Njia mpya ya wizi tuwe makini, epuka kutapeliwa

Njia mpya ya wizi tuwe makini, epuka kutapeliwa

Weee jamaa ni mkorofi sana [emoji23][emoji23][emoji23]kwaiyo jamaa kakwepa kumuita dogo boda
Ukisoma huu uzi vizuri..
Utaona akili ya boda na dogo ni kama 20 na twenty 🤓🤓🤓🤓
 
Mimi Na Wife Tulipigwa Kama hivi ilikuwa hivi....
Mimi nilikuwa na Gari nauza basi nikaipost mtandaoni Facebook nauza Gari yangu ghafla akapiga mtu boss habari hiyo Gari mwisho ngapi mimi nikamwambia mwisho Mil 8 maana nilikuwa nauza 9

Baada ya mazungumzo haya akakata Simu akakaaa dk 10 akapiga Simu tena boss samahani hauwezi kuwa na namba ya fundi wa Kufunga aluminium nina nyumba yangu Ipo kwenye ujenzi bado nataka nifunge aluminium dirisha zote.

Mimi kiukweli namba ya Fundi wa aluminium nilikuwa sina Japo home nimefunga aluminium lakini namba ya fundi sina Nilipoteza maana ni miaka imepita toka huyo fundi atufungie basi nikamwambia huyo tapeli sina ngoja nimuulize wife basi baada ya mimi kumuuliza wife wife akasema anayo nikamwambia wife nipe maana yule jamaa anae taka Gari anataka afungiwe aluminium dirisha zote.

Wife Akaniambia hivi subiri kwanza nimpigie fundi wa aluminium maana huwa tukiunganisha dili la kufunga aluminium tena nyumba nzima fundi alisema kuna commission anatoa basi wife akampigia fundi aluminium akamwambia nina mteja anataka afungiwe aluminium nampa namba yako Ila usinisahau na mimi kunipa commission yangu.

Basi Baada ya wife kuongea na fundi wa aluminium ndipo tukampigia jamaa tapeli na kumpa namba ya fundi aluminium basi baada ya wife kuwaunga kwa mtindo huo zikapita dk 20 kumbe sasa katika hizo dk 20 jamaa tapeli baada ya kupewa Namba Za fundi aluminium akampigia na kumwambia namba zako amenipa dada fulani.

Nina uhitaji wa kutengenezewa nyumba yangu nzima aluminium Nipo njiani natokea dar nakuja morogoro anbako Ndiko niliko jenga Nipo kwenye private car kwa hiyo nikifika nyumbani nakupigia fundi akajibu poa boss haina shida ukifika tutawasiliana poa poa waka fanya na MAPUNGUZIANO kabisa basi baada ya kuongea hayo zikapita dk 30 jamaa tapeli akampigia Simu fundi aluminium samahani Gari yangu imepata hitilafu kidogo na nilipo hamna atm

Maana ndio pekee ninayotumia kufanya miamala naomba unisaidie kunitumia elfu 25 ili niite fundi nimlipe Wewe nakuja kukulipa huko huko nikifika (na ikumbukwe sisi hayo yote tulikuwa hatujui wife na mimi) basi fundi nae akatuma 25 kwa jamaa tapeli jamaa akatoa basi zikapita tena dk kama 15 jamaa tapeli si akapiga tena Simu Gari bado inanisumbua nitumie kama elfu 30 tena nakuja kukupa.

Nikifika moro hapo fundi akaingia ukakasi kidogo hakutuma akatupigia sisi sasa hapo ndipo mashaka ya kuhisi huu ni utapeli yakaanza hapo maana tukajiuliza mbona sisi kwetu alikuwa anataka anunue Gari kwetu halafu kwa fundi kamwambia ana Gari Yake Binafsi mara tena anamuomba fundi hela basi tukapiga Simu yake akawa hapokei fundi nae akipiga hapokei kwake pia mwisho jamaa tapeli akazina Simu.

