Njia rahisi ya kuleta 'sense' kwa Wamalawi: Tanzania itangaze kuanza utafiti wa mafuta Ziwa Nyasa!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,478
39,996
Kama Tanzania inaamini nusu ya Ziwa Nyasa ni mali yake kwanini wanasubiri kuwabembeleza Wamalawi kuhusu suala la kusitisha utafiti wa mafuta ili kupisha majadiliano? HIvi tumekuwa wasahaulifu hivi kiasi kwamba hatujui suala hili nusura litulete katika vita na Kamuzu Banda?

Tanzania inaamini mpaka wake na Malawi umepita kwenye Ziwa Nyasa. Sasa kama hii ni imani ya Kikwete na Membe na serikali yetu kwa ujumla kwanini wanataka kupoteza muda wa kuwashawishi Wamalawi? Jambo rahisi ni Serikali kuanza utafiti wa mafuta na gesi kwenye "upande wetu" na kutoa kibali kwa makampuni ya kimataifa kufanya hivyo. Wamalawi watafanya nini?

Unless tuna jeshi lisiloweza kulinda mipaka yetu! Kama Wamalawi wameweza kuingia "nusu yetu" ni nini kinatuzuia kuwazuia? Si Idi Amin naye alisema sehemu ya ardhi yetu ni yake akateua hadi Mkuu wa Wilaya?

Lakini nani anafikiri kuna kiongozi anayeweza kusimama vikali hivi? Watu wameng'ang'ania ati JWTZ lilinde mitambo ya umeme ya Tanesco! na mipaka analinda nani?
 
mkuu tatizo la Tanzania ni siasa hata kwenye maswala ya utendandaji,hawa wamalawi ilikua ni kuwasogezea vifaa vya kijeshi na wanajeshi kadhaa wawe wanapiga jeramba pembezoni mwa ziwa. sidhani kama Malawi wengethubutu kukanyaga hata fukwe za Tanzania.!!
 
Matokeo ya kuwa na Raisi dhaifu.
Zingekuwa enzi za Mwl. Nyerere si Bingu wa Mutharika wala Joyce Banda ambae angethubutu kupandisha mabega kwamba ziwa nyasa lote ni sehemu ya nchi yao. Kamuzu Banda alitaka kumjaribu Mwalimu Nyerere, anafahamu alichotaka kufanyiwa na mwl.hadi akashika adabu yake.

Zingekuwa enzi za Mkapa yeye angeshusha vikosi vya jeshi mara moja ziwa nyasa na wamalawi wangetia akili.
Sasa enzi hizi za kikwete mipaka ya nchi imekosa usimamizi, haina ulinzi, wahamiaji haramu wanaingia kadri wanavyotaka, na malawi sasa wanataka kujimegea kipande cha ziwa nyasa, lakini raisi yuko kimya kama vile hilo ni jambo dogo sana kwake.
 
Tumekuwa nchi ya namna kwamba wakati watu tunapotaka kuona uthabiti na uwezo wa uongozi wetu ndio tunapokutana sononesho, ila kwenye masuala ya kijinga ndio watu mapovu yanawatoka jumlisha hujuma kali.
 
Kwa kweli huu mchezo wa Wamalawi natamani baba wa taifa angekuwepo wala wasingethubutu. natoa rai kwa Raisi wetu wa Jamhuri at least aonyeshe mfano katika hili ahakikishe harijirudii tena. Put a stop to it once for all!
 
...jamani, Wajeshi wetu waende Nyasa, na msitu wa Mabwepande nani ataulinda?!!

...zoezi la vitambulisho vya Taifa si la lazima, mipaka ya nini sasa jamani?!!
 
ujue si watanzania ni wapole sana...na sidhani tilldate kama kuna magwanda yeyote yanayoweza kupambana kijeshi zaidi ya kuota vitambi na kusumbua wapinzani wa vyama. Just imagine mipakani kulivyokuwa na uhaini wa kupitiliza....

Biashara za watu kupitia huko mipakani.
Biashara haramu kama vile sukari za magendo nk huko mipakani
Kupitishia magogo yetu na badae yanaletwa kwa njia ya baharini na kudai yanatoka South A.
Na mengineyo mengi...na wanajeshi wapo tu...nothing they do, just hujuma kulipua kambi za Gombs na kuua raia wasio na hatia.
 
Dawa ni kulinda mpaka wetu......kuhusu utafiti wa mafuta.......hali hii isitulazimishe eti na sisi tufanye kama wanvyofanya wao......tutafanya utafiti kwa wakati wetu tunaoona unafaa...hata kama ni 50 ijayo.....cha msingi ni kulinda mpaka na heshima yetu........
 
