Mtikisiko wa kutisha unaendelea Chama cha Walimu Tanzania

HaMachiach

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
3,399
6,077
Kama tulivyowahabarisha hapo awali juma hili hili kwenye jukwaa hili hili, Chama Cha Walimu Tanzania kimeendelea kupigwa vita na waliokuwa viongozi wa awali huku wakiendelea kupata msaada mkubwa kutoka kwa baadhi ya viongozi waandamizi wa Serikali ambao kwa sasa wamekwishaungana kwa ajili ya jambo hilo.

Ili kukamilisha jambo hilo wameanza na Japhet Maganga ambaye ndiye mtendaji mkuu wa chama na katika kipindi cha muda mfupi amezuia upigaji wa fedha za chama ambao uongozi wa awali umefanya kwa kiwango cha kutisha na baadhi ya wafaidika ni viongozi waandamizi Serikalini wenye uhakika wa kwamba kama Maganga hatakuwepo 2025 na watakapokuwa wamefanikiwa kuweka mtu/watu wao watapata msaada mkubwa wa kifedha kuwasaidia kwenye uchaguzi mkuu wa 2025. Kwa muda mfupi Maganga amefanikiwa kufanya yafuatayo.
  1. Kwa kushirikiana na viongozi amefanikiwa kuleta utulivu na uthabiti ndani ya Chama cha Walimu
  2. Ameweza kupunguza kwa kiwango kikubwa malalamiko ya walimu dhidi ya uongozi wa chama hususani yanayohusu ubadhirifu, uwajibikaji na huduma kwa wanachama. Mwezi Agosti 2023 kwa mfano, alifanya kikao cha siku mbili kwa watendaji wote wa ngazi za wilaya na mikoa akawapa maelekezo na mikakati ya namna bora ya kuwahudumia wanachama vikiwemo; Kwa siku tano za kazi za juma siku tatu ni lazima makatibu waende kwenye sehemu za kazi kusikiliza na kutatua kero za walimu, Asilimia 15 ya michango ya walimu inayorudishwa sehemu za kazi ipelekwe kila mwezi kwenye sehemu za kazi; Vikao kwenye kamati mbalimbali vifanyike kwa mujibu wa katiba ya CWT; watendaji wapeleke kwa katibu mkuu taarifa ya kazi ikijumlisha pamoja na yaliyoainishwa hapo juu kila baada ya miezi mitatu. Walikubaliana pia hatua za kinidhamu zitakazochukuliwa dhidi ya mtendaji ambaye hatatekeleza muongozo huo. Haya ni machache kati ya tuliyofanikiwa kuyapata kutokana na kikao kazi hicho.
  3. Kuzuia matumizi mabaya ya fedha na rasilimali za chama. Ikumbukwe kwamba michango hii inatoka kwenye asilimia 2 ya mishahara kiduchu ya walimu kama ilivyoainishwa kwenye katiba ya chama chao. Kitendo cha Maganga kuzuia upigaji kiasi cha kupelekea mapambano na uongozi uliopita ukiungwa mkono na baadhi ya wanasiasa wanufaika inatukumbusha maneno ya Nicollo Machiavelli aliyoyaandika kwenye kitabu chake cha The Prince, nayanukuu kwa kiingereza “It should be borne in mind that there is nothing more difficult to arrange, more doubtful of success, and more dangerous to carry through than initiating changes. The innovator makes enemies of all those who prospered under the old order”, akimaanisha "Ni vyema kufahamu kwamba hakuna jambo lenye ugumu zaidi wa kuandaa, lenye shaka zaidi kwa mafanikio, na lenye hatari zaidi kutekeleza kuliko kuanzisha mabadiliko. Mwenye kuleta mabadiliko huwa na maadui miongoni mwa wale waliokuwa wafaidika wa mfumo wa awali. Ushahidi wa vita hii ni ufuatao;

