Nitamuachaje mmama huyu anae nizidi miaka tisa?

Nitamuachaje mmama huyu anae nizidi miaka tisa?

Heee amekuingizia pesa yote na humtaki tena mnaishi jirani? Utarogwa tu.
 
Ok, kama unayakumbuka maneno yako uliyotumia wakati unamtokea tumia hayo hayo ila yapindue
 
BAK kwanza kabs atuambie huyo mke ni kabila gani
tupo apa yaani akimtema tu kama huyu mama/binti anampenda yaan atamloga adi akome
atajazwa minuksi adi aone maisha yamesmama...................
hakuna kaitu kibaya kama kucheza na hisia za mtu
Mkuu huyo mwanamke ni msukuma.
 
Mdogo wangu oa huyo mwanamke,nakwambia maisha ni maelewano na mafanikio,tunawatafuta sana hao hatuwapati.
 
KALINZI NYUMBANI

Huyo ana uwezo wa kizaa hata watoto wawili. Siwezi kukushauri umuoe, kwani ni dhahiri humpendi kabisa ila umri umeiona kuwa ni sababu strong ya kujustify kumuacha kwa sababu angekuwa moyoni mwako, swala la umri ungeliweka pembeni na swali ambalo ungelileta hapa lingekuwa jinsi ya kuwashawishi ndugu na jamaa zako ili wampokee kama sehemu ya familia.

Usichokiona kwa sasa ni kuwa, huyo ni mwanamke anaejua maisha kwani alikwishayaanza kabla yako na akakomazwa kwa ndoa na uzazi. Hahitaji training kwani ana akili na uwezo wa kutambua na kufanya maamuzi sahihi yenye manufaa kwake na kuweka pembeni yasiyo ya msingi tofauti na mtu alie na umri mdogo au alie immature kiakili.

Kuna watu wameoa wanawake wanaojua sana label za bia, lakini hawawezi hata kununua au kuingiza units za luku. Wengine wanajua kuvaa na kutumbua sana ila mpe mtaji umwambie; "Baby, hebu izungushe hii milioni 5, usomeshe watoto wetu na kile nachopata mimi (mume) tukitumie kumalizia mjengo wetu". Ndani ya mwezi tu atakwambia biashara imemshinda kwa sababu hajazoea kupigizana kelele na wateja, kukaa sehemu moja au kuzunguka. Sasa muulize ulipo mtaji uliompa. Hapo ndipo utakapozusha ugomvi ambao hutausahau.

Kipindi ulipozinguliwa, uliapa kutafuta mtu mzima, ukampata anaefaa kabisa, ila unapokaribia kugraduate, unamuona hafai na inawezekana na tayari umeishampoint unaemwona anafaa zaidi, sasa yakijirudia wakati hizo ml 11 zimeishapukutishwa benki, uje utupe mrejesho pia.
 
Last edited by a moderator:
Huyo ana uwezo wa kizaa hata watoto wawili. Siwezi kukushauri umuoe, kwani ni dhahiri humpendi kabisa ila umri umeiona kuwa ni sababu strong ya kujustify kumuacha kwa sababu angekuwa moyoni mwako, swala la umri ungeliweka pembeni na swali ambalo ungelileta hapa lingekuwa jinsi ya kuwashawishi ndugu na jamaa zako ili wampokee kama sehemu ya familia.

Usichokiona kwa sasa ni kuwa, huyo ni mwanamke anaejua maisha kwani alikwishayaanza kabla yako na akakomazwa kwa ndoa na uzazi. Hahitaji training kwani ana akili na uwezo wa kutambua na kufanya maamuzi sahihi yenye manufaa kwake na kuweka pembeni yasiyo ya msingi tofauti na mtu alie na umri mdogo au alie immature kiakili. Kuna watu wameoa wanawake wanaojua sana label za bia, lakini hawawezi hata kununua au kuingiza units za luku. Wengine wanajua kuvaa na kutumbua sana ila mpe mtaji umwambie; "Baby, hebu izungushe hii milioni 5, usomeshe watoto wetu na kile nachopata mimi (mume) tukitumie kumalizia mjengo wetu".

Ndani ya mwezi tu atakwambia biashara imemshinda kwa sababu hajazoea kupigizana kelele na wateja, kukaa sehemu moja au kuzunguka. Sasa muulize ulipo mtaji uliompa. Hapo ndipo utakapozusha ugomvi ambao hutausahau.Kipindi ulipozinguliwa, uliapa kutafuta mtu mzima, ukampata anaefaa kabisa, ila unapokaribia kugraduate, unamuona hafai na inawezekana na tayari umeishampoint unaemwona anafaa zaidi, sasa yakijirudia wakati hizo ml 11 zimeishapukutishwa benki, uje utupe mrejesho pia.

Mkuu asante sana kwa ushauli wako,But unajua mimi nmezaliwa huko kijijini tunapotafutiwa wake wakuoa.Pia hofu yangu kubwa ni pale ntakapo mpeleka kijijini kwa bi MKUBWA.Hio ndio nahofia zaidi.Kuhusiana na kuwa na binti mwingine wala sina.

Na lengo lakuleta huu mjadala wangu hapa nikupata mawazo mbalimbali ili mwisho wa siku nafanye maamuzi.Napia niliahidi kuwa ntamuoa ili afanye kazi akiwa anajua anaandaa maisha yetu.Ndio maana nikasema tatizo kubwa ni umri ndio unao sababisha nisimpende.

Mkuu asante sana kwa ushauli wako murua.
 
Wenzio tunatafuta wanawake wenye akili ya kusaka pesa kama hao, wewe ndio unamtupa? Kweli tumetofautiana sana aisee!
Mwanamke mwenye uwezo wa kusimamia majukumu akiwa peke yake bila mashauzi na kujitegemea, kwangu ni asset ya maana kuliko chochote.


wenzio wanaogopa wanawake wenye akili kama ukoma wanataka mabwege cjui hawajiamin
 
wenzio wanaogopa wanawake wenye akili kama ukoma wanataka mabwege cjui hawajiamin

Binadamu tumetofautiana sana, mwanamke anakuzalishia pesa unampiga chini? I'll fight for mwanamke wa hivyo, kumuacha itakuwa ngumu, labda kuwe na sababu solid.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
piga chini...isiwe kesi...au umesahau uchawi hauendi kwa mental...!!!?
 
Liishalo ndilo jema kuliko linalokuja............
 
Binadamu tumetofautiana sana, mwanamke anakuzalishia pesa unampiga chini? I'll fight for mwanamke wa hivyo, kumuacha itakuwa ngumu, labda kuwe na sababu solid.



watu ni tofauti kuna mwanaume alishanambia wew mwanamke unawaza mambo ya kiwanja si utakuja kunikalia wew duuuu
 
watu ni tofauti kuna mwanaume alishanambia wew mwanamke unawaza mambo ya kiwanja si utakuja kunikalia wew duuuu

Hahaha! Dah! Hiyo kiboko aisee! Kwa hiyo alikuwa anataka muwe mnatumbua tu bila kupanga maendeleo? Inachekesha sana!
 
Back
Top Bottom