Njombe: Mvua iliyoambatana na upepo mkali yaezua ofisi za walimu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Mvua iliyoambatana na upepo mkali iliyoanza kunyesha majira ya saa tisa alasiri usiku wa kuamkia leo imeezua paa la jengo la utawala la ofisi za walimu na baadhi ya vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Ikonda iliyopo wilaya ya Makete mkoani Njombe

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Enelika Kayombo amesema pamoja na uharibifu uliojitokeza lakini anashukuru Mungu wanafunzi hawakuwepo shuleni hapo huku akibainisha kuwa msaada mkubwa unaohitajika ili wanafunzi waendelee na masomo ni bati ili kuezeka majengo na vitabu kwa kuwa vimenyeshewa na mvua.


Mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi Ikonda Calisto Sanga na Jackson Mbilinyi ambaye ni mjumbe wa kamati ya shule wameiomba serikali na wadau kusaidia wanavyoweza ili miundombinu ya shule iweze kufanyiwa maboresho na wanafunzi waweze kuendelea na masomo vizuri.
IMG-20231022-WA0005.jpg
IMG-20231022-WA0006.jpg
IMG-20231022-WA0007.jpg
IMG-20231022-WA0009.jpg
 
Back
Top Bottom