Njia rahisi ya Serikali kutoa elimu ya katiba ni kufanya katiba kuwa "COMPULSORY STUDY/BOOK" level zote za elimu kuanzia primary to University

Mto Songwe

JF-Expert Member
Jul 17, 2023
6,028
12,351
Kwa kuzingatia kichwa cha uzi.

- Kama kweli serikali ya Tanzania ina nia ya kutoa elimu ya katiba na kufanya Watanzania karibia wote wa nchi hii kuijua katiba yao vizuri.

Serikali haina budi kuchukua uamuzi mara moja wa kutoa elimu ya katiba kuanzia ngazi mbalimbali za elimu yetu kwa kuanza na primary education mpaka level ya University.

Serikali ichukue uamuzi wa kuchapisha nakala nyingi za katiba ya Tanzania na kuzisambaza mashuleni kote na vyuoni kote na kufanya "mafunzo/elimu/katiba yenyewe" kuwa ni takwa la lazima wanafunzi wote wafundishwe na wafahamu kwa kina.

Kuwa elimisha wanafunzi kwanza ni kuielimisha jamii kwa asilimia kubwa.

Hii ni njia bora ikitumika kama serikali ipo serious kuhusu suala la katiba ya nchi.
 
Wazanzibar walitengeneza katiba yao pasipo hata kupewa elimu ya miaka 3 hiyo,kwa kuwa katiba inayotakiwa inawahusu na watanganyika wanataka itolewe elimu ya miaka3 ili waendelee kudumu madarakani.
 
Wazanzibar walitengeneza katiba yao pasipo hata kupewa elimu ya miaka 3 hiyo,kwa kuwa katiba inayotakiwa inawahusu na watanganyika wanataka itolewe elimu ya miaka3 ili waendelee kudumu madarakani.
Kama serikali inasema watu wake hawana wanachojua kuhusu katiba basi ni vyema wachukue huo ushauri wangu kwanza ndio mengine yafuate
 
Kama serikali inasema watu wake hawana wanachojua kuhusu katiba basi ni vyema wachukue huo ushauri wangu kwanza ndio mengine yafuate
Hata ushauri namna gani hawatakuelewa kwa kuwa wao wanachoangalia ni katiba inayowapa feva ya kuendelea kuwepo madarakani.

Hii ya kutoa elimu ya miaka 3 ni janjajanja ya mama tu, kwa kuwa anajuwa kuwa katiba iliopo inambeba mpaka kipindi chake chote hiki,ukiongeza na miaka 3 ya kutoa elimu,tayari atakuwa ametinga awamu ya pili,elimu mpaka ije ikamilike kutolewa tayari atakuwa ameshaondoka madarakani na atakayemrithi jibu lake litakuwa ni kama la Magufuli kuwa Mimi sikuwaahidi katiba mpya.
 
Back
Top Bottom