Nitamuachaje mmama huyu anae nizidi miaka tisa?

Nitamuachaje mmama huyu anae nizidi miaka tisa?

Kama upendo hamna, usimuoe. Ukimuoa wakati humpendi mtapata shida wote wawili. Ila kama unampenda na tatizo ni umri tu, tofauti ya miaka 10 sio mingi kiiivyo. Vijana wa sasa unaowataka watakupeleka mbio na utazeeka kumzidi huyo akupendae ndani ya muda mfupi tu!
 
Huyo ana uwezo wa kizaa hata watoto wawili. Siwezi kukushauri umuoe, kwani ni dhahiri humpendi kabisa ila umri umeiona kuwa ni sababu strong ya kujustify kumuacha kwa sababu angekuwa moyoni mwako, swala la umri ungeliweka pembeni na swali ambalo ungelileta hapa lingekuwa jinsi ya kuwashawishi ndugu na jamaa zako ili wampokee kama sehemu ya familia.

Usichokiona kwa sasa ni kuwa, huyo ni mwanamke anaejua maisha kwani alikwishayaanza kabla yako na akakomazwa kwa ndoa na uzazi. Hahitaji training kwani ana akili na uwezo wa kutambua na kufanya maamuzi sahihi yenye manufaa kwake na kuweka pembeni yasiyo ya msingi tofauti na mtu alie na umri mdogo au alie immature kiakili. Kuna watu wameoa wanawake wanaojua sana label za bia, lakini hawawezi hata kununua au kuingiza units za luku. Wengine wanajua kuvaa na kutumbua sana ila mpe mtaji umwambie;

"Baby, hebu izungushe hii milioni 5, usomeshe watoto wetu na kile nachopata mimi (mume) tukitumie kumalizia mjengo wetu". Ndani ya mwezi tu atakwambia biashara imemshinda kwa sababu hajazoea kupigizana kelele na wateja, kukaa sehemu moja au kuzunguka. Sasa muulize ulipo mtaji uliompa. Hapo ndipo utakapozusha ugomvi ambao hutausahau.

Kipindi ulipozinguliwa, uliapa kutafuta mtu mzima, ukampata anaefaa kabisa, ila unapokaribia kugraduate, unamuona hafai na inawezekana na tayari umeishampoint unaemwona anafaa zaidi, sasa yakijirudia wakati hizo ml 11 zimeishapukutishwa benki, uje utupe mrejesho pia.

Thanks Boss nimeipenda sana mtazamo wako, naamini ukiwa na mtazamo kama huo ndoa haiwezi kukushinda kabisa kwa kuwa utamtafuta mnayeweza jenga naye maisha na sio wa maonesho kwenye kumbi mbalimbali za masherehe,

Umri si kikwazo ktk maisha ya ndoa otherwise uwe na mawazo ya kumtafuta mateka wa ndoa ambaye utataka uwe una mpa order za kijeshi na kuhoji baada ya utekelezaji au hakuna kabisa.

We need an assistant.. Ambaye mtashauriana kujenga maisha zaidi ikiwemo kuwa na pato la pamoja kwa kuchanga mishahara na kuweka wazi vipaumbele vyenu vya maisha au kwa kuanzisha biashara mbadala yenye matawi na wasimamizi wawili wenye malengo ya pamoja.

I appreciate that.
 
Hahaha! Dah! Hiyo kiboko aisee! Kwa hiyo alikuwa anataka muwe mnatumbua tu bila kupanga maendeleo? Inachekesha sana!

yaan nlikimbia kama nmevamia uchochoro wa vibaka halafu yuko serious., wew mwanamke sio aisee juzi tu ulikuwa unaongea na fundi wa ujenzi sijui ushajenga, leo tena unaleta habar hzi. hadi leo sitomsahau yule kijana na masters yake. uck mwema best
 
Kama upendo hamna, usimuoe. Ukimuoa wakati humpendi mtapata shida wote wawili. Ila kama unampenda na tatizo ni umri tu, tofauti ya miaka 10 sio mingi kiiivyo. Vijana wa sasa unaowataka watakupeleka mbio na utazeeka kumzidi huyo akupendae ndani ya muda mfupi tu!
Mkuu kumpenda nampenda lakini umri ndio unasababisha nisimpende,But kiukweli ananisikiliza sana mpaka kumfanyia ujinga ili tuachana najishtukia sana.Maana ananisikiliza kinoma na akikosa ni mwepesi kukili kosa na kuomba msamaha.
 
