Njia mpya ya wizi tuwe makini, epuka kutapeliwa

Njia mpya ya wizi tuwe makini, epuka kutapeliwa

Nlishawau kutoa kisa kinachofanana na chako ,[emoji1312]
 
Rafiki yangu kapigiwa simu na jamaa amejitambulisha kwamba wamesoma wote, na jamaa akaanza kwa kumuita jina kabisa. Ebwana baada ya kuitwa jina akarelax so akapiga naye stori kadhaa kisha jamaa akamuambia yeye amekua HR ana nafasi mbili za kazi kama ana mtu anamjua amuunge naye.

Nafasi moja inahitaji mtu ambaye hajasoma sana mshahara laki nne ya pili angalau dip au degree mshahara laki saba. Rafiki yangu akampa mshkaji namba pia akawapigia ndugu zake kuwaambia kawaunganisha na mtu.

Kilichoendelea huku ni wale mabinti kuambiwa nafasi za kazi zipo bandarini anahitajika secretary na anahitajika mtu wa clearing and forwarding so kwanza watume 25K ya reflectors. Kila mmoja akatuma, kama baada ya saa 1 jamaa akawarudia tumeni 50K ili tuchonge kibali wote wakatuma.

Akakaa kwa saa mbili akarudi akasema sasa tumeni 150K ili nimpe senior wangu coz yeye ndiye mpitisha majina. Huyu wa degree akatuma ila yule wa form four akasema pesa hiyo hana kwa muda huo. Muda huo ishakua mida ya saa 2 usiku, yule wa degree akaambiwa kesho nitakupa maelekezo wapi uje.

Kesho yake huyu rafiki yangu akaenda interview TRA simu yake aliizima siku nzima. Ananiambia alivyoiwasha saa nne usiku ziliingia SMS nyingi za lawama kutoka kwa ndugu zake, mostly kwakua kutopatikana kulifanania na yeye kuhusika na tukio.

Huu utapeli niliusikia mwaka 2017. Ila kuna mtu kakutana nao mwaka huu na akaanguka. Hoja ya kwamba uliwahi sikia aina fulani ya utapeli hivyo ni haiwezekani tukio kutokea ni hoja mfu.

Kwa sisi wa muda kidogo tunaikumbuka DECI si ndiyo? Na je hii Kalyinda ilivyotapeli watu ndiyo tuseme tukio la Kalynda ni uongo?
Hii ni chai ya mchana kabisa, kama sio chai basi we na bodaboda wako wote wazembe NA wala hapa hakuna utapeli.
Unapigiwa tu simu na mtu humjui unaanza kumtumia namba za watu? na huyo boda anaambiwa tu atume hela kwa mtu ambaye hamjui na anatuma?
Peleka upuuzi wako jukwaa la vichekesho
 
Kuna boda mmoja kapigwa 1,200,00 hivyo hivyo,ndugu zake ndio wanailipa kidogo kwa jamaa wa huduma za miamala hapa Mtaani,yeye aliagizwa utumbo.
Na Bado Kuna mtu anajua ni chai yaan wabongo bhna
 
Huyu wa Mtaani hapa yeye alipigiwa simu akaambiwa namba yako nimepewa na Mwl fulani wa Shule fulani,ambaye huyu boda wanafahamiana,basi jamaa akamwambia nichukullie utumbo kilo moja niletee,jamaa akampigia tena kuwa namba nakupa itumie 1,600,000 mimi nipo na mafundi hapa home ukifika nakupa,yule dogo akaenda kwa wakala ambaye wanafahamiana yule wakala akamwambia ipo 1,200,000 tu,dogo akampigie yule jamaa simu kuwa ipo mil 1.2 jamaa akamwambia weka hata hiyo.dogo akaweka akawasha boda ili kumfuata alipomuelekeza,kufika pale anapiga simu haipokelewi,pesa imeenda ule utumbo kabaki nao.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Habar ya Leo,

Naomba kushare na wa Tanzania wenzangu kuna aina ya wizi mpya umeanza kushamili.

Iko hivi, Jana nikiwa nimekaa na familia yangu majira ya jioni nilipigiwa simu na namba ngeni, nilipopokea sauti ilikuwa ya kiume ikiniita Mkuu samahani naomba unisaidie namba ya bodaboda ambaye unamwamini nahitaji aniletee chakula eneo la new park range, nikamjibu sawa mkuu muda si mrefu nikamutumia Ile namba ya bodaboda ambaye mimi huwa ananisaidia kazi

Kumbe baada tu ya kumtumia namba alimpigia yule boda akamwambia namba nimepewa na fulani hivyo nahitaji kukuagiza chips uniletee na kweli yule bodaboda alikubali akaenda kuchoma chips wakati anachoma chips alipokea simu nyingne kutoka kwenye Ile namba akamwambia naomba uniwekee shilling elf 30,000/ kwenye namba yangu hii ukiwa unaleta chips basi utakuja kuipata pesa Yako. Kweli bodaboda alifanya hivyo Kwa kumuwekea pesa hiyo kwenye namba hiyo, na baadaye aliendelea kuchoma chips