KWA HIYO NDUGU ZANGU UTAPELI HUU UPO NA HIKI NI KISA CHA KWELI KILITUPATA SISI KWA HIYO UZI HUU WA JAMAA SIO CHAI NI KWELI UTAPELI HUU UPO NI KUWA MAKINI TU

MARAN ATHA - BWANA WETU YESU KRISTO ANAKUJA [emoji885]
Mlimrudishia fundi elfu 25 yake??
 
Wapo baadhi. Mimi kuna boda huwa ninamuagiza vitu mpaka hata vya 70k ananunua akileta namrudishia pesa yake
Yawezekana hanunui kwa cash bali anachukua duka analofahamiana/amejijengea uaminifu kwa mali kauli tu.

Mie yupo alikuwa ananiletea vifaa vya ujenzi kwa staili hiyo hata mzigo wa 80K
 
Habar ya Leo,

Naomba kushare na wa Tanzania wenzangu kuna aina ya wizi mpya umeanza kushamili.

Iko hivi, Jana nikiwa nimekaa na familia yangu majira ya jioni nilipigiwa simu na namba ngeni, nilipopokea sauti ilikuwa ya kiume ikiniita Mkuu samahani naomba unisaidie namba ya bodaboda ambaye unamwamini nahitaji aniletee chakula eneo la new park range, nikamjibu sawa mkuu muda si mrefu nikamutumia Ile namba ya bodaboda ambaye mimi huwa ananisaidia kazi

Kumbe baada tu ya kumtumia namba alimpigia yule boda akamwambia namba nimepewa na fulani hivyo nahitaji kukuagiza chips uniletee na kweli yule bodaboda alikubali akaenda kuchoma chips wakati anachoma chips alipokea simu nyingne kutoka kwenye Ile namba akamwambia naomba uniwekee shilling elf 30,000/ kwenye namba yangu hii ukiwa unaleta chips basi utakuja kuipata pesa Yako. Kweli bodaboda alifanya hivyo Kwa kumuwekea pesa hiyo kwenye namba hiyo, na baadaye aliendelea kuchoma chips

Baada tu ya kumaliza kuchoma anampigia simu namba haipokelewi, alipiga Mara 3 namba haipokelewi akasema afike eneo alilotajiwa hakukuta mtu yeyote ndipo aliponitafuta na kuniuliza nikawaambia ni kweli mtu huyo alinipigia na Mimi ndiye niliyemtumia namba

Nikajaribu kumpigia kwa namba yangu pia hakupokea, baada ya muda kidogo ndipo nilipogundua amemtapeli bodaboda kwa kupitia Mimi.

Please ndg zangu naomba share kadri uwezavyo watu wapate uelewa na kufahamu
Aisee
 
Kuna boda gani mjinga kisi cha kutuma 30000Tsh kwa mtu asiyemjua ili akaifate akienda..?

Yaani nikuazime 30000Tsh kisha uniambie nitaikuta nikija (probably baada ya 30mins kwamfano), kama unayo ya kunirudishia nikifika hapo kwanini usiitumie hiyo badala ya kuniomba yangu.?

Haiingii akili, CHAI hii.
Angemuuliza kwani hapo ulipo hakuna chips ukanunua mwenyewe tu kuliko gharama ya kukuletea.
 
Kwahiyo wewe mtu akikupigia na kusema mkuu nisaidie namba ya fulani basi unampa bila kuhoji wewe ni nani? Ulifanya kosa kubwa sana kutoa namba ya boda kwa mtu usiyemjua, na kushukuru tu alitapeliwa, wengine wanaweza kuua na kupora pikipiki.
 
Nlishawai kuandika thread ya aina hii ya utapeli [emoji1313]

Habari wakuu,

Leo nimestaajabu sana tukio lilimtokea moja ya watu wangu wa karibu wanaojishughulisha na biashara za mtandaoni. Ilikua hivi;

Alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kama mteja na alihitaji bidhaa fulani akataka afanyiwe delivery. Basi baada ya kuelewana bei. huyu jamaa yangu akaenda kununua huo mzigo mjini, then akampigia yule mteja kuwa mzigo upo tayari. Yule mteja akaomba number za bodaboda ili amuelekeze mahali anapoishi.

Sasa kwenye kumuelekeza bodaboda, yule mteja akamwambia bodaboda wakati unakuja naomba uninunulie umeme halafu ukifika nyumbani ntakupa hela yako, kwa bahati mbaya yule bodaboda hakuwa na hela, hivyo yule mteja akampigia simu jamaa yangu akiomba anunuliwe umeme wa 50k then bodaboda atarudi na hela yake.

Kutokana na hiyo conversation, jamaa yangu hakua na wasiwasi akapewa meter number akanunua umeme. Cha ajabu bodaboda alipofika mtaa aliyoelekezwa na mteja, mteja akawa hapokei simu, wamepiga simu sana ikawa ndio hivyo haipokelewi.

Jamaa yangu mpaka sasa haamini kilichotokea, sababu ni mzoefu wa biashara za mtandaoni ila hata yeye anajishangaa alikubalije kununua umeme from no where tena kwa mtu asiyemjua?

Kwa kifupi huyu tapeli alidai anaishi Mbezi Beach kwa Zena ile barabara ya Lukuvi jirani kabisa na nyumba anayoishi Diamond Platnumz.

Yule bodaboda alivyojaribu kuwauliza wale bodaboda wa kwa Zena walisema ile mitaa kwavile wanakaa washua watu wengi hutapeliwa sana kwa style hiyo.

Yaani wanastyle nyingi sana za kutapeli, kuweni makini hawa watu hawana huruma na pesa zenu.
 
Pole Sana.Mara nyingi ukiwa kwenye huitaji wa haraka au mtu wa tamaa tatizo linaanzia hapo na akili yako inakuwa Kama imefungwa Cha msingi Ni kuwa makini kila hatua unayoiga.Kuna jamaa yangu Fulani yeye alitapeliwa kupitia mke wake maana alikuwa kitu kimoja na hao matapeli akapigwa 8M,Cha msingi pesa Haina uaminifu husimwamini yeyote isipokuwa wewe tu .
 
Nyie mnao komenti sijui Chai endeleeni kubisha tu kuna matukio ya papo kwa papo unapigwa then unakaa kama Nusu sana ndio ubongo unakupa taarifa hapo umepigwa hapo umetapeliwa.

shida Watz tumekua na vichwa ngumu sana mtoa mada katupa funzo then kuwa watu humu wameanza kuhukumu mara ooo wewe huyo tapeli lenu moja pamoja na watu wote kutoa shuhuda ila bado tumekua wagumu kuelewa.

kumbuka ndege mjanja hunaswa na tundu bovu na kenge hasikii mpaka aone damu masikioni.
 
Hii ni chai ya mchana kabisa, kama sio chai basi we na bodaboda wako wote wazembe NA wala hapa hakuna utapeli.
Unapigiwa tu simu na mtu humjui unaanza kumtumia namba za watu? na huyo boda anaambiwa tu atume hela kwa mtu ambaye hamjui na anatuma?
Peleka upuuzi wako jukwaa la vichekesho
Sio Chai kaka ipo sana hiyoo

Sent from my Pixel 3 using JamiiForums mobile app
 
Habar ya Leo,

Naomba kushare na wa Tanzania wenzangu kuna aina ya wizi mpya umeanza kushamili.

Iko hivi, Jana nikiwa nimekaa na familia yangu majira ya jioni nilipigiwa simu na namba ngeni, nilipopokea sauti ilikuwa ya kiume ikiniita Mkuu samahani naomba unisaidie namba ya bodaboda ambaye unamwamini nahitaji aniletee chakula eneo la new park range, nikamjibu sawa mkuu muda si mrefu nikamutumia Ile namba ya bodaboda ambaye mimi huwa ananisaidia kazi

Kumbe baada tu ya kumtumia namba alimpigia yule boda akamwambia namba nimepewa na fulani hivyo nahitaji kukuagiza chips uniletee na kweli yule bodaboda alikubali akaenda kuchoma chips wakati anachoma chips alipokea simu nyingne kutoka kwenye Ile namba akamwambia naomba uniwekee shilling elf 30,000/ kwenye namba yangu hii ukiwa unaleta chips basi utakuja kuipata pesa Yako. Kweli bodaboda alifanya hivyo Kwa kumuwekea pesa hiyo kwenye namba hiyo, na baadaye aliendelea kuchoma chips