Kosa kubwa tunalifanyaga wanaume ni kutoa ahadi za uongo uongo ambazo tunajua kabisa kwenye akili zetu hatuwezi kuzitimiza....
Nina hakika kwa 99% ulishawahi kumwambia huyo mwanamama kuwa utamwoa jambo ambalo ulidhani unalisema kwa wakt huo ili kutimiza adhma yako fulani na hukuwa na maana ya dhati ndo maana hutaki kumuoa... Ushauri wangu mweleze tu ukweli.. Itamuuma ila I hope hatakuwa na jinsi
 
Sasa kwanini umuache mwanamke kama huyu banaaa!? Mungu akupe nini tena? Dah! Unaweza kuja kumkumbuka sana huyu utakapokuwa unapelekeshwa puta na huyo mpya ukiamua kurudi kwake utakuta njemba nyingine imeshatia nanga.

Usifanye makosa hayo banaaa umri si kikwazo kihivyo cha kukufanya wewe umuache huyu mmetoka naye mbali huyu na amekusaidia sana. Unaweza kupata laana ya Mungu. Usimuache Mkuu.

Mkuu kumpenda nampenda lakini umri ndio unasababisha nisimpende,But kiukweli ananisikiliza sana mpaka kumfanyia ujinga ili tuachana najishtukia sana. Maana ananisikiliza kinoma na akikosa ni mwepesi kukili kosa na kuomba msamaha.
 
Sasa kama humpendi unamgegedaje au unamvutia hisia yule wa zamani aliyekupiga chini.
Mwanamke ni mzuri pia anavutia kinoma sema nachohofu nakupelekea nisimpende ni umri.Nawaza ntakavyo mtambulisha kwa bi mkubwa itakuwaje?.
 
Sasa kwanini umuache mwanamke kama huyu banaaa!? Mungu akupe nini tena? Dah! Unaweza kuja kumkumbuka sana huyu utakapokuwa unapelekeshwa puta na huyo mpya ukiamua kurudi kwake utakuta njemba nyingine imeshatia nanga.

Usifanye makosa hayo banaaa umri si kikwazo kihivyo cha kukufanya wewe umuache huyu mmetoka naye mbali huyu na amekusaidia sana. Unaweza kupata laana ya Mungu. Usimuache Mkuu.
Mkuu nimekuelewa zaidi ya sana but vipi bi mkubwa atalichukuliaje suala hili,Kwa sababu mama zetu huwa wanamaindi mishe hii ya kuoa mtu anae kuzidi.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Huo nao ni mtihani lakini kama Bi mkubwa nimuelewa ni kukaa naye chini na kumueleza kwanini unataka kumuoa huyu mazuri yake yote yaanike hadharani sasa ikija kwenye umri hapo ndio kasheshe bi mkubwa anaweza kugoma,

tatizo kama ile Biological clock imeshapitiliza na Bi mkubwa anataka wajukuu. Katika dunia ya leo kuwapata wanawake kama huyu ni nadra sana na ndio sababu moyo wako unasita kumuacha huyu mpaka ukaamua kuja hapa kuomba ushauri.

Mkuu nimekuelewa zaidi ya sana but vipi bi mkubwa atalichukuliaje suala hili,Kwa sababu mama zetu huwa wanamaindi mishe hii ya kuoa mtu anae kuzidi.
 
Hivi best, ndugu zako wanajuaje umri wa mwenza wako kama hujawashirikisha? Hivi mwanaume unweza peleka mchumba home na wakauliza kazaliwa mwaka gani?
Huo nao ni mtihani lakini kama Bi mkubwa nimuelewa ni kukaa naye chini na kumueleza kwanini unataka kumuoa huyu mazuri yake yote yaanike hadharani sasa ikija kwenye umri hapo ndio kasheshe bi mkubwa anaweza kugoma,

tatizo kama ile Biological clock imeshapitiliza na Bi mkubwa anataka wajukuu. Katika dunia ya leo kuwapata wanawake kama huyu ni nadra sana na ndio sababu moyo wako unasita kumuacha huyu mpaka ukaamua kuja hapa kuomba ushauri.
 