Baada tu ya kumaliza kuchoma anampigia simu namba haipokelewi, alipiga Mara 3 namba haipokelewi akasema afike eneo alilotajiwa hakukuta mtu yeyote ndipo aliponitafuta na kuniuliza nikawaambia ni kweli mtu huyo alinipigia na Mimi ndiye niliyemtumia namba

Nikajaribu kumpigia kwa namba yangu pia hakupokea, baada ya muda kidogo ndipo nilipogundua amemtapeli bodaboda kwa kupitia Mimi.

Please ndg zangu naomba share kadri uwezavyo watu wapate uelewa na kufahamu

Ulimrudishia dogo 30,000 yake? Maana kosa ni lako, nafikiri kwanza tuanzie hapo???!!!???
 
bodaboda wengi ni waha na waburundi anaweza akatapeliwa
 
Tujihdhari na PESA maana Bora Mtu umpe kitu kingine na sio PESA Kama pesa.
 
Habar ya Leo,

Naomba kushare na wa Tanzania wenzangu kuna aina ya wizi mpya umeanza kushamili.

Iko hivi, Jana nikiwa nimekaa na familia yangu majira ya jioni nilipigiwa simu na namba ngeni, nilipopokea sauti ilikuwa ya kiume ikiniita Mkuu samahani naomba unisaidie namba ya bodaboda ambaye unamwamini nahitaji aniletee chakula eneo la new park range, nikamjibu sawa mkuu muda si mrefu nikamutumia Ile namba ya bodaboda ambaye mimi huwa ananisaidia kazi

Kumbe baada tu ya kumtumia namba alimpigia yule boda akamwambia namba nimepewa na fulani hivyo nahitaji kukuagiza chips uniletee na kweli yule bodaboda alikubali akaenda kuchoma chips wakati anachoma chips alipokea simu nyingne kutoka kwenye Ile namba akamwambia naomba uniwekee shilling elf 30,000/ kwenye namba yangu hii ukiwa unaleta chips basi utakuja kuipata pesa Yako. Kweli bodaboda alifanya hivyo Kwa kumuwekea pesa hiyo kwenye namba hiyo, na baadaye aliendelea kuchoma chips

Baada tu ya kumaliza kuchoma anampigia simu namba haipokelewi, alipiga Mara 3 namba haipokelewi akasema afike eneo alilotajiwa hakukuta mtu yeyote ndipo aliponitafuta na kuniuliza nikawaambia ni kweli mtu huyo alinipigia na Mimi ndiye niliyemtumia namba

Nikajaribu kumpigia kwa namba yangu pia hakupokea, baada ya muda kidogo ndipo nilipogundua amemtapeli bodaboda kwa kupitia Mimi.

Please ndg zangu naomba share kadri uwezavyo watu wapate uelewa na kufahamu
Hapa kintelejinsia wewe na uliempa namba shauri lenu ni moja ,unajidai tu kwamba humjui unamjua fika so wewe ni player or joker hizi ni mbinu unazitumia wewe na kuwakwamisha hao boda boda wako senti zako .Haiwezekani hata kidigo mimi ukanipigia simu nikupe number ya boda boda wangu bila mm kukufahamu wewe.Huo mchezo wacha .What Goes Around .Comes Around.
 
Pole sana. Next time uliza maswali ya kutosha ujiridhishe kabla ya kutoa namba za watu wanaokuhusu. Unaweza kuja kuhusishwa na matukio makubwa ya uhalifu ukajikuta pabaya.
 
Hebu wenkeni namba za hao matapeli hapa. Mnaogopa nini?
 
Kuna boda gani mjinga kisi cha kutuma 30000Tsh kwa mtu asiyemjua ili akaifate akienda..?

Yaani nikuazime 30000Tsh kisha uniambie nitaikuta nikija (probably baada ya 30mins kwamfano), kama unayo ya kunirudishia nikifika hapo kwanini usiitumie hiyo badala ya kuniomba yangu.?

Haiingii akili, CHAI hii.
Hapana acha ujuaji na kupinga kila kitu. Ni kweli ni ngumu kuamini ila haya mambo yapo.

Kuna mmoja alijifanya mwalimu huku kwetu na kumpigia mtu wa stationary akijifanya kuagiza vitu vingi vya statinary na kisha akamwambia nitumie 20,000/= boda atakaye niletea hivyo vifaa vya stationary nitampa na pesa yako. Hahaha, jamaa akajichanganya na kumtumia. Jamaa alivyopokea muamala tu, akazima simu na boda alishatumwa hadi eneo alilosema watakutana ili achukue vifaa vya stationary. Hivyo vitu vipo mkuu. Usiwe unabisha.
 