Baada tu ya kumaliza kuchoma anampigia simu namba haipokelewi, alipiga Mara 3 namba haipokelewi akasema afike eneo alilotajiwa hakukuta mtu yeyote ndipo aliponitafuta na kuniuliza nikawaambia ni kweli mtu huyo alinipigia na Mimi ndiye niliyemtumia namba

Nikajaribu kumpigia kwa namba yangu pia hakupokea, baada ya muda kidogo ndipo nilipogundua amemtapeli bodaboda kwa kupitia Mimi.

Please ndg zangu naomba share kadri uwezavyo watu wapate uelewa na kufahamu
...Kosa linaanzia Kwako. Wewe ulitoaje namba ya Mtu ambaye hamfahamiani ?
SI ungemuambia TU kuwa huna Boda Boda yoyote unayemjua ?
Kama Uhalifu wowote unafanyika, Kesi itaanzia Kwako, Mkuu.
 
Habar ya Leo,

Naomba kushare na wa Tanzania wenzangu kuna aina ya wizi mpya umeanza kushamili.

Iko hivi, Jana nikiwa nimekaa na familia yangu majira ya jioni nilipigiwa simu na namba ngeni, nilipopokea sauti ilikuwa ya kiume ikiniita Mkuu samahani naomba unisaidie namba ya bodaboda ambaye unamwamini nahitaji aniletee chakula eneo la new park range, nikamjibu sawa mkuu muda si mrefu nikamutumia Ile namba ya bodaboda ambaye mimi huwa ananisaidia kazi

Kumbe baada tu ya kumtumia namba alimpigia yule boda akamwambia namba nimepewa na fulani hivyo nahitaji kukuagiza chips uniletee na kweli yule bodaboda alikubali akaenda kuchoma chips wakati anachoma chips alipokea simu nyingne kutoka kwenye Ile namba akamwambia naomba uniwekee shilling elf 30,000/ kwenye namba yangu hii ukiwa unaleta chips basi utakuja kuipata pesa Yako. Kweli bodaboda alifanya hivyo Kwa kumuwekea pesa hiyo kwenye namba hiyo, na baadaye aliendelea kuchoma chips

Baada tu ya kumaliza kuchoma anampigia simu namba haipokelewi, alipiga Mara 3 namba haipokelewi akasema afike eneo alilotajiwa hakukuta mtu yeyote ndipo aliponitafuta na kuniuliza nikawaambia ni kweli mtu huyo alinipigia na Mimi ndiye niliyemtumia namba

Nikajaribu kumpigia kwa namba yangu pia hakupokea, baada ya muda kidogo ndipo nilipogundua amemtapeli bodaboda kwa kupitia Mimi.

Please ndg zangu naomba share kadri uwezavyo watu wapate uelewa na kufahamu
...Inawezekana ndio maana uko 'Very Poor,' kama jina lako ! [emoji57][emoji57]
Huko Makini kwenye Mambo ya Msingi...!
 
Hapana acha ujuaji na kupinga kila kitu. Ni kweli ni ngumu kuamini ila haya mambo yapo.

Kuna mmoja alijifanya mwalimu huku kwetu na kumpigia mtu wa stationary akijifanya kuagiza vitu vingi vya statinary na kisha akamwambia nitumie 20,000/= boda atakaye niletea hivyo vifaa vya stationary nitampa na pesa yako. Hahaha, jamaa akajichanganya na kumtumia. Jamaa alivyopokea muamala tu, akazima simu na boda alishatumwa hadi eneo alilosema watakutana ili achukue vifaa vya stationary. Hivyo vitu vipo mkuu. Usiwe unabisha.
Nilikuwa sijui kama kuna watu wana akili ndogo kiasi cha kutapeliwa kirahisi namna hiyo. Alichosema mleta mada na hiki ulichosema wewe, naomba uniamini tu kwamba litafanya kazi wa watu wenye akili ndogo sana.
 
Back
Top Bottom