Njia mpya ya wizi tuwe makini, epuka kutapeliwa

Njia mpya ya wizi tuwe makini, epuka kutapeliwa

Unagawaje namba ya mtu pasipo ridhaa yake? Je angeitwa kwebda kuporwa na kuuawa ungehusika tu.
PERIOD
 
Yaani namba ya mtu anakupigia humfahamu halafu unamuunga na Boda? Yaani Mimi ningemuuliza maswali mengi Sana na hata anipe majibu gani nisingempa namba. Shukuru Mungu hawakumwibia Bodaboda Boda yake au kwenda kumuua wachukue Boda. Yaani ingekuta muda huu unaisaidia Jamhuri.
Ukweli huu haupingiki hata kwa unafiki.
 
Kutoa namba ya simu ya mtu kwa mtu mwingine bila ridhaa ya mwenye namba husika ni kosa kisheria
 
KAMA HAIJAKITOKEA UTASEMA NI CHAI,ILA NI UKWELI MTUPU HUO NDIO UTAPELI WA SASA WA KUWAPIGA BODABODA BADALA YA TUMA KWA NAMBA HII,WANAJUA BODABODA MFUMO WAO WA KAZI WANATUSAIDIA WATEJA WAO KUNUNUA MAHITAJI HATA KUTUINGIZIA PESA TUNAWARUDISHIA WAKIFIKA NDO MAANA INAKUWA RAHISI KUTAPELIWA BILA KUHOJI ILIMTOKEA MUME WANGU AKAJIKUTA ANALIPA PESA KWAKUA ALIMUUNGA BODABODA NA TAPELI.

TAPELI ALITUMA MESEJI MIMI MWALIMU UNA NAMBA YA BODABODA UNITUMIE KUNA VITU NATAKA ANINUNULIE ANILETEE,MUME WANGU ANAJUANA NA WALIMU WENGI,NA HUWA HA SAVE NAMBA ILA WAO WANA NAMBA YAKE NA KATUMIWA MESEJI AKIWA BUSY NA KAZI ZAKE HAKUWA NA SHAKA AKAMTUMIA TAPELI AKAMWAMBIA NIMWAMBIE NAMBA KANIPA NANI MUME WANGU AKAMTAJIA MWAMBIE FLANI, DAKIKA KADHAA TAPELI AKATUMA MESEJI AKAMWAMBIA SIMPATI HUNA NYINGINE MUME WANGU AKAAMPA NAMBA YA BODABODA WANGU,TAPELI AKATUMA MESEJI ANASEMA YUKO MBALI ANA ABIRIA HAUNA NAMBA YA BODABODA MWINGINE,MUME WANGU AKASEMA SINA MAONGEZI YAKAISHIA HAPO.

KUMBE UPANDE WA 2 ALIMPATA BODABODA WA 1 AKAMWAMBIA NIMEPEWA NAMBA NA MTU FLANI UNAMJUA BODABODA AKASEMA NDIO NAMJUA TAPELI AKAMUAGIZA TAMBI NA CARTOON 1 YA MAJI AKAMUELEKEZA SEHEMU YA KUPELEKA KIDOGO AKAMPIGIA NIINGIZIE PESA KIASI FLANI UKIJA NITAKUPA BODABODA AKAMTUMIA KAFIKA ENEO ALOMWAMBIA ANAPIGA HAPOKEI PALE NDIO AKAGUNDUA KISHA TAPELIWA AKARUDI OFISINI KWA MUME WANGU KUMWAMBIA NDIPO MUME WANGU IKABIDI AMLIPE BODABODA HASARA ALOINGIA NA AKAMPIGIA BODABODA WANGU KUMPA TAHADHARI AKASEMA JAMAA ALINIPIGIA AKASEMA UMEMPA NAMBA ANATAKA MAJI NIMPELEKEE NIKAMWAMBIA NA ABIRIA NIMETOKA KIJIWENI NIMERUDI AKAPIGA TENA NILETEEE MAJI NA NIINGIZIE PESA NJOO SEHEMU FLANI NITAKUPA PESA YAKO NIKAMWAMBIA MIE SINA PESA AKASEMA BODABODA UNAKOSAJE PESA NIKAMWAMBIA SEHEMU ULIPO MADUKA KIBAO NA WAKALA WEWE CHUKUA MAJI INGIZA PESA MIE NITAKUFATA NIKUPELEKE JAMAA AKAMWAMBIA UMESHTUKA WAJIFANYA MJANJA BASI AKAKATA SIMU AKAMWAMBIA MUME WANGU MIE MPAKA MTU NIMJUE NDO NAWEZA MTUMIA PESA SIO MTU TU AHATA KAMA KAKUTAJA WEWE BASI AKAWA KAPONA HIVYO MSISE TU CHAI CHAI.
 
Kuna boda gani mjinga kisi cha kutuma 30000Tsh kwa mtu asiyemjua ili akaifate akienda..?


Yaani nikuazime 30000Tsh kisha uniambie nitaikuta nikija (probably baada ya 30mins kwamfano), kama unayo ya kunirudishia nikifika hapo kwanini usiitumie hiyo badala ya kuniomba yangu.?

Haiingii akili, CHAI hii.

Wala siyo chai..

Mfano sisi tunauza bidhaa fulani mtandaoni
Huwa wanapiga anaweka list ya bidhaa anazohitaji, kisha anakwambia mpe boda

Ukishampa namba ya boda anamwambia nipo hotel hamna Mpesa around niwekee 30,000 ukifika hapa nakupa cash, Boda anatumia uaminifu wake kwangu anakubali kumwekea akifika Eneo la hotel anakula block..
 
Kuna boda gani mjinga kisi cha kutuma 30000Tsh kwa mtu asiyemjua ili akaifate akienda..?


Yaani nikuazime 30000Tsh kisha uniambie nitaikuta nikija (probably baada ya 30mins kwamfano), kama unayo ya kunirudishia nikifika hapo kwanini usiitumie hiyo badala ya kuniomba yangu.?

Haiingii akili, CHAI hii.

Anakuwa anamaanisha ana cash yeye anataka Float, kutokana na kushinda kufika dukani anaona bora amwagize boda anaekuja kuleta chips.
 
Hii Kali Sana,
Ila, ilibidi, ushituke umuulize kwani, we jirani, waitwa nani?
Maana number za, boda tunatoa kwa watu tunaowajua.
 
Hao matapeli wakikamatwa wafirwx tu.
Tumechoka kila siku kusoma habari zao..
 
Watanzania ujinga sijui utaisha lini.


Unagawa namba ya watu wengine bila kumjua huyo unaemgawia namba.


Hujui kuwa huyo bodaboda kama angepata shida na wewe ungeungwa kama sehemu ya uhalifu.
 
Back
Top Bottom