Nitamuachaje mmama huyu anae nizidi miaka tisa?

Nitamuachaje mmama huyu anae nizidi miaka tisa?

KALINZI NYUMBANI

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2015
Posts
2,081
Reaction score
2,179
Wakuu salama,

Kipindi nipo form five,nilipata demu mmoja hivi tulie kuwa tunalingana nae hakika tulipendana sana. Baada ya kumaliza form six sote tulifaulu, tukawa tumechaguliwa chuo, lakini tulienda vyuo tofauti. Baada ya kufika chuo tulipomaliza semister ya kwanza, huyo msichana alianza kuniletea mizinguo nikamvumilia sana mwisho wa siku tukaachana.

Sasa baada ya kuachana nae nilipokuwa naenda likizo nyumbani huko mkoani, niliona nikatafute mwanamke anae nizidi umli labda yeye atatulia. Sasa nilipofika nyumbani mta kama wa tatu kutoka nyumbani, alikuwepo mwanamke fulani hivi mwenye watoto wawili. Ambae mume wake alifariki kwa ajali ya gari.

Nikawa nimemtokea akawa amekubali lakini kiumri alikuwa mkubwa kwangu, alkuwa ananizidi miaka tisa.Sasa baada ya kuanza mahusiano nae baada ya kama miezi mitano na kwa vile alionyesha kuniheshimu sana na kunijali sana. Nilimshauli tuanza nae biashara akawa amekubali. Nilianza na mtaji wa laki nne ambayo nilikuwa nmeibana kutoka kwenye BUM.

Nikaanza kwa kununua madira na vitenge nikawa navisafirisha kwenda mkoani, akawa anauza kwa mkopo kwa wanawake wenzake. Kila mwisho wa mwezi akawa ananitumia hela nanunua mzigo nausafirisha anaupokea dhen anauza.

Tumefanya biashara hiyo ndani ya miaka miwili, nampaka ninavyoongea hivi sasa kanizalishia faida ya milioni kumi na moja nimeihifadhi benki na bado tunaendelea kufanya nae kazi na kugegedana pia.

Lakini sasa mwaka huu namaliza course yangu ya Mechanical Engineering na tatizo anadai nikimaliza nimuoe. Kusema kweli simpendi hata kidogo lakini nipo nae kwa ajili ya kumgegeda na kufanya nae biashara hiyo.

Sasa waungwana mpaka sasa sijui nimuachaje maana nmeshafanya majaribio ya kumuacha mwaka huu takribani mara mbili lakini wapi! maana kaniganda sana.Sasa kiukweli mie siwezi kumuoa na wala simpendi na tatizo kubwa ni umri wetu mimi na yeye. Kwahiyo wakuu nifanyeje huyu mwanamke niweze kuachana nae?

Naombeni ushauri

Asanteni sana.

..........................
...........................
Mrejesho leo 06/01/2016

Niliamua kuachana nae,sikuwa tayari kuoa mtu ambae tayali ana watoto.

Pesa tuligawana nusu kwa nusu,na kwa bahati nzuri anatarajiwa kuolewa mwaka huu.Ingawa bado nawasiliana nae na anafahamu kama mi namsichana mwingine lakini bado anataka niwe namgegeda.

Anadai hata akiolewa awe hata mchepuko wangu.

Nimesema noo.

Asanteni wale wote mlio toa ushauli katika uzi huu.Mungu awabariki sana.

 
Last edited:
Usifanye majaribio ukiwa mbali!
Kaa naye ongea naye kiume, msaidie mtaji naye Aweze kujikimu hata kama hukumkuta navyo but ni moyo tu wa kibinadam
 
Usifanye majaribio ukiwa mbali!
Kaa naye ongea naye kiume, msaidie mtaji naye Aweze kujikimu hata kama hukumkuta navyo but ni moyo tu wa kibinadam
Hamnashida mkuu nimeongea nae sana lakini hasikii kitu zaidi ya kutaka nimuoe.Kuhusu mtaji kiukweli lazima nimpe.
 
Oa mwanamke mwingine yeye mwenyewe atakuacha tu, umezaa nae watoto wangapi??
 
Hapo umepatikana, na usijaribu mbinu zako akagundua atakutoa uhai mapema
 
Biashara mmefanya pamoja na kuingiza faida ya milioni 11. Mpe milioni 5 zake kama shukrani yake kwa kuletea faida kisha umwambie ukweli,

"Mimi sina mapenzi kabisa na wewe hivyo siwezi kukuoa nilikuwa nakufanya kipozeo tu tu ili kupunguza genye zangu. Hii hapa ni milioni 5 ambayo ni faida yetu katika biashara tuliyoifanya pamoja." Kisha unasepa zako kimoja.
 
Wenzio tunatafuta wanawake wenye akili ya kusaka pesa kama hao, wewe ndio unamtupa? Kweli tumetofautiana sana aisee!
Mwanamke mwenye uwezo wa kusimamia majukumu akiwa peke yake bila mashauzi na kujitegemea, kwangu ni asset ya maana kuliko chochote.
 
Biashara mmefanya pamoja na kuingiza faida ya milioni 11. Mpe milioni 5 zake kama shukrani yake kwa kuletea faida kisha umwambie ukweli,

"Mimi sina mapenzi kabisa na wewe hivyo siwezi kukuoa nilikuwa nakufanya kipozeo tu tu ili kupunguza genye zangu. Hii hapa ni milioni 5 ambayo ni faida yetu katika biashara tuliyoifanya pamoja." Kisha unasepa zako kimoja.
Sawa mkuu nimekuelewa zaidi ya sana,Asante sana.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom