Nitatoa zawadi ya 200,000

Kaniumiza parefu sana aiseeeee.....
Hata hivyo ww umefanya makosa ama kwa uzembe, kutojua au kwa bahati mbaya. Hukutakiwa kumpigia yeye, bali ulitakiwa kuwapigia customer care ya mtandao uliotumia kutuma pesa wangeblock na wangekurudishia hiyo hela. Usirudie kufanya makosa ya namna hiyo
 
Daah kwenye pesa siaminigi mtu kabsa mkuu.. Ungepga mtandao husika baada ya kubaini ili wazuie...ila ndo ishatokea...pole mkuu
 
Nadhani neno sahihi ni tapeli, sio mwizi.
 
Inaelekea ni muumini wa kkkt kimara, nenda kanisani ukafanye upelelezi utampata
 
Hayajakukuta. Kuna siku Italia kilio cha mbwa meno hayaumani.
Yashanikuta,bahati nzuri haikuwa pesa kubwa nikapotezea baada ya niliyemtumia kuingia mitini!
Kuna siku nikiwa chuo,nilikuwa nimepigika kinoma na rafiki yangu!Hatukuwa na hata mia ya kula mchana!Ilikuwa jmos,basi tukawa tumelala tu hostel kila mtu akihangaika na simu kucheki ndugu wa kututoa kwenye majanga!Mimi nilikuwa nimepiga mzinga watu kama watatu hivi!Nikawa nasubiri,ghafla 100,000/= ikaingia!Kilichofuata nikamshtua jamaa twende tukale mzigo umeingia!Kwa njaa niliyokuwa nayo hata sikuangalia nani katuma,nikaenda kutoa 30,000 tukaenda kula!Tukiwa katikati ya msosi,nikapigiwa simu na mama mmoja akaniambia amekosea kutuma hela!Daah nilisinyaa!Ikabidi nimueleze hali halisi bila kuficha!Nikamuomba nimrudishie 70,000 ikiyokuwepo kwny simu then nikipata nitamtumia kiasi kilichobaki!Huyo mama hakuamini,akasema mwanangu basi tu usitume hata hiyo 70,000!Itakusaidia na usome kwa bidii!Mpaka leo huyo mama tunawasiliana na kujuliana hali!
Ukikosea kutuma pesa basi fanya kama umepoteza tu,usiihesabie kabisa!Halafu mtu huwezi muanika kisa ameingia mitini na hela uliyomtumia kimakosa!
 
Jumapili nenda hapo kkkt kimara utamuona anasimama hapo alipopigia picha, akitaka kupiga nyingine au umwambie mchungaji atangaza hapo kanisani!
Lakini isije ikatokea ukamwaga machozi hapo kanisani maana ndipo hapo Bashite alipomwaga machozi!
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Sasa nani ana kosa? Wewe au yeye?
 
Acha hadithi za uongo
 
Wewe ulifanya busara sana. Na huyo jamaa angechukua hata laki tu si mbaya. Kutokomea ndo kosa.
 
Hii kesi itakugeukia wewe... Na umejibehaave kama bashite kabisa.. Ushaidi wote unao...namba yake na eneo... Unakimbilia kuja muanika JF..

UNAWEZA UKAMPATA NDIO ....JE AKIKULIPA NA AKUGEUZIE KESI YA KUANIKA PRIVACY ZAKE UTAFANYAJE...

MAANA MPAKA SASA YE SI MWIZI...ILA WEWE CYBER CRIMINAL..

UMECHEMKA SANA BRO.
 
Mkuu Ushimen nimemcheki kijana Facebook yake naona yupo tu anatamba ila Instagram ndio kaweka Private!

Nahisi kumpata ni rahisi ila kuipata hela ndio inaweza kuwa ngumu!

Halafu dogo anafanana na Bashite nahisi wana undugu!
Umeona ushimeni alivyofanya makosa... Huyu mtu akienda mahakamani Ushimen haponi...
 
huo ni kuchafuana brand!una uhakika gani kama ndio yeye?kosa ni kako au lake?kwa nini umejipa kazi ya polisi na mahakama?kama sio yeye uko tayari kumlipa fidia?achaupuuzi
Kichefuchefu cha kutetea wezi na majambazi kila uchao kinazidi, tunakunywa maji mengi kuzuia kutapika, lakini inashindikana hadi tunatapika sasa.
Hivi nikuulize wewe mwenye dalili zote za kihalifu, hiyo sim card# ya simu yako mnaimiliki watu wangapi?
Mtu asemeje hadi umsapoti kuwa kadhulumiwa Kitapeli cha kiaminifu?
Ndiyo nyie mnaodai hata mwizi akikamatwa hatakiwi kuitwa mwizi, bali ni mtuhumiwa hadi atiwe hatiani na mahakama. Na mahakama inahukumu kosa ama tendo la wizi na haimuiti huyo aliyepatikana na hatia ya wizi kuwa ni mwizi. Itamfunga bila kumuita mwizi, akifika jela haitwi mwizi, bali anaitwa mfungwa.
Sasa mwizi huwa ni nani?
WaTz tumezoea blahblah za kishenzi sana na upotoshaji wa lugha kwa uwazi bila ya soni.
Kwa hiyo kumuita mtu mwenye tabia za ukwapuaji kuwa ni mwizi ni kumharibia brand!
Kweli jf linakada zote
 
Ten
Hawa watoto tatizo kwakua wanatuona tunashinda nao humu na kutaniana nao, wanadhani tunafanana nao.
Kama jamaa ameshindwa kua muungwana, nami sioni ajizi kumuanika aiseeeee.... Na hii itakua fundisho kwa wenye tabia kama yake
Na usiishie tu hapa jf, mpeleke mpaka facebook huko ili dunia yote imjue.maana amekosa ubinadam kabisa.
 
Nenda hapo kimara KKT alipopigia picha na hiyo status inaonesha ni muumini hapo
 
"Thank God for priceless gifts and miracles....."
Aisee anajiona kama myahudi aliyeshushiwa chakula cha bure toka angani. Shetani amemshinda kabisa.
Pole mkuu yalishawahi kunikuta kama mpokeaji na mpelekaji. Nilishawahi kuipokea kwa jamaa toka Mbeya 120,000 jamaa akalialia nikamuelekeza utaratibu wa kurudisha pesa yake ikarudi akanishukuru. Siku nyingine nilituma kwa wakala ambaye sie nae akaitoa haraka. Nikawapigia tigo akairudisha baada ya siku tatu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…