backtobasics
Member
- Apr 24, 2024
- 26
- 40
Wana JF,
Ni njia gani isiyo na madhara ya kumfanya mtoto aache kunyonya vidole, ana miezi 7 sasa ila naona kwa kasi anayoenda nayo yaani hadi usingizini yeye yuko navyo tu...
Sitamani afike umri mpaka anaanza shule awe ananyonya na pia nasikia vinaharibu dental formula hivyo nawezaje kumsaidia?
===
Ufuatiliaji wa JamiiCheck
Ni njia gani isiyo na madhara ya kumfanya mtoto aache kunyonya vidole, ana miezi 7 sasa ila naona kwa kasi anayoenda nayo yaani hadi usingizini yeye yuko navyo tu...
Sitamani afike umri mpaka anaanza shule awe ananyonya na pia nasikia vinaharibu dental formula hivyo nawezaje kumsaidia?
===
Ufuatiliaji wa JamiiCheck
Je, kunyonya vidole kwa mtoto ni hali ya kawaida?
Tovuti ya Hopekins medicine kupitia makala yake yenye kichwa “Finger sucking in children” wanabainisha kuwa watoto huzaliwa na uwezo wa wachanga huzaliwa na uwezo wa asili wa kutafuta na kunyonya, wakati mwingine hata kabla ya kuzaliwa.
Watoto hunyonya vidole kwa sababu kufanya hivyo huwafariji basi wanaweza kujenga tabia ambayo inaweza kuwa ngumu kuja kuiacha. American Dental Association na American Academy of Pediatric Dentistry wanashauri kuwa watoto wanapaswa kuacha kunyonya vidole kati ya umri wa miaka 2 hadi 4.
Tovuti ya colgate inaeleza kuwa hali hii humpa mtoto faraja, na anapokua inaweza kumsaidia kujihisi salama na mwenye furaha. Pia watoto wengi wachanga na wadogo hutumia kama njia ya kujikimu wanapokuwa na wasiwasi au wametengana na wazazi wao. Tabia hii pia husaidia kupata usingizi, ndiyo maana baadhi ya watoto hunyonya vidole vyao jioni kabla ya kulala.
Mtoto akiendelea kunyonya vidole baada ya kufikisha miaka 4 nini hutokea?
Kama ilivyoelezwa hapo awali angalu kwa kawaida inategemea mtoto aache kunyonya vidole kati ya akiwa na miaka miwili (2) hadi minne (4). Iwapo mtoto ataendelea kunyonya vidole zaidi ya hapo anaweza kukutwa na baadhi ya changamoto.
Iwapo mtoto ataendelea kunyonya vidole zaidi ya hapo inaweza kupelekea kuathiri mpangilio wake wa meno, Pia kunaweza kuathiri sehemu ya juu ya ndani ya mdomo inayojulikana kama kaakaa la juu (palate). Hatari ya matatizo ya meno huwa kubwa zaidi ikiwa watoto hunyonya vidole kwa muda mrefu na mara kwa mara.
Hopkins Medicine wanabainisha pia kuwa Kunyonya vidole mara nyingi si tatizo hadi meno ya kudumu ya mtoto yanapoanza kuota. Hata hivyo, tabia ya kunyonya vidole kwa muda mrefu inaweza kusababisha:
Nini cha kufanya ili mtoto aache tabia ya kunyonya vidole
- Mfumo usio wa kawaida wa kumeza au kuzungumza kwa kusukuma ulimi mbele, ikiwemo lafudhi ya kutamka vibaya baadhi ya herufi.
- Ulimi kukaa katika nafasi isiyo ya kawaida ukiwa umetulia.
- Kupungua kwa nguvu ya ulimi.
- Kupungua kwa uwezo wa ulimi kusogea vizuri (kama kuinuliwa au kusogezwa upande kwa upande), jambo linaloweza kuathiri matamshi na ulaji.
- Meno ya mbele kubaki wazi (open bite), hali inayoweza kuathiri kung’ata, kutafuna na kuzungumza.
Tabia hii mara nyingi hukoma yenyewe bila kuwa na tatizo kubwa au juhudi maalum. Mara nyingi, njia bora ni kuipuuza tu. Watoto huja kugundua wenyewe kupitia mazingira ya kijamii na ushawishi wa wenzao kwamba tabia hiyo haikubaliki tena. Hata hivyo, ikiwa itaendelea baada ya umri wa kwenda shule ya awali, basi unaweza kufanya yafuatayo;
Mayo Clinic wanaeleza kuwa mara chache wataalamu wa afya hushauri kutumia ,pamoja na kupaka kitu chenye ladha chungu kwenye kucha ya kidole, kufunga bandeji kwenye kidole, kutumia kifaa maalum cha mdomoni au kufunika mkono kwa soksi wakati wa usiku.
- Tengeneza ratiba au mfumo wa zawadi kufuatilia maendeleo ya mtoto katika kuacha tabia hiyo.
- Mhimize na umsifie mtoto anapojaribu kuacha.
- Mpeleke mtoto kwa daktari wa meno ili kujifunza faida za kuacha tabia hiyo.
- Tambua visababishi. Ikiwa mtoto wako hanuniwi lakini bado ananyonya kidole, jaribu kugundua kinachomfanya ajisikie hivyo. Unaweza kumpa faraja kwa kumbatio au maneno ya kumtuliza. Pia unaweza kumpa mto au mdoli wa kukumbatia ili ashike na kujituliza.
- Endelea kumkubusha kwa upole. Ikiwa mtoto wako ananyonya kidole bila kujitambua, mkumbushe kwa upole aache. Epuka kumkemea au kumkosoa mtoto wako.
Nini cha kufanya iwapo njia zote hazitozaa matunda?
Kwa baadhi ya watoto, kunyonya kidole ni tabia ngumu sana kuacha. Jaribu kutokuwa na wasiwasi sana. Usiweke shinikizo kubwa kwa mtoto kuacha kunyonya kidole kwani kunaweza kuchelewesha zaidi mchakato huo. Zungumza na daktari wa meno wa meno ikiwa unahitaji msaada zaidi.