Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
10,434
Reaction score
17,204
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg

Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia.
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Smart Guy Mapank Mamaya Extrovert
Niaje mazee!?
Hivi ushawazaga kwenye concert kubwa kubwa zile mpangilio wa sound hua niaje?
Hebu check mfano sound hiyo apo kwenye stage
Kwenye matamasha kama haya
Unakuta kuna amplifier 40-50-60
Then kuna speaker kama 80
Sound inayotoka hapo mzee ni balaa!
Ushajiuliza waya za signal hua ngapi! Si zitakua uchafu!
Vipi kama ikiungua au kupata hitilafu moja ikiwa show inaendelea?
Stay nkupe mchongo!

Ukisikia sound engineer kwa wenzetu huko ujue kweli wanapiga kazi!
Kuongoza vyombo vyote hivi ,inahitajika akili na utimamu
Japo wenzetu ki teknolojia wako mbali

Kwanza kabisa wenzetu kwa sasa hawatumii tena haya ma amp ya CAT
Sio mbaya bali hazipo ki teknolojia
Wanatumia amp kama D10Q!
Unajua kwanini kwasababu zinauwezo wa kupokea ethernet
So mfano una amplifiers zako 50 zote engineer anaweza kuzi control kwa kupitia computer yake!
Anaweza kuizima au kuiwasha.. kusoma joto la amplifiers na kuangalia kama inafanya kazi kwenye normal condition

Kwa mfano show inaendelea bahati mbaya amplifiers moja ikazingua
Bado kuna kua na amp kama 5,6-10 ambazo zinakua connected but standby
Kwa maana ya kua ndani ya nusu sekunde inawezakana kuzima amp hi na ikaongia hi!
Yaana ile dj anasema mama aminaaaa
We unajibu huku nyuma wamezima amp zote wamewasha zingine ndan ya sekunde !!!!

Lakini pia hawatumii cable zs kawaida kusafilisha signal bali hutumia ethernet kusafilisha signal zao
Sema muziki unaokua unatoka hapa mzee kama upo eneo la tukio walahi una konga nyoyo kinoma lazima utoke umeenjoy sana hasa kama DJ atakua anajua nini maana ya burudani na kuzitendea haki hiyo sound...
 
Smart Guy Mapank Mamaya Extrovert
Niaje mazee!?
Hivi ushawazaga kwenye concert kubwa kubwa zile mpangilio wa sound hua niaje?
Hebu check mfano sound hiyo apo kwenye stage
Kwenye matamasha kama haya
Unakuta kuna amplifier 40-50-60😁
Then kuna speaker kama 80😄
Sound inayotoka hapo mzee ni balaa!
Ushajiuliza waya za signal hua ngapi! Si zitakua uchafu!
Vipi kama ikiungua au kupata hitilafu moja ikiwa show inaendelea?
Stay nkupe mchongo!

Ukisikia sound engineer kwa wenzetu huko ujue kweli wanapiga kazi!
Kuongoza vyombo vyote hivi ,inahitajika akili na utimamu
Japo wenzetu ki teknolojia wako mbali

Kwanza kabisa wenzetu kwa sasa hawatumii tena haya ma amp ya CAT
Sio mbaya bali hazipo ki teknolojia
Wanatumia amp kama D10Q!
Unajua kwanini kwasababu zinauwezo wa kupokea ethernet
So mfano una amplifiers zako 50 zote engineer anaweza kuzi control kwa kupitia computer yake!
Anaweza kuizima au kuiwasha.. kusoma joto la amplifiers na kuangalia kama inafanya kazi kwenye normal condition

Kwa mfano show inaendelea bahati mbaya amplifiers moja ikazingua
Bado kuna kua na amp kama 5,6-10 ambazo zinakua connected but standby
Kwa maana ya kua ndani ya nusu sekunde inawezakana kuzima amp hi na ikaongia hi!
Yaana ile dj anasema mama aminaaaa😂
We unajibu huku nyuma wamezima amp zote wamewasha zingine ndan ya sekunde 😅!!!!

Lakini pia hawatumii cable zs kawaida kusafilisha signal bali hutumia ethernet kusafilisha signal zao
Hizi sound huwa CCM anajaribu kutuletea kwenye miji mikubwa kama Dar, Mwz, Arusha, Mbeya ni balaa sana
 
Wakuu habari zenu,
kuna swali nataka kuuliza wenda lishajibiwa huko nyuma ila kwakuwa mm ndo naingia leo kwa uzi huu itakua poa mkinifahamisha..

Naomba kujua ipi tofaut kati ya sound bar na home theater ..

na pia ipi ina ubora kuzid mwenzake kati ya hzo..kwa mfano sony sound bar ya watt 1000 na sony hometheater ya watt 1000
 
Zamani zilikuwa na mtazamo huu kwamba Home theater zinamziki Mkubwa kuliko sound bars, ila nimekuja kugundua unalinganisha brands zipi. Sound bars zinapiga nyie, na zinakupa kile na zaidi ya unachopata kutoka kwenye HT,.muhimu bajeti yako..

