Habari njema kwa nchi, gesi nyingine ya Helium yagunduliwa Bonde la Ziwa Nyasa. Tanzania kuwa muuzaji kinara Duniani

The Sunk Cost Fallacy 2

JF-Expert Member
Nov 8, 2022
7,382
8,437
Habari wadau,

Habari njema kwa Tanzania ni kwamba, imefanikiwa kugundua Gas nyingine ya Helium Kaskazini ya Bonde la Ziwa Nyasa eneo la Matema wilaya ya Kyela mkoani Mbeya.

Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na jarida la The Business Wiz likinukuu kampuni ya Helium One iliyokuwa inafanya Utafiti kwa kushirikiana na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam; zinaonyesha kwamba sampuli zimebainisha uwepo wa gas nyingi ya Helium inayoweza kuzalishwa kibiashara.

Ikumbukwe pia Kampuni ya Helium One ya Australia inamiliki vitalu vya gas ya Helium Kaskazini mwa Bonde la Ziwa Nyasa Mkoa wa Rukwa/Songwe ambapo inaendelea na mchakato wa kuanza kuzalisha kibiashara.

Taarifa rasmi za ugunduzi huu zitachapishwa mwaka ujao baada ya kukirihisha na kiwango cha deposits.

Ugunduzi huu utaifanya Tanzania kuwa mzalishaji na muuzaji kinara Duniani wa Gas ya Helium, hivyo kuingiza pato la taifa na kuimarisha mapato ya nchi.

My Take
Serikali ijipange zaidi kuehiriki kwenye sekta hii ili nchi ipate tunachostahili badala ya kushangilia halafu wanafaidi Wazungu.

========

The ASX’s newest Helium-focused entrant, Noble Helium (ASX:NHE), has confirmed early-stage evidence supporting possible commercial-scale helium deposits underground at the company’s second most developed project, the North Nyasa play.

That early-stage evidence comes in the form of a soil gas survey analysis which has turned over data showing anomalies coincident with helium gas accumulation.

In short, first-pass interpretation of the numbers shows helium concentrations at 40% above normal background levels (7.8ppm).

“This additional helium can only be explained as the result of micro-seepage from underground,” the company states.

Data is being processed at the University of Dar es Salaam; the former capital of Tanzania and home to the country’s financial district.

Crucial context: the 2022 US helium shortage

Two unplanned plant shutdowns earlier this year at a facility in the US, and another in Russia respectively, kicked off a US helium shortage that is echoing into global markets.

While helium can be synthesised, it is most often mined—and that is why a number of Australian companies are searching for the gas.

Noble is not alone on the ASX, as far as helium plays go. Grand Gulf Energy (ASX:GGE), located in Utah, are also seeking to produce helium for sale into the US markets as companies scramble to extract more of the gas from the ground.

Blue Star Helium (ASX:BNL) is also located in the US; Renergen (ASX:RLT) also searches for helium.
The helium shortage is impacting everything from weather balloons to the manufacture and operation of MRI machines, where helium is needed to keep magnets cool.

Some market research firms predict the value of the global helium market to reach US$6.6bn by 2028; a CAGR of 5% from US$4.7bn in 2021. A shortage is predicted to continue defining market dynamics.

Prospective resource inbound

While data has not been fully processed yet, once the whole kitchen sink of results are in, the company will get to work amalgamating soil gas survey results with existing 2D seismic and airborne data to begin forming a prospective resource estimate.

Noble Helium expects its maiden estimate for the North Nyasa project to be published in 2023, but, does not provide guidance on when delivery can be expected.

“The preliminary data is highly encouraging, demonstrating elevated helium concentrations and only trace CO2 and methane concentrations,” Noble chief Justyn Wood said.

Methane, for all intents and purposes, is synonymous with natural gas, meaning that there’s also strong evidence Noble hasn’t accidentally discovered the wrong kind of gas deposit.

“The North Nyasa project has a very similar setting to [our other project] North Rukwa, which as we have seen is highly prospective for helium,” Wood added.

The company’s chief also cited good working relationships with local stakeholders.

Two projects at once

Noble’s North Nyasa project sits second in the race to production behind the company’s flagship project, North Rukwa.

Worth noting is Noble highlights early-stage results at North Nyasa echo those early stage results pulled from Rukwa.

Both projects are located in Tanzania; for the uninitiated, a country in east Africa.
The North Nyasa project tenements are located near a small town called Matema on the edges of Lake Nyasa, nearby the Malawian border to the southwest.
A look at Noble Helium's six month charts. Between November 23 and 25, over 4 million shares were bought

A look at Noble Helium's six month charts. Between November 23 and 25, over 4 million shares were bought


Marketindex
 

Attachments

  • Screenshot_20221201-061925.png
    Screenshot_20221201-061925.png
    68.7 KB · Views: 12
Tutakuwa tunashangilia hivo hivo miaka yote kama ilivo Mwadui, Geita, North Mara, Mtwara, Bulyankulu, Chunya, Yaani unufaikaji wetu haupo kwa maslahi ya taifa, hata gesi ya Mtwara tulielezwa sio yetu na kwa aina ya viongozi waliopo ambao hawana uzalendo wanaojali matumbo yao ndio maana tunaibiwa rasilimali zetu mchana kweupe tunazidiwa hadi na Uganda na Botswana wanapata mgao wao wa kueleweka sisi ni mazezeta kabisa.
 
