Nairobi to Jozi?

beluwa

Member
Jul 15, 2020
77
78
Nilikua Dar for a month hapo 2022, lakini kweli Dar pagumu aisee, ila nilijaribu niwezavyo kuhustle, kawni Ilinibidi nirudi Kenya, licha ya moja mbili tatu zinazotuma nipachukie hapa Kenya SANAA! Sababu zenyewe ambazo zikasababisha niondoke na kwenda Dar.

Imefika mda tena masaibu yangu Kenya kama hapo awali yamerejea, nilivoondoka ghafla kwenda Dar, sasa nataka niende Jozi for good uhuni wa Kenya unitokomee kabisa, siwazi kurudi tena Kenya Ng'o!

Licha ya hayo, nikitoka Dar kurudi Kenya maisha ya Dar yaliposhindikana, nilikuwa nimechelewa nikapitisha pasi kwa siku mbili, nilikua nimepewa pasi ya mwezi na Customs.

Zaidi ya hayo, hapo mwanzoni nikitoka Kenya kuenda Dar, hao customs walikula hongo elfu taano za kenya (eti ya kulipia mhuri), nikasema dah,, hamna shida, nitafika Dar nifanye biashara nirudishe hasara. Ng'o, hustle ikakua ngumu, nikasema sina budi kurudi Kenya. (BAada ya mwezi na siku mbili).

Ule mwezi ulipoisha nikaanza safari ya kurudi Kenya. Wale polisi wa barabara ambao kucheck pasi before ufike Namanga walinikamata kwa kupitisha siku kwa ku-overstay. Walikula hongo, bali niliwasumbua, bei yao ya elfu kumi za kenya ikashuka ikawa elfu 2 za kenya.

Hio jambo ikasababisha nisiingie office za custom pale namanga ili wabonyeze clearance na kuniwekea mhuri kuwa nimetoka TZ. Sababu ya kutoingia custom ya namanga ilikua vile wao walinikula hongo ya 5K nikiingia, na jinsi polisi wa border walikula hongo nikiwa on my way kutoka Tanzania, nikajua kuingua huko customs itakua kujipeleka kichinjioni. So, record yangu sasa hivi ni kuwa technically niko Tanzania (since 2022), kwa kuwa siku-clear na customs.

Sasa suala ni hili. Kuenda Jozi, lazima nipitie Tanzania, sina hela ya kutosha ndege, lazima niabiri basi. Nataka ushauri vile nita-navigate customs bila kusumbuliwa, ila nashuku nitaitishwa hongo kali kutokana na dhambi zangu nyingi!!!!

Je pia, kuna basi za kutoka Arusha mpaka border ya Zambia, badala niingie kwenda Dar, nichukue basi ya kwenda Zambia? Naona kama hapo ni kurudi nyuma!

Je, kuna truckers ambao hawaezi mind? Bora niregeshe mkono? Actually kuna mmoja apa Kenya alinipa hio advice na akapromise kunipa connection lakini alikua jamaa wa Facebook skuizi simwoni

Ayaa, twende kazi.
 
Back
Top Bottom