1. Raisi wa Chama, Katibu Mkuu na Mwekahazina kwa mujibu wa katiba ya CWT walliitisha kikao cha kamati ya utendaji ya taifa na kabla ya kuanza kikao saa 2 asubuhi kwenye ukumbi wa St. Gasper jijini Dodoma, Katibu Mkuu Maganga alipokea barua kutoka kwa msajili imeambatanishwa ikizuia kufanyika kwa kikao hicho kwa sababu eti muda wa Katibu Mkuu kuwa ofisini umeisha kwa tarehe ya barua hiyo. Ikumbukwe kuwa barua hiyo ni ya tarehe 23 Septemba ambayo ndio siku ya kikao ina maana msajili alishinikizwa kutoka juu. Tarehe 23 hiyo hiyo Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke alimuandikia barua Japhet Maganga kumuarifu kuwa kibali chake kinaisha tarehe 30 Septemba na anapaswa kuripoti kazini tarehe 1 Mwezi Oktoba. Hapa inabidi kuangalia yafuatayo (a). Msajili anasema kibali cha Maganga kimekwisha, Mkurugenzi anasema kupitia barua yake kuwa kibali kinaisha tarehe 30 Septemba, mgongano wa taarifa hii unasababishwa na nini? Ni ushahidi kwamba wote wamefanya kazi kwa shinikizo tena siku isiyo ya kazi. Kikao cha kamati ya utendaji kimeitishwa na uongozi wa juu lakini anayetajwa hapa ni Maganga tu, kwa nini? (b)wajumbe hao wametumia gharama kwenda kwenye kikao, hii ni hasara kwa chama (c) mawasiliano kati ya mtumishi na mwajiri ni binafsi, lakini barua ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke kwa Maganga tarehe hiyohiyo imewekwa kwenye tovuti na mitandao ya kijamii rasmi ya Ofisi ya Rais Tamisemi jambo linaloendelea kuwashangaza wengi wakiibuka na maswali lukuki kwa mfano; kwa nini itolewe taarifa kwa umma ikionesha mpaka check no. ya Maganga. Kwa kila mpenda haki atagundua kuwa huu ni uonevu na udhalilishaji. Swali jingine Je huu ndio utaratibu wa mawasiliano kati ya mtumishi na mwajiri wake? Je Maganga ametenda dhambi gani hadi alengwe kutendewa haya? Kama umekuwa ukifuatilia maandiko yetu kwenye jukwaa hili hili, tulieleza sababu za Maganga kupigwa vita, sababu kubwa ikiwa ni chama kusimama imara kwenye kuwatetea walimu na kuzuia upigaji.

Ukipitia maoni kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii baada ya taarifa hiyo kuanza kusambaa, Maganga kurejeshwa kwa muajiri kumetafsiriwa kama Kisasi kutokana na Mwalimu Maganga pamoja na mwenzake Mwalimu Leah Ulaya kutokuhudhuria kwenye kuapishwa kwa nafasi za Ukuu wa Wilaya walizoteuliwa na mamlaka. Tunaamini kuwa wahusika kutoripoti kwenye nafasi zao kunaweza kuwa na sababu mbili. Mosi au hawakujulishwa hapo awali kabla ya kutangazwa hadharani kama ulivyo utaratibu ama bila Mheshimiwa Rais kutofahamishwa kwa kina, uteuzi huu ulikuwa wa kimkakati ili kuwapisha wapigaji kwa kuwa uteuzi ulimhusisha rais wa chama, makamu wa rais wa chama na katibu mkuu ambao hao wote kasoro makamu wa rais walikuwa na mwezi mmoja tu tangu waidhinishwe na mkutano mkuu wa walimu ambao ndio wenye mamlaka hiyo kwa mujibu wa katiba ya CWT. Maana yake CWT ingebaki bila uongozi wa kitaifa. Wapo walioamini kuwa uteuzi huo ulikuwa ni “mwarobaini” kutatua migogoro ndani ya CWT, huku kundi kubwa la walimu wenyewe wakiamini ni juhudi za uongozi dhalimu uliopita wa Deus Seif na baadhi ya wanasiasa waandamizi kutaka ama kurudi madarakani ama kuweka watu wao. Kuingia kwa hila kwa Joseph Misalaba kama tulivyokwisha eleza hapo awali kama Naibu Katibu Mkuu ilikuwa ni moja ya mafanikio yao. Kwa taarifa, Joseph Misalaba ana undugu wa damu na moja ya wanasiasa na kiongozi wa serikali wa ngazi ya juu ambaye pia Deus Seif akiwa Afisa elimu msingi wilaya ya Geita yeye alikuwa ni Afisa Elimu taaluma.