Huo nao ni mtihani lakini kama Bi mkubwa nimuelewa ni kukaa naye chini na kumueleza kwanini unataka kumuoa huyu mazuri yake yote yaanike hadharani sasa ikija kwenye umri hapo ndio kasheshe bi mkubwa anaweza kugoma,

tatizo kama ile Biological clock imeshapitiliza na Bi mkubwa anataka wajukuu. Katika dunia ya leo kuwapata wanawake kama huyu ni nadra sana na ndio sababu moyo wako unasita kumuacha huyu mpaka ukaamua kuja hapa kuomba ushauri.

Mkuu hio ndio hofu yangu maana ana miaka 33.Na mimi kumaliza chuo ni mwaka huu na kitu nachohofu zaidi huenda nikimuacha ni kaangukia kwa maumiza kichwa.Ni kabaki najutia lakini pia suala la watoto ndo nawaza kinoma maana yeye tayali ana watoto wawili mimi je?.
 
Hili ni swali zuri sana, sidhani kama wazazi au ndigu wanaweza kuuliza swali kama hili, labda itokee mmoja anamfahamu kwa karibu muhusika au muonekano wake uonyeshe umri mkubwa kuliko mume mtarajiwa.

Hivi best, ndugu zako wanajuaje umri wa mwenza wako kama hujawashirikisha? Hivi mwanaume unweza peleka mchumba home na wakauliza kazaliwa mwaka gani?
 
Kama hiyo story sio ya kutunga kama tulivyozoea kwa watu wa aina yako huku kwanza nakuambia yafuatayo:
Wewe inaonyesha unajivuna halafu hujatulia hata hiyo course sidhani kama ni kweli umesoma wewe muongo ni story tuu
Pili hakuna mwanamke utakae mpa laki 4 gafla aje azalishe milioni 11 na bado ana familia ya watoto 2 leo hii unakuja kupost story za kumuacha
Tatu ka ulikuwa humpendi utampaje hela wewe bila shaka upo darasa la saba na story za mapumziko ya saa nne wakati unasubiri uji
 
Mkuu miaka 33 wala huna sababu ya kuingia mitini. Hebu chakarika mfunge pingu za maisha Mkuu acha kurukaruka huku na kule kuhusu hii tofauti ya umri. Mwanamke mzuri, anakupenda unampenda, anakuheshimu nadhani nawe unamuheshimu.

Kama nawe unataka watoto huyu bado ana uwezo wa kukupa watoto wawili hata wanne kama mnataka kuwa na timu ya Basketball, labda kama kakwambia hataki tena watoto. Muaminifu umempa mtaji wa laki nne faida baada ya miaka kadhaa ni milioni 11. Chakarika Mkuu uweke ndani mke bora.

Mkuu hio ndio hofu yangu maana ana miaka 33.Na mimi kumaliza chuo ni mwaka huu na kitu nachohofu zaidi huenda nikimuacha ni kaangukia kwa maumiza kichwa.Ni kabaki najutia lakini pia suala la watoto ndo nawaza kinoma maana yeye tayali ana watoto wawili mimi je?.
 
mkuu yani kweli humpendi... !! Mungu akupe nini tena... Labda kupenda tu ila ishu ya umri hata ingekuwa miaka 10 si mbaya.
mtu mzima anakuheshimu, anakuelewa, anajituma kazini, faida mnapata, haleti maringo sasa ninikingine mkuu.... hiyo kitu wife material. . daa angalia usije ukaruka mkojo ukakanyaga mavi.
 
Huo nao ni mtihani lakini kama Bi mkubwa nimuelewa ni kukaa naye chini na kumueleza kwanini unataka kumuoa huyu mazuri yake yote yaanike hadharani sasa ikija kwenye umri hapo ndio kasheshe bi mkubwa anaweza kugoma,

tatizo kama ile Biological clock imeshapitiliza na Bi mkubwa anataka wajukuu. Katika dunia ya leo kuwapata wanawake kama huyu ni nadra sana na ndio sababu moyo wako unasita kumuacha huyu mpaka ukaamua kuja hapa kuomba ushauri.

Huyu ana watoto tayari. Mwanamke akishazaa mara ya kwanza, hata akiwa 45 anazaa tu bila tatizo lolote. Hivyo huyu anazaa watoto 3 bila hata ya chenga.
 
Back
Top Bottom