Hapa kintelejinsia wewe na uliempa namba shauri lenu ni moja ,unajidai tu kwamba humjui unamjua fika so wewe ni player or joker hizi ni mbinu unazitumia wewe na kuwakwamisha hao boda boda wako senti zako .Haiwezekani hata kidigo mimi ukanipigia simu nikupe number ya boda boda wangu bila mm kukufahamu wewe.Huo mchezo wacha .What Goes Around .Comes Around.
Acha pumbavu huu ni utapeli upo watu wanainiwa daly huna haja ya kubisha broo
 
Nilidhani imetokea Nyeregete huku mpaka nilipoona New Park Range!

Huyo tapeli akamwambia boda kwamba namba kapewa na fulani!
 
Mimi Na Wife Tulipigwa Kama hivi ilikuwa hivi....
Mimi nilikuwa na Gari nauza basi nikaipost mtandaoni Facebook nauza Gari yangu ghafla akapiga mtu boss habari hiyo Gari mwisho ngapi mimi nikamwambia mwisho Mil 8 maana nilikuwa nauza 9

Baada ya mazungumzo haya akakata Simu akakaaa dk 10 akapiga Simu tena boss samahani hauwezi kuwa na namba ya fundi wa Kufunga aluminium nina nyumba yangu Ipo kwenye ujenzi bado nataka nifunge aluminium dirisha zote.

Mimi kiukweli namba ya Fundi wa aluminium nilikuwa sina Japo home nimefunga aluminium lakini namba ya fundi sina Nilipoteza maana ni miaka imepita toka huyo fundi atufungie basi nikamwambia huyo tapeli sina ngoja nimuulize wife basi baada ya mimi kumuuliza wife wife akasema anayo nikamwambia wife nipe maana yule jamaa anae taka Gari anataka afungiwe aluminium dirisha zote.

Wife Akaniambia hivi subiri kwanza nimpigie fundi wa aluminium maana huwa tukiunganisha dili la kufunga aluminium tena nyumba nzima fundi alisema kuna commission anatoa basi wife akampigia fundi aluminium akamwambia nina mteja anataka afungiwe aluminium nampa namba yako Ila usinisahau na mimi kunipa commission yangu.

Basi Baada ya wife kuongea na fundi wa aluminium ndipo tukampigia jamaa tapeli na kumpa namba ya fundi aluminium basi baada ya wife kuwaunga kwa mtindo huo zikapita dk 20 kumbe sasa katika hizo dk 20 jamaa tapeli baada ya kupewa Namba Za fundi aluminium akampigia na kumwambia namba zako amenipa dada fulani.

Nina uhitaji wa kutengenezewa nyumba yangu nzima aluminium Nipo njiani natokea dar nakuja morogoro anbako Ndiko niliko jenga Nipo kwenye private car kwa hiyo nikifika nyumbani nakupigia fundi akajibu poa boss haina shida ukifika tutawasiliana poa poa waka fanya na MAPUNGUZIANO kabisa basi baada ya kuongea hayo zikapita dk 30 jamaa tapeli akampigia Simu fundi aluminium samahani Gari yangu imepata hitilafu kidogo na nilipo hamna atm

Maana ndio pekee ninayotumia kufanya miamala naomba unisaidie kunitumia elfu 25 ili niite fundi nimlipe Wewe nakuja kukulipa huko huko nikifika (na ikumbukwe sisi hayo yote tulikuwa hatujui wife na mimi) basi fundi nae akatuma 25 kwa jamaa tapeli jamaa akatoa basi zikapita tena dk kama 15 jamaa tapeli si akapiga tena Simu Gari bado inanisumbua nitumie kama elfu 30 tena nakuja kukupa.

Nikifika moro hapo fundi akaingia ukakasi kidogo hakutuma akatupigia sisi sasa hapo ndipo mashaka ya kuhisi huu ni utapeli yakaanza hapo maana tukajiuliza mbona sisi kwetu alikuwa anataka anunue Gari kwetu halafu kwa fundi kamwambia ana Gari Yake Binafsi mara tena anamuomba fundi hela basi tukapiga Simu yake akawa hapokei fundi nae akipiga hapokei kwake pia mwisho jamaa tapeli akazina Simu.

KWA HIYO NDUGU ZANGU UTAPELI HUU UPO NA HIKI NI KISA CHA KWELI KILITUPATA SISI KWA HIYO UZI HUU WA JAMAA SIO CHAI NI KWELI UTAPELI HUU UPO NI KUWA MAKINI TU

MARAN ATHA - BWANA WETU YESU KRISTO ANAKUJA [emoji885]
 
Back
Top Bottom