Kurejeshwa kwa Maganga kwa mwajiri wake sio kwa sababu ya kukataa uteuzi, bali ni kwa sababu ya kiu yake ya kutaka mabadiliko na maendeleo ya walimu kupitia chama cha walimu. Ni vema ikafahamika kwamba barua ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke ni ujumbe kwa walimu wote nchini kwamba, yeyote atakayejitokeza kutaka kupigania mabadiliko hasa ya kuwanufaisha walimu na kuwakwamisha wapigaji ni lazima akumbane na rungu la wapigaji hao kupitia waajiri wao. Yani ukileta fyoko fyoko unahamishwa au unashushwa madaraka, au unatengenezewa zengwe kwa mfano ulikuwa masomoni bila kibali hivyo ni utoro kazini ajira inapotea. Hili ni walimu tu wanaoweza kulielewa.

Kikao cha kamati ya utendaji ya taifa CWTcha jana tarehe 23 kilisambaratishwa na polisi jijini Dodoma, kesho tarehe 25 Septemba 2023 kuna kikao cha baraza la taifa CWT kitakachofanyika St. Gaspar jijini Dodoma, mambo mawili kwa uhakika yatatokea, moja polisi watasambaratisha kikao hicho kwa sababu tayari order wanayo; wanachoogopa ni kwamba, kwenye kikao hicho cha Baraza la Taifa ni kwamba Wajumbe wa Baraza la Taifa wataelezwa ukweli wote kuhusu hujuma zinazofanywa kwa chama na mipango mkakati ya chama ambayo itazidi kuumbua uongozi uliopita; mbili msajili ataleta barua nyingine ya kumzuia Maganga kuitisha kikao hicho japo yeye anamuona Maganga hauoni Uongozi. Polisi kuvamia vamia vikao vya vyama vya wafanyakazi ni kuukiuka uhuru wa vyama vya wafanya kazi kwani vikao hivi havina wala havijawahi kuwa na uvunjifu wa amani na kumzuia Maganga kushiriki ni kumnyima haki yake kwa mujibu wa sheria ya ajira na mahusiano kazini ibara ya 9(5) ya mwaka 2004. Sarakasi hizi pia ni ukiukwaji wa azimio la shirika la Wafanyakazi duniani ILO ambalo Tanzania imeridhia.

Ushauri wetu kwa Maganga, uzalendo wako ndio unaoendelea kukuponza na umepambana na uongozi wa Deus ambao umekuwa ukiwanufaisha wanasiasa na baadhi ya viongozi walafi serikalini. Usifiki genge hilo umemamalizana nalo, maana hata ukirudi kwa mkurugenzi Temeke hutabaki salama. Endelea kuwapambania walimu na Mungu yuko upande wako na walimu wapo upande wako

Ushauri kwa walimu; simameni imara muendelee kupiga kelele kwa sana kona zote za nchi kwa maslahi yenu na kwa mustakabali wa chama chenu mnachokijua kwa muda mrefu, mnazifahamu ofisi zake kila mkoa na kila wilaya, kuliko kughilibiwa na wanaowaonesheni kwamba eti wao ni nafuu, ukiuliza wako wapi wala huwezi kujua, Kama mnaona kwamba michango ya asilimia 2 ni kubwa japo ipo kwenye vyama vyote halali vya wafanyakazi nchini toeni maoni yenu kwenye mabadiliko ya katiba ya CWT. Huwezi kuleta mabadiliko kwa kuanzisha kitu kipya, badilisha kile ulicho nacho kwani kipo ndani ya uwezo wako. Tunapenda kuwaasa walimu pia, kukumbuka maneno ya mwanaharakati Malcom X aliyewahi kusema kama hutokuwa muangalifu utafanywa uwachukie watu unaopaswa kuwapenda, huku ukiwapenda unaopaswa kuwachukia.

