Niulizeni mimi yaliyonikuta Afrika Kusini

New ID l

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
248
476
Hello everyone....
Hope U mzima....
:TruE stoRy:

Kwa kawaida vijana wengi huwa tuna ndoto ya kuvuka border na kuingia upande wa pili haswa bala la ulaya" nchi za kimagharibi kwa ujumla....

Wala sikuujali ule msemo mkataa kwao ni mtumwa
Nilihakikisha nafanya juu chini
ili niweze kupata vitu muhimu vitakavyonisaidia huko niendako.

Haikuwa rahisi kuvipata..but nilijitahidi na hatimae nikapata Passport' driving license,
sikuishia hapo2...bali nilikwenda kusomea umeme wa magali' ikiwemo na udereva pia.

Vyote hivyo vilitokana na ushawishi wa brother wangu fulani iv" ambae yeye alikuwa mstari wa mbele ktk kunishawishi nisepe
nikastruggle mbele....

Ilipita km mwaka m1 iv' tangu nivipate vile vitu uku nikizichanga changa kama nauli etC.
Kwa bahati pale kitaani kuna jamaa fulani yeye pia ni baharia,
simaanishi melini......so' alirudi kutoka Mozambique....hivyo nilikutana nae km mjuavyo tena'
Wabongo hatukosagi ya kuongopa...basi akahadithia aliyokutana nayo huko...ya uwongo na kweli ilimradi mbwembwe2....

Nami nikamchana kuhusu dhamira yangu....
Kwa kweli hakuwa mchoyo ktk kunishawishi juu ya dhamira yangu, ingawa mm nilimweleza kuwa sitamani kuzunguka in Africa....
Akasema: kama unataka kwenda America' Europe...eTc,
basi ni vyema safari yako ukaiyanzia South Africa...kuliko hapa Bongo....coz hapa #wakuda_sana.

Pia hakusita kuniuliza km nina ndugu au marafiki huko niendako...nikamjibu aah...me baaria bhana.....!
Akanisisitiza niende South Africa na kusema kuwa' kule ukifika2...wabongo lazima wakupokee kwa namna yoyote ile.

Dah....sikutaka kupinga coZ" niliamini kuwa south pia ni kuzuri
hivyo naweza kuishi kwa muda then nitaendelea mbele.

Nilianza kuwa mwepesi baada ya kuona kuna uwezekano ya kupata company ktk safari yang*

Yule brother wangu mwengine nae alinipa moyo kwa kusema:
ukiwa tayari...niambie me kuna rafiki yangu anaishi huko South
nimeshampanga tayari au vp?!
Huwa namuitika poa bro+

Baada ya km wiki2 nilipata kiasi fulani cha pesa ambacho kingeweza kunifikisha South .A
bila tabu yoyote.
Hapo ni wiki2 tangu kuonana na yule baharia.....

Nikamfuata na kummwambia: ebhana me nimeshapata kisi kadhaa cha pesa....alafu si unajua tena pesa haikai ndani mkuu...?!
Akasema: ni kweli' sasa tunafanyaje na mimi michongo haijakaa level....tunge sepa wote jamaa yangu dah!

Alimalizia kwa kusema:
au km vp...wewe tangulia mimi nitakuja baada y siku chache2,
Komaa baalia wangu....usiwasikilize hao wakatishaji tamaa au vp baalia?!
Nikamjibu: aah' wewe...hizi ndoto ni za usiku na sio za mchana...so' zina ukweli ndani yake hahaha.

Siku mbili zijazo...akanielekeza namna ya kupita border 2 border...na hata pale nitakapo fika" nifanyeje....YeaH+

Kesho yake bila kulemba mzee..
Asubuhi nikaenda pale Mnazi mmoja....kufuatilia #yellow_fever
kumradhi km nimekosea hizo herufi,
Baada ya pale nikamfuata yule baalia...nikamuonyesha ile kadi,
Akasema: sasa inabidi ukakate tiketi ya kesho kuelekea Zimbabwe.....

Faster....sikuvuta pumzi...nikapanda gari hadi Ubungo, kufika pale Ubungo..
nikaonana na Vishoka wa pale terminal...kwa bahati nikaonana
kijana mmoja mstaarabu kisi chake....akanisaidia kwenye zoezi la kukata hile tiketi.....
Tiketi ilikuwa inaonyesha kuwa..
gari itaanza safari saa 12:00 asubuhi•

Yes" nikarejea kitaani huku roho inadunda maana nahisi ninachokifanya si kwa akili yangu....ukizingatia hakuna ndugu yangu yeyote niliyemuelezea juu y safari yangu yote kwa ujumla...
Ispokuwa ni wale wawili2
Brother & Baharia...only!

Niliporudi" nikamfuata yule Brother...nikamwambia kuwa
me niko tayari..so' fanya mpango ili kesho nianze safari
wakati huo nakumbuka jana yake nilimueleza kuwa kesho nakwenda kukata tikeketi....

YaP;
Akasema: dah! Huyu jamaa mwenyewe naona analeta mashauzi kinyama i'see....
Hata simuelewi...nimeona bola nimpotezee2

Palepale nilianza kupoteza nguvu kiasi fulani....ingawa ile safari niliipanga mwenye, lkn
kutokana na ushawishi wao" ndio umenifanya nikate tiketi haraka haraka...

Aah! Nilijipa moyo na kusema kuwa mimi ni baalia bhana...
Just do it...niliieleza hivyo nafsi yangu.....!

Nakumbuka...sikulala nyumbani siku hiyo...nilikwenda kulala kwa ndugu yangu fulani...mtaa km wa 4 kutoka home....yule ndugu wala hakujua kuwa nina safari kesho yake....
Pia kwa bahati....yule ndugu alikuwa nakiparty kwa friends zake....hivyo nilimtaka aniachie Cd nyingi pale mezani" nitazame weeh mpaka asubuhi.

Yes' Ilifanyika hivyo, hata ilipofika saa kumi kasoro....nilikwenda kizungu siku
hiyo' nilioga faster...nilipofika stand nilihisi kuchelewa kupanda daladala...so' nilikodi Bodaboda to > Ubungo terminal.

Nilihakikisha ninaripoti sehemu husika...yeah nilisubiri muda...
Na muda ulipotimia nikaingia ndani ya basi...huku nikijishauri
au nirudi....[ @£$ ]
Nikajisemea moyoni...huwenda
wachawi wameshajua kuwa nakwenda kuzoa mipesa huku..
Na ndio maana nafsi inakuwa nzito...hahaha...lol.

Na hatimae taratibu basi lilianza kutoka >>>>
mahabusu to mahakamani

Je' wataka kujua kilichonikuta
njiani....?

Gonga likes nyingi...
Then tukutane part 2

Tooth Brush
#$$$
 
Back
Top Bottom