Nitawashangaa sana chama tawala mkimpitisha huyu wa sasa hiyo 2025. Viatu vimempwaya mno!

Mzalendo Uchwara

JF-Expert Member
Jan 26, 2020
3,721
11,714
Tuwe wakweli, huyu mheshimiwa mama naniliu hajawahi kuchaguliwa na chama wala wananchi kushika nafasi ya rais wa nchi. Yupo pale kumalizia kipindi cha hayati na kuivusha nchi kwa mujibu wa katiba. Na tumshukuru kwa kazi hiyo.

Lakini kwa uwezo wake wa uongozi aliounesha katika kipindi hiki cha kumalizia ungwe ya hayati ni wazi kuwa viatu vya urais ni vikubwa mno kwakwe.

Taifa haliwezi kuwa na rais ambaye anaamini kutoka moyoni mwake kuwa sisi hatuwezi kitu na maendeleo yetu yatapatikana kwa kuwaomba na kuwalamba miguu mabeberu. Kutwa kucha kiguu na njia kuzurura huko kwa hao anaodhani wanatoa free lunch.

Taifa haliwezi kuchaguliwa rais na wakala wa CIA ambaye wapumbavu wanamwita 'king maker', na ambaye mheshimiwa anamwona ndio turufu yake ya kuendelea kubaki ikulu na ameamua kumweka karibu na anaambatana nae huku na kule.

Taifa haliwezi kuwa linahangaika na matatizo yaleyale yaliyomalizwa na mtangulizi, mambo kama migao ya umeme, uhaba wa maji, uhaba wa sukari, uhaba wa fedha za kigeni, mfumuko wa bei, rushwa na ubadhirifu serikali N.K ni aibu kwa taifa na kiongozi wake.

Wazalendo ndani ya chama walifanya uzalendo wa kutukuka ile 2015 kulilinda taifa, i expect nothing less hiyo 2025. Upigwe mchujo kamili apatikane mtu sahihi.

Nilikuwa na matumaini sana na huyu mheshimiwa, lakini ukweli tuuseme tu, ngazi ya taifa sio sehemu ya kufanya experiment za uongozi.
 
Kwa Kauli Ya W/Mkuu Na Mheshimiwa Kinana Wakiwa Wilayani Ruangwa
Walisema Form Ni Moja Tu Kwa Nafasi Ya Rais Na Anatakiwa Eti Amalizie
Miaka Yake Iliyobaki


Ndugu Zangu Mwafaa!!!
Huyu akiendelea mpaka 2030 basi kila mtu atakuwa na kisima cha maji nyumbani na jenereta lake la kujizalishia umeme. Bidhaa kama mafuta ya petroli na sukari tutakuwa tunanunua kwa magendo huko vichochoroni.
 
Mkuu Mzalendo Uchwara una hoja imara na muhimu sana kwa taifa hili.

Ila kwa Bahati mbaya uwepo wa mkizimkazi kwenye hiyo ofisi kubwa kumekuwa ni neema kwa wenye biashara kubwa(haramu na halali) ambao wana turufu ya maamuzi kwenye chaguzi zetu.
Kwa mantiki hiyo, hili tatizo bado tutaendelea kuwa nalo kwa miaka mingine mitano.
Kumbuka, ndani ya chama cha mambuzi wenye pesa ndio wenye maamuzi.
 
Back
Top Bottom