Njombe ilinyofolewa kutoka Iringa leo ina watu wachache kuliko mikoa yote Tanzania Bara

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
670
Naendelea kuchunguza hizi takwimu za sensa za mwaka 2022 na kuendelea kujiuliza sababu ya kugawanya mikoa na wilaya. Kwa watoto lazima mjua baadhi ya mikoa ilikuwa wilaya tu awali, mikoa hiyo ni pamoja na Songwe, Katavi, Geita na Njombe.

Leo nimeangalia mkoa wenye watu wachache nchini Tanzania, mikoa ya Zanzibar ina watu wachache. Lakini kwa kufananisha mikoa ya bara pekee, mkoa wa Njombe ni mkoa wenye watu wachache zaidi nchini.
1700208873775.png

Je, ni kweli tunaanzisha wilaya na mikoa kwa ajili ya kupeana zawadi kwa nafasi za teuzi. Je ugawaji wa mikoa na wilaya unaongeza tija kwa maendelea ya sehemu husika?

Kwa kuzingatia gharama za uendeshaji mkoa, Je ni kweli tunazingatia kuona umuhimu wa kuwa na mikoa mingi. Kama tutahofu kuhusu ukubwa wa eneo kijiografia, hatuoni kuwa tunatoa umuhimu kwa nchi kugawwa ili kuwa na marais wawili kuunguza mzigo.

So manya questions.
 
Naendelea kuchunguza hizi takwimu za sensa za mwaka 2022 na kuendelea kujiuliza sababu ya kugawanya mikoa na wilaya. Kwa watoto lazima mjua baadhi ya mikoa ilikuwa wilaya tu awali, mikoa hiyo ni pamoja na Songwe, Katavi, Geita na Njombe.

Leo nimeangalia mkoa wenye watu wachache nchini Tanzania, mikoa ya Zanzibar ina watu wachache. Lakini kwa kufananisha mikoa ya bara pekee, mkoa wa Njombe ni mkoa wenye watu wachache zaidi nchini.
View attachment 2816382

Je ni kweli tunaanzisha wilaya na mikoa kwa ajili ya kueana zawadi kwa nafasi za teuzi. Je ugawaji wa mikoa na wilaya unaongeza tija kwa maendelea ya sehemu husika?

Kuna vitu kama:
1. Jiografia
2. Shughuli za kiuchumi
3. Shughuli za kiutawala.
RAS yupo Iringa, watumishi na wananchi wapo Ludewa au Ikonda Makete. Why?
 
Geographical + Economical ndio iliamua hio, mtu utoke Manda uende Iringa jua unafika saa 4 usiku Iringa au uamue kulala Njombe kwanza, utumie siku 2, then na wakat wa kurudi hivo hivo, utakuta mtu akitaka kwenda mkoani inabidi atumie week nzima,
Wakat ingekuwa Njombe angetumia siku 2 au tatu max,

Kingine Njombe ni mkoa wenye pesa
 
Naendelea kuchunguza hizi takwimu za sensa za mwaka 2022 na kuendelea kujiuliza sababu ya kugawanya mikoa na wilaya. Kwa watoto lazima mjua baadhi ya mikoa ilikuwa wilaya tu awali, mikoa hiyo ni pamoja na Songwe, Katavi, Geita na Njombe.

Leo nimeangalia mkoa wenye watu wachache nchini Tanzania, mikoa ya Zanzibar ina watu wachache. Lakini kwa kufananisha mikoa ya bara pekee, mkoa wa Njombe ni mkoa wenye watu wachache zaidi nchini.
View attachment 2816382

Je ni kweli tunaanzisha wilaya na mikoa kwa ajili ya kueana zawadi kwa nafasi za teuzi. Je ugawaji wa mikoa na wilaya unaongeza tija kwa maendelea ya sehemu husika?

Kwa kuzingatia gharama za uendeshaji mkoa, Je ni kweli tunazingatia kuona umuhimu wa kuwa na mikoa mingi. Kama tutahofu kuhusu ukubwa wa eneo kijiografia, hatuoni kuwa tunatoa umuhimu kwa nchi kugawwa ili kuwa na marais wawili kuunguza mzigo.

So manya questions.
Ila Sasa inazidi Mikoa yenye watu wengi Kwa Uchumi.

Kigezo Cha Kugawa maeneo sio idadi ya watu pekee.Inbekuwa hivyo Kila Wilaya ya Dar ingekuwa Mkoa.

