Njia ya kumuachisha mtoto kunyonya kidole

Njia ya kumuachisha mtoto kunyonya kidole

Jamani hiyo ni stage katika ukuaji mtoto wa miezi Saba ni mdogo Sana inaweza kua anaota meno nakushauri usome mtandaoni kitu gani cha kutegemea kwenye kila mwezi kuanzia anavyozaliwa jua kila mwezi utegemee kitu gani mfano kule tick-tock kuna madaktari wengi wanaelezea hii stage ya kunyonya kidole na jinsi ya kumuchisha mtoto kama akipitiliza mana wengi wanaacha wenyewe wangu ameacha mwenyewe akiwa na miezi 8 au 9 sikumbuki vzuri
 
Kwani hakashibi? Hutujui huyo tubinadamu kanashiba vizuri na bado kanataka kulambalamba vitušŸ™ŒšŸ¾
Tabia ya kunyonya kidole watoto huanza akiwa anacheleweshwa kunyonya anapopata njaa kwahiyo anajifariji kwa kidole, wengine ni wale unakuta mama yake alimrambisha sukari au asali kwenye kidole kwa lengo la kumfanya awe anatulia peke yake akinyonya kidole au unakuta ameona mtoto mwenzie akifanya hivyo.
sababu za juu hapo huwa ni ngumu kuacha akianza ndiyo unatumia mbinu kufanya aache
 
Tabia ya kunyonya kidole watoto huanza akiwa anacheleweshwa kunyonya anapopata njaa kwahiyo anajifariji kwa kidole, wengine ni wale unakuta mama yake alimrambisha sukari au asali kwenye kidole kwa lengo la kumfanya awe anatulia peke yake akinyonya kidole au unakuta ameona mtoto mwenzie akifanya hivyo.
sababu za juu hapo huwa ni ngumu kuacha akianza ndiyo unatumia mbinu kufanya aache
Duhh!šŸ¤”
 
Duhh!šŸ¤”
Ni jambo la kawaida watoto kunyonya vidole kwenye hatua zao za ukuaji wengine wanasahau mapema na wengine wanaokuwa peke yao hukaa na hiyo tabia muda mrefu
 
Mtoto mchanga wa miezi 7 anakuumiza kichwa jamani!! hakikisha anashiba vizuri, mpe michezo ya kumfanya awe busy, google toys za watoto wa umri huo ukanunue, muwekee 'Pacifer' pia huenda magego yanamuwasha, tofauti na hapo kua na amani hua wanaacha wenyewe
 
Funga bandage kidole anachonya wengine pia hutoboa kidogo kidole na sindano akinyonya anaumia anaacha.
Kuna dogo licha ya kumsema yeye amenyonya kidole hadiu anamaliza chuo na sahivi akiwa katika kazi zake anajisahau unakuta kidole mdomoni
Watu mna ukatiliii! Mtoto wako uliyemzaa unawezaje kumtoboa na sindano kwa makusudi
 
Hili siyo tatizo. Ataacha mwenyewe hasa akianza shule. Usihangaike. Kna watu tuna watoto walinyonya vidole .... yaani kila mtoto wangu alinyonyalakini waliaacha wenyewe.
so waliacha wakiwa umri gani?meno yao vipi?ni kweli yaliathirika?
 
Mr Backtobasics, msikilize kwa makini na hiki nachokwambia ukitekeleze,

Kesho apeleke Mwanao hospitali ambayo anaweza kupima kipimo cha Damu kiitwacho FBP.

Kwa kuwa hii ni dalili ya upungufu wa Damu au upungufu wa madini ya chuma mwilini.

Kwa kuwa wewe sio Dokta basi jieleze kwa Daktari kuwa nimeshauriwa na marafiki wa JF.

Ktk kipimo hicho hata Wewe unaweza kutazama mambo yafuatayo

Wingi wa Damu Hb
Ukubwa wa seli hai nyekundu za Damu yaani MCV na wingi wa madini ya chuma ndani ya seli hai nyekundu yaani MCHC

Kifupi tazama

HB
MCV
MCHC

Mtoto wa mwenzio muone kama Mtoto wako
hii mpya!!!anyways alipimwaga damu yuko ok, hiyo HB
 
so waliacha wakiwa umri gani?meno yao vipi?ni kweli yaliathirika?
Mtoto mchanga wa miezi 7 anakuumiza kichwa jamani!! hakikisha anashiba vizuri, mpe michezo ya kumfanya awe busy, google toys za watoto wa umri huo ukanunue, muwekee 'Pacifer' pia huenda magego yanamuwasha, tofauti na hapo kua na amani hua wanaacha wenyewe
sio mtoto wangu wa kwanza so this is my first experience, hayo yote yanafanyika au unataka hadi usingizini awe na toy!!?pacifier tushachelewa naona haitaki...
 
Wana JF,

Ni njia gani isiyo na madhara ya kumfanya mtoto aache kunyonya vidole, ana miezi 7 sasa ila naona kwa kasi anayoenda nayo yaani hadi usingizini yeye yuko navyo tu...

Sitamani afike umri mpaka anaanza shule awe ananyonya na pia nasikia vinaharibu dental formula hivyo nawezaje kumsaidia?
Je, kunyonya vidole kwa mtoto ni hali ya kawaida?

