alihamia tukiwa form two nikawa nae kuanzia form three so kwao ilikuwa Dar afu me mkoani. Hata baada ya kumaliza shule tulikuwa tunawasiliana vyema kabisa. She loved me for real aisee. Kinokia changu kilikuwa kinatuunganisha.
Mshahara tulikuwa tunapokea tarehe 7 au week ya mwanzo wa mwezi. Tena dirishani ofisini ila ulinzi unakuwepo mkubwa tu.
Mwezi wa pili tarehe 7 nikapokea dirishani pesa yangu kubwa. Toka nikue ndio pesa ndefu niiyopokea. Ilikuwa shilingi 79,860/=. Ndio shilingi sabini na tisa mia nane na sitini!!!
What a smile. What the first pay. Nakiri ilikuwa ni pesa nyingi kwangu kwani licha ya kupiga vijikazi mjini sikuwahi kumake zaidi ya elfu tano kwa mara moja. So i was so damn happy.
Siku za mishahara basi huwa kuna kuwa na minada. Wanauza kila kitu.
Nami nikaenda mnadani. Nikanunua nyanya lita moja za buku nikasepa home bila kutazama Nyuma. Njiani nikapata lift. I was so happy Jamani. Nikafika home nikampa mama nyanya zake na pesa zote. Nikasema anipe tu elfu tano tu kwa mwezi inanitosha sana. Matumizi ni sadaka na vocha tu. Miaka kadhaa hapo mabundle yalikuwa rahisi tu.
Kazini kulikuwa njema. Headman alinipenda ila alikuwa anani treat kama msomi sijui kutokana na family status.
Yeah, sijisifu ika family yetu pale kijiji ilikuwa ya kipekee sana. Marehemu baba alikuwa strict sana. Na mama ndio kabisa.
***********