Tutakua tunashangilia hivo hivo miaka yote kama ilivo mwadui, geita, north mara, mtwara, bulyankulu, chunya, yaani unufaikaji wetu haupo kwa maslahi ya taifa, hata gesi ya mtwara tulielezwa sio yetu na kwa aina ya viongozi waliopo ambao hawana uzalendo wanaojali matumbo yao ndio maana tunaibiwa rasilimali zetu mchana kweupe tunazidiwa hadi na Uganda na Botswana wanapata mgao wao wa kueleweka sisi ni mazezeta kabisa
Hawezi gundua mwingine afu mkagawana sawa ,tunachokipata ndio stahiki zetu'.

Ukitaka kikubwa weka teknolojia,staff na mtaji ugundue mwenyewe
 
Nilitegemea ushangilie kuwa Sasa tutaanzisha viwanda vinavyohitaji gesi hiyo ya helium hapa nchi na gharama ya kuviendeshahivyo viwanda itakuwa ndogo kwakuwa nishati ipo hapa nchini.

Na viwanda hivyo vitaajiri watanzania wengi watakao saidia kuzalisha bidhaa za kuuzwa Nje ya nchi na kutupatia fedha za kigeni. Fedha hizo zitagharamia miradi ya maendeleo kama miundombinu mingine ya kurahisisha uzalishaji nchini. Yaani kiwango cha ubora wa maisha ya watanzania kitapanda sana.

Haya ndiyo maneno ambayo yangefaa kusikika masikini mwao watanzania kwa mujibu wa maoni yangu.

Lakini, mwenzetu mleta mada unashangilia kuuza helium Nje. Kweli twatofautiana. Ha ha hahahaha AAA!
 
Hawezi gundua mwingine afu mkagawana sawa ,tunachokipata ndio stahiki zetu'.

Ukitaka kikubwa weka teknolojia,staff na mtaji ugundue mwenyewe

Umeangalia mgao wa botswana kwenye dhahabu na madini yao ni kiasi gani? Umeona jinsi walivyoframe mikataba ya rasilimali zao? Au unaongea tu bila kufahamu wengine wanafanya nini?
 
Hizi zingeweza kuwa story zenye maana kama tungekuwa na viongozi waadirifu,tuliambiwa hizi story kipindi gesi ya songosongo inagunduliwa, wajanja wakacheza tiktak, sasa huwa hata hatuelewei gesi iliishia wapi! Tukajenga Bomba la gesi kutoka Mtwara mpaka Dar, kwenye kinu cha kufufua umeme, matokeo yake, wenye meno wakacheza tena, sasa hv tunachopata ni mgawo wa umeme.

Neema itapatikana kama wezi wa CCM watakufa, lakini kama Hawa kenge wapo hai, Kikwete, Kinana, Makamba, walioba, and their family members, firends, tusitegeme kitu.

Nchi zenye maendeleo huwezi kusikia Raid anapewa PHD ya heshima,China, Korea, SA, US, Uwezi. Kukuta upuuzi kama wa huku Bongo.

20221201_043559.jpg
 
Umeangalia mgao wa botswana kwenye dhahabu na madini yao ni kiasi gani? Umeona jinsi walivyoframe mikataba ya rasilimali zao? Au unaongea tu bila kufahamu wengine wanafanya nini?
Unadhani madini Yao Ni sawa na haya ya kwetu substandard?

Madini Yao Ni very quality na Ni mengi pia hivyo kuwa na kiburi,pia wao walishajiandaa kwenye sekta ya madini maana ndio bavkborne ya Uchumi wao lazima wakomae.

Sie pia tunaweza weka jeuri kwenye Helium na mengine ambayo yanapatikana kwenye Nchi chache ili kupata faida kiasi.
 
Serikali huwa haijengi viwanda mzee na matumizi ya hiyo gas ni kwenye mitambo, machines za MRI,viwandani na weather balloons.

Njia pekee ya kufanya viwanda bike ni kuwashawishi wawekezaji kwa kuwapa offer kibao tofauti na hapo watapeleka kwao kwenye viwanda zaidi.
 
Wa tz ndio kwanza wanazidi kutumbukia kwenye dimbwi la umasikini sijui hizi lasirimali zinawasaidia vipi?
 
Hapa nitakufa na nitazaliwa tena na nitakufa bado gesi haijaanza kuchimbwa Liganga na Mchuchuma ilianza kuimbwa bado nipo kijijini nacheza mchezo wa kuigiza nachunga Ng'ombe na kukimbizana na kujificha kwenye vichaka mpaka leo hii nina akili zangu nimezunguka nchi nzima na mataifa mengine kadha wa kadha lakini bado madini hayo yanaimbwa tu.

Hii nchi na viongozi wetu sijui nani katuloga hata hatujui ni kipi kinatufanya kubaki tulivyo na hatusogei mbele
 
Usiwe mkali bro Jaribu kupita kwenye miji inayozalisha lasirimali for a quick start...
ni mashimo na uharibifu wa mazingira
Ukiangalia kwa mtizamo huoninakosea kwa sababu Hakuna sheria inayolazimisha sehemu ya faida kubakia maeneo hayo ukiacha csr ambayo Ni kiduchu Sana.

Ukitaka Hilo tubaeili Katiba ili iwape favour kiasi kuliko ilivyo Sasa ambapo Pesa inapelekwa kapu kuu na kugawanya wanavyoona wao bila kujali maeneo ya Mali ilikotoka.
 
Unanufaika nini hata ikigundulika? Tutaendelea kushangilia hivyohivyo ila wanufaika ni vibaraka wachache tu
 
Back
Top Bottom