Ushauri wetu kwa serikali, Kwa muda mrefu tumekuwa tukiandika maandiko kuonesha kinachotokea kwenye chama cha walimu kiini chake na kwa bahati mengi ya tunayoyabainisha yanatokea hii ni dhahiri kwamba wanaoyafanya hawaogopi nguvu ya walimu au ni kesi ya ngedere unamshtakia nyani. Ni wakati sahihi kwa viongozi na mamlaka adilifu serikalini kulichukulia hatua hili kwa kuwathamini walimu na kuyafanyia kazi malalamiko yao ya muda mrefu. Chama cha walimu kilindwe kisidhoofike kwani kudhoofika kwake kuna athari hasi kwa jamii. Tusubiri tuone yatakayotokea kesho.
 
Kuna mtu aliandika humu kwamba ukitoka UWT next level ni CWT
 
Ni muda sasa wa kutoa wito kwa wanasheria nguli na waadilifu kama kina Mh Kibatara, Mh Mwambukuzi na wengine kuingilia kati kuhusu hujuma hii kwa CWT. Wanasiasa wana maslahi yao kuelekea 2024 na 2025 katika hujuma hiyo.
 
Team Maganga at large! Ujumbe Unafika walimu wanajua watakachokifanya 2024/2025
 
Huu ni mwanzo mzuri wa ukombozi kwa nchi yetu. Baada ya kifo cha CWT, naomba na ccm nayo ijiandae. Maana na wenyewe siku zao za kuwandamiza na kuwaibia Watanzania, zinahesabika.
 
Walimu wengi hawakipendi na hawakitaki chama hiki. Nikiwa kama katibu wa tawi nilifanya umafia kuwasainisha walimu wakatwe asilimia mbili ya mishahara yao. Matokeo yake niliandaliwa mapinduzi nipinduliwe kwa kitendo kuwasainisha bila wao kupenda kukatwa hiyo asilimia mbili. Wanadai chama hicho ni chama cha kipigaji tu na hakina msaada kwao hawakitaki
 
Bwana Maganga anarudi kwenye ualimu.
 
Hivi ile benki ya waalimu MCB bado inafanya kazi ilifutwa?
 
Walimu wengi hawakipendi na hawakitaki chama hiki. Nikiwa kama katibu wa tawi nilifanya umafia kuwasainisha walimu wakatwe asilimia mbili ya mishahara yao. Matokeo yake niliandaliwa mapinduzi nipinduliwe kwa kitendo kuwasainisha bila wao kupenda kukatwa hiyo asilimia mbili. Wanadai chama hicho ni chama cha kipigaji tu na hakina msaada kwao hawakitaki
Tena una bahati,Kuna watu wlishaandaa mapanga aisee.Usirudie Tena ule ujinga.
 
nilitengwa na staff nzima nikawa nashindia kwenye vipindi vyangu madarasani. Walijuta kunichagua kwa asilimia mia moja niwe muwakilishi wao huko chamani. Nilijifunza mengi huko chamani ikiwemo kuwaburuza walimu kwa mambo ambayo hawayataki kwa kutumia ubabe na umafia kufanikisha agenda za chama. Kuna walimu wana misimamo mikali kuhusu chama hawakitaki kabisa. Wakati wa uchaguzi wale wote ambao wako kinyume na chama hawapati nafasi majina yao kusonga mbele na kupigiwa kura. Ndio hao wanaotaka chama mbadala
 
Huyo Maganga na timu yake na hicho chama wote ni wauaji, alitakiwa akanyongwe huko asiletee walimu wetu maradhi mabaya ya tamaa huko shule...
 
Halafu walimu wanaendelea kukatwa kila mwezi huku watu wanagombania hela zao
 
Back
Top Bottom