Kwa kuanzia, jeshi likafanye mazoezi ya silaha kwenye ziwa Nyasa
...your end is psychologically traumatised by this man, mmmh?!! lol
460-kim-jong_862915c.jpg
 
Nadhani watu wanazungumzia kupeleka wanajeshi kule kwa urahisi sana. Hupeleki wanajeshi kwenye mpaka wa nchi nyingine bila kuwa tayari kupigana vita. Kuna vitendo ambavyo kisheria vikifanyika vinachukuliwa kuwa ni "act of war". Tanzania haipaswi kupeleka wanajeshi wake karibu na mpaka na Malawi bila kuwa tayari kwenda vitani. Swali, Watanzania mko tayari kwa vita siyo kwenda kujionesha tu. Nani kawaambia ati mkipeleka wanajeshi basi wamalawi watanywea? Na wenyewe si wana jeshi?

Unafikiri kuwa na wingi wa jeshi na silaha ndio kushinda vita? Lakini kubwa zaidi ni kuwa viongozi wetu tayari hawana ile cloud ya kuwa viongozi wa wakati wa vita. Kama kwenye amani wametutawala hivi wakati wa vita itakuwaje? Njia pekee ya kuleta hiyo heshima ni sisi kutangaza tunaanza utafiti wetu wa mafuta kwenye nusu yetu tukiheshimu mipaka yetu na hatutagusa nusu ya Malawi. Malawi watakuwa wametupiwa mpira!

Kama wao wanaamini ziwa zima ni lao basi wao ndio wafanye hatua ya kwanza vita.... hapo ndio JWTZ linapoenda kulinda mpaka wetu!
 
Kama Tanzania inaamini nusu ya Ziwa Nyasa ni mali yake kwanini wanasubiri kuwabembeleza Wamalawi kuhusu suala la kusitisha utafiti wa mafuta ili kupisha majadiliano? HIvi tumekuwa wasahaulifu hivi kiasi kwamba hatujui suala hili nusura litulete katika vita na Kamuzu Banda?

Tanzania inaamini mpaka wake na Malawi umepita kwenye Ziwa Nyasa. Sasa kama hii ni imani ya Kikwete na Membe na serikali yetu kwa ujumla kwanini wanataka kupoteza muda wa kuwashawishi Wamalawi? Jambo rahisi ni Serikali kuanza utafiti wa mafuta na gesi kwenye "upande wetu" na kutoa kibali kwa makampuni ya kimataifa kufanya hivyo. Wamalawi watafanya nini?

Unless tuna jeshi lisiloweza kulinda mipaka yetu! Kama Wamalawi wameweza kuingia "nusu yetu" ni nini kinatuzuia kuwazuia? Si Idi Amin naye alisema sehemu ya ardhi yetu ni yake akateua hadi Mkuu wa Wilaya?

Lakini nani anafikiri kuna kiongozi anayeweza kusimama vikali hivi? Watu wameng'ang'ania ati JWTZ lilinde mitambo ya umeme ya Tanesco! na mipaka analinda nani?

Kwa viongozi wa ngazi za juu tuliokuwa nao kwa sasa usitegemee MAAMUZI MAGUMU kama kuruhusu makampuni kuanza utafiti UPANDE WA KWETU waa Ziwa Nyasa!!! Hawapendi kuitwa DHAIFU lakini masuala kama hili la MPAKA WETU NA MALAWI ndiyo yanadhihirisha UDHAIFU unaolalamikiwa
 
Nchi yetu wazenji wakitaka kujitenga utasikia fasta vikosi vya JW vimetumwa, lakini kwenye inshu muhimu ya kulinda mipaka ya nchi ni kimyaaaaaa! watakwambia wanatumia njia za kidiplomasia kutatua tatizo hilo "Yaani mtu anakuchomoka kidole cha masaburi unachekacheka tu!"
Kweli huu urafiki na waarabu umetuharibu.
 
.....
Njia pekee ya kuleta hiyo heshima ni sisi kutangaza tunaanza utafiti wetu wa mafuta kwenye nusu yetu tukiheshimu mipaka yetu na hatutagusa nusu ya Malawi. Malawi watakuwa wametupiwa mpira!

Kama wao wanaamini ziwa zima ni lao basi wao ndio wafanye hatua ya kwanza vita.... hapo ndio JWTZ linapoenda kulinda mpaka wetu!

...wewe una/uli/ume-cheza chess maishani mwako!!
 
Back
Top Bottom