Tovuti ya Hopekins medicine kupitia makala yake yenye kichwa ā€œFinger sucking in childrenā€ wanabainisha kuwa watoto huzaliwa na uwezo wa wachanga huzaliwa na uwezo wa asili wa kutafuta na kunyonya, wakati mwingine hata kabla ya kuzaliwa.

Watoto hunyonya vidole kwa sababu kufanya hivyo huwafariji basi wanaweza kujenga tabia ambayo inaweza kuwa ngumu kuja kuiacha. American Dental Association na American Academy of Pediatric Dentistry wanashauri kuwa watoto wanapaswa kuacha kunyonya vidole kati ya umri wa miaka 2 hadi 4.

Tovuti ya colgate inaeleza kuwa hali hii humpa mtoto faraja, na anapokua inaweza kumsaidia kujihisi salama na mwenye furaha. Pia watoto wengi wachanga na wadogo hutumia kama njia ya kujikimu wanapokuwa na wasiwasi au wametengana na wazazi wao. Tabia hii pia husaidia kupata usingizi, ndiyo maana baadhi ya watoto hunyonya vidole vyao jioni kabla ya kulala.

Mtoto akiendelea kunyonya vidole baada ya kufikisha miaka 4 nini hutokea?

Kama ilivyoelezwa hapo awali angalu kwa kawaida inategemea mtoto aache kunyonya vidole kati ya akiwa na miaka miwili (2) hadi minne (4). Iwapo mtoto ataendelea kunyonya vidole zaidi ya hapo anaweza kukutwa na baadhi ya changamoto.

Iwapo mtoto ataendelea kunyonya vidole zaidi ya hapo inaweza kupelekea kuathiri mpangilio wake wa meno, Pia kunaweza kuathiri sehemu ya juu ya ndani ya mdomo inayojulikana kama kaakaa la juu (palate). Hatari ya matatizo ya meno huwa kubwa zaidi ikiwa watoto hunyonya vidole kwa muda mrefu na mara kwa mara.

Hopkins Medicine wanabainisha pia kuwa Kunyonya vidole mara nyingi si tatizo hadi meno ya kudumu ya mtoto yanapoanza kuota. Hata hivyo, tabia ya kunyonya vidole kwa muda mrefu inaweza kusababisha:

  • Mfumo usio wa kawaida wa kumeza au kuzungumza kwa kusukuma ulimi mbele, ikiwemo lafudhi ya kutamka vibaya baadhi ya herufi.
  • Ulimi kukaa katika nafasi isiyo ya kawaida ukiwa umetulia.
  • Kupungua kwa nguvu ya ulimi.
  • Kupungua kwa uwezo wa ulimi kusogea vizuri (kama kuinuliwa au kusogezwa upande kwa upande), jambo linaloweza kuathiri matamshi na ulaji.
  • Meno ya mbele kubaki wazi (open bite), hali inayoweza kuathiri kung’ata, kutafuna na kuzungumza.
Nini cha kufanya ili mtoto aache tabia ya kunyonya vidole

Tabia hii mara nyingi hukoma yenyewe bila kuwa na tatizo kubwa au juhudi maalum. Mara nyingi, njia bora ni kuipuuza tu. Watoto huja kugundua wenyewe kupitia mazingira ya kijamii na ushawishi wa wenzao kwamba tabia hiyo haikubaliki tena. Hata hivyo, ikiwa itaendelea baada ya umri wa kwenda shule ya awali, basi unaweza kufanya yafuatayo;

  • Tengeneza ratiba au mfumo wa zawadi kufuatilia maendeleo ya mtoto katika kuacha tabia hiyo.
  • Mhimize na umsifie mtoto anapojaribu kuacha.
  • Mpeleke mtoto kwa daktari wa meno ili kujifunza faida za kuacha tabia hiyo.
  • Tambua visababishi. Ikiwa mtoto wako hanuniwi lakini bado ananyonya kidole, jaribu kugundua kinachomfanya ajisikie hivyo. Unaweza kumpa faraja kwa kumbatio au maneno ya kumtuliza. Pia unaweza kumpa mto au mdoli wa kukumbatia ili ashike na kujituliza.
  • Endelea kumkubusha kwa upole. Ikiwa mtoto wako ananyonya kidole bila kujitambua, mkumbushe kwa upole aache. Epuka kumkemea au kumkosoa mtoto wako.
Mayo Clinic wanaeleza kuwa mara chache wataalamu wa afya hushauri kutumia ,pamoja na kupaka kitu chenye ladha chungu kwenye kucha ya kidole, kufunga bandeji kwenye kidole, kutumia kifaa maalum cha mdomoni au kufunika mkono kwa soksi wakati wa usiku.

Nini cha kufanya iwapo njia zote hazitozaa matunda?

Kwa baadhi ya watoto, kunyonya kidole ni tabia ngumu sana kuacha. Jaribu kutokuwa na wasiwasi sana. Usiweke shinikizo kubwa kwa mtoto kuacha kunyonya kidole kwani kunaweza kuchelewesha zaidi mchakato huo. Zungumza na daktari wa meno wa meno ikiwa unahitaji msaada zaidi.
 
Back
Top Bottom