KALINZI NYUMBANI
Huyo ana uwezo wa kizaa hata watoto wawili. Siwezi kukushauri umuoe, kwani ni dhahiri humpendi kabisa ila umri umeiona kuwa ni sababu strong ya kujustify kumuacha kwa sababu angekuwa moyoni mwako, swala la umri ungeliweka pembeni na swali ambalo ungelileta hapa lingekuwa jinsi ya kuwashawishi ndugu na jamaa zako ili wampokee kama sehemu ya familia.
Usichokiona kwa sasa ni kuwa, huyo ni mwanamke anaejua maisha kwani alikwishayaanza kabla yako na akakomazwa kwa ndoa na uzazi. Hahitaji training kwani ana akili na uwezo wa kutambua na kufanya maamuzi sahihi yenye manufaa kwake na kuweka pembeni yasiyo ya msingi tofauti na mtu alie na umri mdogo au alie immature kiakili.
Kuna watu wameoa wanawake wanaojua sana label za bia, lakini hawawezi hata kununua au kuingiza units za luku. Wengine wanajua kuvaa na kutumbua sana ila mpe mtaji umwambie; "Baby, hebu izungushe hii milioni 5, usomeshe watoto wetu na kile nachopata mimi (mume) tukitumie kumalizia mjengo wetu". Ndani ya mwezi tu atakwambia biashara imemshinda kwa sababu hajazoea kupigizana kelele na wateja, kukaa sehemu moja au kuzunguka. Sasa muulize ulipo mtaji uliompa. Hapo ndipo utakapozusha ugomvi ambao hutausahau.
Kipindi ulipozinguliwa, uliapa kutafuta mtu mzima, ukampata anaefaa kabisa, ila unapokaribia kugraduate, unamuona hafai na inawezekana na tayari umeishampoint unaemwona anafaa zaidi, sasa yakijirudia wakati hizo ml 11 zimeishapukutishwa benki, uje utupe mrejesho pia.