Niusaidiaje mchepuko utulie na mkewe?

Ningekuwa sina mtu isingekuwa shida, kuondoka kagoma namtishia kumlipua kwa mkewe wala hatishiki ila akinilipua mm ndo basi nawaza kujilipua kabla hajanilipua ila sijui Kama ntaeleweka, yamenifika haswa.

Angelita inaonekana wewe hujifunzi kutokana na makosa, sasa huyu kijana uliye naye sasa umeisha mjaza moyoni, what if akikutelekeza. Mpende kwa dhati muoaji (ila kama bado una enjoy ujana hutamuona muoaji) na sio kila mwanamume anayesema nakupenda. Kumbuka nakupenda ya mwana.ume may mean a lot - nakutamani, nakutaka, nakupenda, umenivutia, nakuchukia, anything. Sorry wanaume.
 
Well ana weza kuusaidia mchepuko utulie tuliiiiiiiiiiiiiii kama majiya mtungi. And i was thinking of EXTORTION and BLACK MAIL, he will be too broke and afraid to sleep arround. It is bloody difficult but it can be done!

Duuu! Wewe lara1 ni jambazi wa mapenzi. Utafanya wanaume wawaogope wanawake!
 
mbona simpo sana. wewe jitahidi uanzishe urafiki na mkewe, jamaa lazima ataslow down

daaaah mkuu ka unanijua vile! hii ndo dawa yangu always, mtu anayejifanyaga pendapenda mi hiwa natafuta kumjua mkewe au mchumba...!!!

nikimpata tu kwisha habar yako!! najitahid niwe karibu nawe halafu mtu anatoka ndukiiii! from there me tuliiiii naendelea kula maisha
 
Hahahahaaa! SASA ALIE OLEWA KAPATA NINI KAMA BADO MUME ANAPIGIA MAGOTI NYUCHI HUKU NJE? Manake naona ndo kala hasara zaidi. Atazaa mitoto haramu mpaka basiii.

Swali ni je akipigia goti hiyo kitu anapewa na angelita hata sasa?
 
Nenda kwa mke wake kisha jitambulishe kuwa wewe ni mchepuko. Then tukutane hapa hapa kwa ajiri ya mrejesho!

Usifanye hivyo ni hatari kwako. Utashindwa kujibu baadhi ya maswali halafu atakuitia mashoga zake wakushushue.
 
daaaah mkuu ka unanijua vile! hii ndo dawa yangu always, mtu anayejifanyaga pendapenda mi hiwa natafuta kumjua mkewe au mchumba...!!!

nikimpata tu kwisha habar yako!! najitahid niwe karibu nawe halafu mtu anatoka ndukiiii! from there me tuliiiii naendelea kula maisha
HAHAA good approach, hapo hawezi kuwa kung'ang'anizi tene
 
Bado nashangaa sana, kila ninapo_ona majina ya wakristo mkiendekeza dhambi, tena una mshuhudia shetani kiuzembe kwa kutaka ushauri mh!!.

Hiyo ni dhambi tu angelita, hakuna ushauri mzuri zaidi ya kusema /sasa basi/ kisha ingia chumbani mwako ongea na Mungu wako akupe msamaha, siyo kuja kutuletea udhaifu wako hapa and you raise evil to the win, Noooooooo !
 
Kajambeee huko, dhambi zako zimekushinda zawrngine zinakutoa povu. Wale ndugu zako wasioolewa wameishia kuzalishwa nyumbani huwaoni ama?????

Embu nitolee giza mtoto mdogo mie hata hiyo 25 naisikia kwa wengine, Tengeneza ww urafiki na Mungu kama unaweza mwisho wa siku kila mtu na msalaba wake, hunijui sikujui huna ushauri pita mbali usinimwagie povu lako hapa.

Ukitaka kupata yaliyojaza moyo wa mtu, mkoroge! Sasa angelita ndio maana jamaa alikutosa, kama una uwezo wa kufungua mdomo kiasi hiki huyo mwanaume wa kuendelea kukufuata simuoni, labda kama umempa "ndele".
 
well said my dea...nimekulavu bureeeeee................santeeeeeee
Hahahahah angelita wewe ni mtoto?!

Usijidanganywe mwaya, huyo jamaa is just taking advantage of you. Hakuna cha kuwa taaban wala nini. I mean think about it, mmekutana akiwa na mchumba, mkawa pamoja na akakolea kweli kweli lakini recently ameamua kumuoa huyo aliyekuwa anajuta kuna na commitment nae?! We unaona nini hapo?!