Live long Njombe
 
Naendelea kuchunguza hizi takwimu za sensa za mwaka 2022 na kuendelea kujiuliza sababu ya kugawanya mikoa na wilaya. Kwa watoto lazima mjua baadhi ya mikoa ilikuwa wilaya tu awali, mikoa hiyo ni pamoja na Songwe, Katavi, Geita na Njombe.

Leo nimeangalia mkoa wenye watu wachache nchini Tanzania, mikoa ya Zanzibar ina watu wachache. Lakini kwa kufananisha mikoa ya bara pekee, mkoa wa Njombe ni mkoa wenye watu wachache zaidi nchini.
View attachment 2816382

Je ni kweli tunaanzisha wilaya na mikoa kwa ajili ya kueana zawadi kwa nafasi za teuzi. Je ugawaji wa mikoa na wilaya unaongeza tija kwa maendelea ya sehemu husika?

Kwa kuzingatia gharama za uendeshaji mkoa, Je ni kweli tunazingatia kuona umuhimu wa kuwa na mikoa mingi. Kama tutahofu kuhusu ukubwa wa eneo kijiografia, hatuoni kuwa tunatoa umuhimu kwa nchi kugawwa ili kuwa na marais wawili kuunguza mzigo.

So manya questions.
Hata Songwe iliondolewa Mbeya na watu wajinga wasiojua Geography akina Phillip Mulugo. Kumbe alitaka kulinda nafasi yake tu ya ubunge. Hakuna mkoa wenye geography ngumu kama Songwe. Wilaya zake nyingi ziko karibu na Mbeya kuliko wilaya ya Chunya iliyo ndani ya Mbeya.
 
TUNDU LISSU - UGAWAJI MAJIMBO BUNGE, SENSA NA UKUBWA WA ENEO

Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Tundu Antipas Lissu akiangalia mgawanyo wa majimbo yenye watu wengi zaidi anagundua kuwa haiwakilishi na idadi inayostahili ya wabunge. Wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es Salaam Mwanzo

Mfano mkoa wa Dar es Salaam ulitakiwa kuwa na wabunge wasiopungua 25. Lakini una wabunge wachache sana wakati ina idadi kubwa ya wapiga kura .

Mkoa wa Lindi yenye wabunge 9 huku idadi ya wapiga kura ni ndogo sana. Mkoa wa Tabora ina idadi ndogo ya wapiga kura lakini ina wabunge wa kuchaguliwa 12 huku mkoa wa Tanga wenye idadi ndogo pia ya watu ina wabunge 12. Mikoa hii iliyotajwa kama mfano wa uwiano usiolingana baina ya idadi ya wapiga kura na wingi wa wabunge pia ni maeneo yaliyo ngome ya CCM.

Na kwa hiyo mgawanyo wa majimbo umeiba uchaguzi kwa kutumia mifumo ya kikatiba na kitaasisi kwa maana Tume ya Uchaguzi ni ya rais na mwenye mamlaka ya kutengeneza mikoa ni rais na mteuzi wa viongozi wa Tume ya Uchaguzi ni rais pia. Orodha ya Jumla ya majimbo ya uchaguzi kwa kufuata na tovuti ya bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni majimbo 273 : source : Parliament of Tanzania

Huko nchini Kenya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Majimbo ya Uchaguzi yaani IEBC ndiyo yenye mamlaka ya kutengeneza mipaka ya majimbo ktk Kenya yote inayotumia formula ya idadi ya watu ktk sehemu ndiyo itatoa mwangaza kutakuwepo wabunge wangapi. Sababu ni kuwa nchini Kenya demokrasia inaangazia kuwa wabunge wanawakilisha watu kwa kura na siyo eneo.

Tofauti na Tanzania ambapo ambapo Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC haina nguvu kikatiba kutengeneza majimbo kwa kufuatana na idadi ya wapiga kura.

Mfumo huo wa kuangalia eneo hata kama lina wapiga kura wachache na kuwapatia idadi kubwa ya wabunge huku mikoa kama Dar es Salaam, Mwanza yenye idadi kubwa ya wapiga kura inapewa wabunge wachache sana.

Sababu ni kuwa imeonekana maeneo yenye watu wengi ambao ni wapiga kura huwa wana tabia au mazoea ya kuchagua wapinzani hivyo kwa Tanzania wengi hao wanapewa wabunge wachache ili kudhibiti idadi ya wabunge wa upinzani wanaoweza kuchaguliwa . Parliament of Tanzania

Wawakilishi wa waangalizi wa chaguzi toka ndani na nje wameona mapungufu haya ya kuwa kuna maeneo yana wapiga kura wachache sana lakini ina wabunge wengi, huku kuna maeneo yenye wapiga kura wengi inawakilishwa na wabunge wachache sana na hii Indonesia kukosekana uwiano kati ya idadi ya wabunge na wapiga kura wao.