Nimelipa Mzigo wa 680,000/- ila hupo out of stock, nikapewa haka kadubwana ni nitumie, ke nyewe kanapatikana kwa 460,000/- tu ni balaa, Vizio m215a-j6.. channel 2.1
6115hwFM-0L._AC_SL1500_.jpg

Then kuna hii m51ax-j6, inakupa 5.1 channel, kwa uzoefu nilioupata kwenye hiyo 2.1 channel, kinapiga chini HT nyingi tu, ikiwepo za Sony za Watts 1,000. Hii 5.1 itakuwa balaa mara mbili.

Uzuri wauzaji wa hizi product kama Mfuko mdogo wanaruhusu top up, ku upgrade, Malengo yangu nikuja kufika kwenye Elevate Series, hiyo inakupa 5.1.4 channel, kuhusu deep bass naweza kusema Vizio ni Mkali kuliko JBL. Hii debate hata Chat GPT anaimaliza
61GxqCiu57S._AC_SL1500_.jpg
 
Vizio Elevate series, hizo front speaker za kwenye bar naona huwa zinarotate wakati wa kumwaga moto nadhani ndio maana toleo likaitwa elevate..nadhani Mfuko ukikaa vizuri lazima nichukue Elevate 5.1.4 channel.

Kuhusu deep bass hapa hakuna mjadala, zinapiga ni balaa...setting display tunazipata kwenye remote
61wVynQ+qNL._AC_SL1500_.jpg
81h02GPQ4FL._AC_SL1500_.jpg
41jQdi220RL._AC_SL1500_.jpg
 
Zamani zilikuwa na mtazamo huu kwamba Home theater zinamziki Mkubwa kuliko sound bars, ila nimekuja kugundua unalinganisha brands zipi. Sound bars zinapiga nyie, na zinakupa kile na zaidi ya unachopata kutoka kwenye HT,.muhimu bajeti yako..

Nimelipa Mzigo wa 680,000/- ila hupo out of stock, nikapewa haka kadubwana ni nitumie, ke nyewe kanapatikana kwa 460,000/- tu ni balaa, Vizio m215a-j6.. channel 2.1
View attachment 3329804
Then kuna hii m51ax-j6, inakupa 5.1 channel, kwa uzoefu nilioupata kwenye hiyo 2.1 channel, kinapiga chini HT nyingi tu, ikiwepo za Sony za Watts 1,000. Hii 5.1 itakuwa balaa mara mbili.

Uzuri wauzaji wa hizi product kama Mfuko mdogo wanaruhusu top up, ku upgrade, Malengo yangu nikuja kufika kwenye Elevate Series, hiyo inakupa 5.1.4 channel, kuhusu deep bass naweza kusema Vizio ni Mkali kuliko JBL. Hii debate hata Chat GPT anaimalizaView attachment 3329830
Kwahyo mkuu unashaur kuwa Sound Bar ni nzur na zina mziki mkali kuliko HT ila inategemea na brand ni ipi na ina watts ngapi
 
Vizio Elevate series, hizo front speaker za kwenye bar naona huwa zinarotate wakati wa kumwaga moto nadhani ndio maana toleo likaitwa elevate..nadhani Mfuko ukikaa vizuri lazima nichukue Elevate 5.1.4 channel.

Kuhusu deep bass hapa hakuna mjadala, zinapiga ni balaa...setting display tunazipata kwenye remote
View attachment 3329841View attachment 3329842View attachment 3329846
Hizi Vizio sijazifatilia ila kwa kuwa ni brand inayouza sana marekani nafikiri zitakuwa na jambo la maana. Ipo siku ntazifatilia kwa makini.
 
Wakuu habari zenu,
kuna swali nataka kuuliza wenda lishajibiwa huko nyuma ila kwakuwa mm ndo naingia leo kwa uzi huu itakua poa mkinifahamisha..

Naomba kujua ipi tofaut kati ya sound bar na home theater ..

na pia ipi ina ubora kuzid mwenzake kati ya hzo..kwa mfano sony sound bar ya watt 1000 na sony hometheater ya watt 1000
Chukua Soundbar mkuu, hazili hata space ukiiweka ndani haina mambo mengi na inakupa unachotaka, inategemeana tu na uta purchase kampuni gani...

Kuna jamaa angu yuko Tabora alinunua Sony Home Theater hiyo watts 1000 mwezi uliopita kanipigia simu anasema imepiga tayari (imengua) na kapeleka kwa fundi imeshindikana kupona.

So akawa ananiuliza vipi kuhusu Soundbar nikamwambia njoo ghetto unitembelee nina soundbar utapata majibu mwenyewe uamue kurudi kwenye hizo home theater zako au tuungane kwenye soundbar..
 
Back
Top Bottom