Kama angekuwa hoi,taaban or whatever he tells you aingemuoa huyo aliyemuoa bali angekuoa wewe. Sababu ya kumuoa aliyemuoa ni kwamba ANAOGOPA KUMPOTEZA ila wewe hana wasiwasi na wewe hata kidogo. Na ndio maana wewe unajua kuhusu mwenzio na anakutumia apendavyo bila kuwa na future na wewe wakati mwenzio ana-treat-iwa delicately.

Fungua macho uone kisha utafute maisha yako mwenyewe. Huyo mwanaume anakuona wewe ni ----- na anajua huna ujanja juu yake. Wewe ndo uko taaban, amka mama utafute na wewe wa kukufia mpaka atake kuji-commit kwako na sio kwa mwenzio.
 
dada nakuomba jitambue na kujua thamani yako..mwanzo unasema ulikuwa unadate na mtu mzima ambaye nae ni MUME WA MTU...ukaanza kumcheat na huyo MCHUMBA WA MTU ambaye kwa sasa naye ni MUME WA MTU....my dear TAFUTA WAKO na muombe Mwenyezi Mungu akujaalie wepesi katika hilo...tambua kuwa HUNA THAMANI HATA KIDOGO kwa huyo mkaka kwani ungekuwa na thamani angeghairi kumuoa huyo mchumba wake na kuamua kukuoa wewe..lakini WHAT HAPPENED? kamuoa mchumba wake....sasa bibie ushauri wa bure tu, mtishie utamwambia mkewe na kwamba akuache kwa kuwa na wewe umefika wakati unahitaji kutengeneza familia yako na kwamba una mchumba wako tayari ambaye hapendi mahusiano yako na huyo mkaka.....ACHANA NAE NA USHINDE HUO UDHAIFU WAKO MY DEAR.....kila la kheri!
 
mwaka na miezi kazaa tangu nimjue sasa, nakumbuka kuna tatizo lilitokea ikabidi nimuone yeye ofisini kwao, ndo ukawa mwanzo wa penzi letu kuchipua.

Aliniweka wazi kwamba ana mchumba, ila yuko nje ya mji haikuwa shida sababu nilikuwa na stress zangu za mapenzi niliona nimepata pakuzitolea labda nitamsahau yule aliyekuwa mpenzi wangu, kwa takribani miaka minne sasa nitamsahau na kupata pakuanzia.

Ingawa sikuwa single kwa wakati huo, kuna mtu ambaye nilikuwa naye kwa muda mrefu, alinizidi umri sana na ni mume wa mtu, nilihitaji mtu wakuwa naye huru na kwakuwa huyu mchumba wake alikuwa mbali na mie moyo wa kupenda ulikufa sikuona shida kusogeza muda naye.

Kadiri siku zilivyosonga niliona mwenzangu anazidi kukolea, ikabidi nikate mawasiliano, mana ilifika kipindi anajutia kuwa kwenye commitment.ni mwezi sasa na siku kazaa tangu aoe, bado ananiganda anataka tuendelee na mahusiano, binafsi siko tayari kuendelea naye nishatumia njia zote kumkatisha tamaa bado kang'ang'ana.

Tafadhari wale wakurusha mawe pita mbali, hapa ni ushauri jinsi ya kunusuru ndoa ya watu idumu tu.
ver simple method...anzaa kumchuna vitu vikubwa vikubwa akununulie gari,mara akujenge nyumba akusaidie kumpeleka mdogo wako chuo kikuu,,automatic atajiengua mwenyewe
 
Ndio nyinyi mnafeli mtihani kwa genye zenu zakuharakia kujibu bila kusoma vizuri.

Soma bandiko vizuri uelewe, aliyekwambia nilitaka anioe nani, huna ushauri pita mbali nilishatoa onyo mwisho wa bandiko.

Binti kupunguza mihemko na munkari..hili jukwaa lina watu tofauti na wanao fikiri tofauti..na ni wazi huwezi kupendezwa na kila mchango hivyo busara ni kukaa kimya na kupuuza unayo yaona yasiyo yamsingi!
Kuweka angalizo mwisho hakuwafungi wenye mitazamo usiyo ipenda kuchangia! Kuwa mpole.
 
Back
Top Bottom