Source : Forbs Media
Tume ya Uhusiano na Uratibu Rasimu ya Warioba ililenga kuhakikisha ... Warioba alisema idadi ya wabunge isizidi 75, Bunge Maalum likasema..... soma zaidi : source : Hotuba ya Jaji Josefu Warioba kuhusu Rasimu ya Katiba ya Tanzania

N.B
Idadi ya majimbo bunge upande wa Bara ulingane na idadi ya watu kwa kuwa ukubwa wa eneo siyo kigezo msingi
 
Hata Songwe iliondolewa Mbeya na watu wajinga wasiojua Geography akina Phillip Mulugo. Kumbe alitaka kulinda nafasi yake tu ya ubunge. Hakuna mkoa wenye geography ngumu kama Songwe. Wilaya zake nyingi ziko karibu na Mbeya kuliko wilaya ya Chunya iliyo ndani ya Mbeya.
Toa upunguani wako hapa.Ugawaji huu wa maeneo umesogeza Huduma zaidi Kwa Umma kuliko hapo awali ambapo Kila kitu kiliishia Mjini na Kwa wanyakyusa huko.

Naunga mkono zoezi la kuanzisha Mikoa mipya maana ni sawa na kufanya ugatuaji wa Madaraka.
 
Pia Tundu Lissu anauliza wakuu wa wilaya 273 wanaolipwa mishahara na nyuma yao utitiri wa wafanyakazi katika 'boma' yaani ofisi ya mkuu wa wilaya.

Wakati kuna wenyeviti wa Halmashauri na madiwani wanaochaguliwa na wananchi kufanya kazi katika maeneo bila kusahau mbunge anayekwenda katika bunge la serikali kuu Dodoma kuangalia bajeti ya serikali kuu ya Muungano jinsi inavyogawa na kukusanya kodi kwa matumizi ya ulinzi, usalama, miradi mikubwa n.k

1700215015922.png
 
View attachment 2816409
Tundu Lisu ndio nani kwenye Nchi hii?
 
Toa upunguani wako hapa.Ugawaji huu wa maeneo umesogeza Huduma zaidi Kwa Umma kuliko hapo awali ambapo Kila kitu kiliishia Mjini na Kwa wanyakyusa huko.

Naunga mkono zoezi la kuanzisha Mikoa mipya maana ni sawa na kufanya ugatuaji wa Madaraka.
Wewe ndiye mpumbavu ila hujijui tu
 
Nchii hii mgawanyo wa mikoa unatokana ua ushawishi wa wanasiasa. Njombe mshawishi alikuwa Makinda, Simiyu Chenge, Manyara Sumaye, Katavi Pinda. Geita Magufuri (wakati akiwa waziri akataka kufanya makao makuu ya we chato, alipokuwa rais akataka chato uwe mkoa). Nashangaa kwa Majaliwa hakujawa mkoa.
 
1. Mkoa wa Njombe una watu wachache kuliko mikoa yote ya bara kwa mujibu wa sensa.

2. Mkoa wa Njombe ni wa pili baada ya Dar kwa utajiri kwa kigezo cha per capita income.

3. Mkoa wa Njombe unaongoza kwa idafi ya mabilionea nchini.

4. Mkoa wa Njombe, una eneo kubwa la kiutawala kuizidi mikoa mingi ya bara.

Je, kigezo cha kuwa mkoa, una uhakika ni idadi ya watu pekee yake?

Lakini ufahamu pia, sensa ni kwaajili ya kutoa picha tu ya jumla, lakini siyo halisia. Watu wengi siku ya sensa hawakuhesabiwa maeneo yao.

Tukitaka kupata idadi halisi ya watu toka eneo la kila mahali, labda tufanye sensa kama ilivyokuwa inafanyika enzi za Yosefu na Maria. Wao walisafiri mpaka eneo walikozaliwa, Betlehemu ili kwenda kuhesabiwa.

Idadi hiyo kubwa kabisa ya Dar, wala siyo wakazi wa Dar, bali wapo kwa shughuli za muda mfupi, wa kati au mrefu. Ni wachache ambao ni wakazi wa kudumu. Hata Mwalimu Nyerere aliishi Dar wajati wote akiwa Rais, lakini alipostaafu alirudi kwao, Butiama- Musoma.

NB: Mara nyingi wenye uchiumi mzuri husafiri na kutawanyika sana.
 
Back
Top Bottom