Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
10,434
Reaction score
17,203
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg


Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia.
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Wewe sina shaka mkuu utakuwa unajua maana ya mziki mzuri! Maana mie nilipata experience nzuri sana hasa ya bass ambayo sikutegemea yani kama kuna subwoofer ya kichina inaweza kuwa na mziki mzuri namna ile! Nilishasikiliza miziki mingi mikubwa subwoofers ila ule ulikuwa na extra punch

Subwoofer nyingi za mchina zina boomy bass (bass lililochanganyika na midrange) sio deep bass (bass kavu) halafu husikii ile range ya woofer bass notes ambayo unaipata kwenye zile hi-fi systems!
Seapiano 993 je ikoje Mkuu ? Ni nzuri ?
 
Zina kita deep bass mkuu, balaa zito. Box la woofer ni dogo, Ila roof inatikiswa. Unaweza kuwatembelea dukani kwao wapo jirani na MIC Hotel hapo Ubungo, ruhusa kutest mtambo. Kuna matoleo mengi. V series, M Series na Elevate. Hizi elevate ndio za million + japo ni mtumba...
 
Smart Guy Mapank Mamaya Extrovert
Niaje mazee!?
Hivi ushawazaga kwenye concert kubwa kubwa zile mpangilio wa sound hua niaje?
Hebu check mfano sound hiyo apo kwenye stage
Kwenye matamasha kama haya
Unakuta kuna amplifier 40-50-60😁
Then kuna speaker kama 80😄
Sound inayotoka hapo mzee ni balaa!
Ushajiuliza waya za signal hua ngapi! Si zitakua uchafu!
Vipi kama ikiungua au kupata hitilafu moja ikiwa show inaendelea?
Stay nkupe mchongo!

Ukisikia sound engineer kwa wenzetu huko ujue kweli wanapiga kazi!
Kuongoza vyombo vyote hivi ,inahitajika akili na utimamu
Japo wenzetu ki teknolojia wako mbali

Kwanza kabisa wenzetu kwa sasa hawatumii tena haya ma amp ya CAT
Sio mbaya bali hazipo ki teknolojia
Wanatumia amp kama D10Q!
Unajua kwanini kwasababu zinauwezo wa kupokea ethernet
So mfano una amplifiers zako 50 zote engineer anaweza kuzi control kwa kupitia computer yake!
Anaweza kuizima au kuiwasha.. kusoma joto la amplifiers na kuangalia kama inafanya kazi kwenye normal condition

Kwa mfano show inaendelea bahati mbaya amplifiers moja ikazingua
Bado kuna kua na amp kama 5,6-10 ambazo zinakua connected but standby
Kwa maana ya kua ndani ya nusu sekunde inawezakana kuzima amp hi na ikaongia hi!
Yaana ile dj anasema mama aminaaaa😂
We unajibu huku nyuma wamezima amp zote wamewasha zingine ndan ya sekunde 😅!!!!

Lakini pia hawatumii cable zs kawaida kusafilisha signal bali hutumia ethernet kusafilisha signal zao
 

Attachments

  • IMG_3036.jpeg
    IMG_3036.jpeg
    441.2 KB · Views: 13
  • IMG_3035.jpeg
    IMG_3035.jpeg
    871.5 KB · Views: 21
Smart Guy Mapank Mamaya Extrovert
Niaje mazee!?
Hivi ushawazaga kwenye concert kubwa kubwa zile mpangilio wa sound hua niaje?
Hebu check mfano sound hiyo apo kwenye stage
Kwenye matamasha kama haya
Unakuta kuna amplifier 40-50-60😁
Then kuna speaker kama 80😄
Sound inayotoka hapo mzee ni balaa!
Ushajiuliza waya za signal hua ngapi! Si zitakua uchafu!
Vipi kama ikiungua au kupata hitilafu moja ikiwa show inaendelea?
Stay nkupe mchongo!

Ukisikia sound engineer kwa wenzetu huko ujue kweli wanapiga kazi!
Kuongoza vyombo vyote hivi ,inahitajika akili na utimamu
Japo wenzetu ki teknolojia wako mbali

Kwanza kabisa wenzetu kwa sasa hawatumii tena haya ma amp ya CAT
Sio mbaya bali hazipo ki teknolojia
Wanatumia amp kama D10Q!
Unajua kwanini kwasababu zinauwezo wa kupokea ethernet
So mfano una amplifiers zako 50 zote engineer anaweza kuzi control kwa kupitia computer yake!
Anaweza kuizima au kuiwasha.. kusoma joto la amplifiers na kuangalia kama inafanya kazi kwenye normal condition

Kwa mfano show inaendelea bahati mbaya amplifiers moja ikazingua
Bado kuna kua na amp kama 5,6-10 ambazo zinakua connected but standby
Kwa maana ya kua ndani ya nusu sekunde inawezakana kuzima amp hi na ikaongia hi!
Yaana ile dj anasema mama aminaaaa😂
We unajibu huku nyuma wamezima amp zote wamewasha zingine ndan ya sekunde 😅!!!!

Lakini pia hawatumii cable zs kawaida kusafilisha signal bali hutumia ethernet kusafilisha signal zao
 

Attachments

  • IMG_3037.jpeg
    IMG_3037.jpeg
    566.5 KB · Views: 18
Nahitaji radio yenye muonekano mzuri, ndogo na mziki mkubwa speaker au twita ziwe mbili na muonekano mzuri, Cha msing muonekano na sound nzuri isiwe kubwaa
Kamq fundi
Nadhani hi kwangu imekua changamoto
Napata dm nyingi za watu wakitaka kuambiwa subwoofer gani nzuri”
Ki msingi hua inaniwia vigumu tokana na either kua juu ya matakwa au chini au nje kabisaa
Thus why hua naona heri nkasema nenda dukani kaaombe wakusikilizishe
Then ukiipenda ichukue….
 
Kamq fundi
Nadhani hi kwangu imekua changamoto
Napata dm nyingi za watu wakitaka kuambiwa subwoofer gani nzuri”
Ki msingi hua inaniwia vigumu tokana na either kua juu ya matakwa au chini au nje kabisaa
Thus why hua naona heri nkasema nenda dukani kaaombe wakusikilizishe
Then ukiipenda ichukue….
Unaweza ukaniambie ya Bei chini ya Lak 2 ambayo ni nzur
 
Moja kati ya multimedia system iliyokua pendwa kitaa ni hi!
Kuna wengine till now wanatumia
Naam ni sp 1002 na
Sp 7700
Nalaa
Sp 1002 mzigo ulipewa tf ya 18,0,18VAC
ikachapwa TDA 2050 zake 4
Mbili zinapiga bridge (bass) mbili ni stereo ya tweeter!
8ohm inch 8 speaker zinatupa dundo makini
Zilikosa Bluetooth tu!
Ila baadae wakaziboresha kidogo kwa kuzipa Bluetooth na zikawa noma zaidi

Punde si punde likatokea la kutokea😂😂
 

Attachments

  • IMG_3040.jpeg
    IMG_3040.jpeg
    229.1 KB · Views: 18
  • IMG_3039.jpeg
    IMG_3039.jpeg
    252.2 KB · Views: 17
  • IMG_3038.jpeg
    IMG_3038.jpeg
    265.6 KB · Views: 13
Back
Top Bottom