Gorgeousmimi
JF-Expert Member
- Jun 21, 2010
- 9,296
- 7,688
piga chini...isiwe kesi...au umesahau uchawi hauendi kwa mental...!!!?
Haaa we definition!!!:shock::shock:
Last edited by a moderator:
piga chini...isiwe kesi...au umesahau uchawi hauendi kwa mental...!!!?
Sasa kwanini umuache mwanamke kama huyu banaaa!? Mungu akupe nini tena? Dah! Unaweza kuja kumkumbuka sana huyu utakapokuwa unapelekeshwa puta na huyo mpya ukiamua kurudi kwake utakuta njemba nyingine imeshatia nanga.
Usifanye makosa hayo banaaa umri si kikwazo kihivyo cha kukufanya wewe umuache huyu mmetoka naye mbali huyu na amekusaidia sana. Unaweza kupata laana ya Mungu. Usimuache Mkuu.
Haaa we definition!!!:shock::shock:
namwonea huruma anapelepwetwa...!!!! ukute ndo walewale wajane wa kichaga...lazma na yy akate moto..milioni 10 itiwe kibindoni.
Umri ndio unasababisha nisimpende.
utakua mtamu sana wewe
We bana itabidi nikupunge,I wish pangekuwa na kitufe cha dislike nikibofye!!Mpe hongera na moyo mwenzio kapata mwanamke ambae ni aghalabu kupatikana kwa dunia ya sasa!Hawa vijana wenzio kubebana mzigo!!
Ha ha ha utoto unakusumbua na wewe.....dah..!!! afu nme sahau kuku salimia.."shikamo" jamaa nahisi ana nyota ya makombo....bahati ipi mama anajua ana soko tena ndo.maana kawa rubaa...!!!!
Mkuu kumpenda nampenda lakini umri ndio unasababisha nisimpende,But kiukweli ananisikiliza sana mpaka kumfanyia ujinga ili tuachana najishtukia sana.Maana ananisikiliza kinoma na akikosa ni mwepesi kukili kosa na kuomba msamaha.
Mkuu asante kwa bandiko lako hili,Ila tatizo hujapiga mahesabu vizuri.Kama hiyo story sio ya kutunga kama tulivyozoea kwa watu wa aina yako huku kwanza nakuambia yafuatayo:
Wewe inaonyesha unajivuna halafu hujatulia hata hiyo course sidhani kama ni kweli umesoma wewe muongo ni story tuu
Pili hakuna mwanamke utakae mpa laki 4 gafla aje azalishe milioni 11
na bado ana familia ya watoto 2 leo hii unakuja kupost story za kumuacha
Tatu ka ulikuwa humpendi utampaje hela wewe bila shaka upo darasa la saba na story za mapumziko ya saa nne wakati unasubiri uji
Mkuu nimekuelewa zaidi ya sana but vipi bi mkubwa atalichukuliaje suala hili,Kwa sababu mama zetu huwa wanamaindi mishe hii ya kuoa mtu anae kuzidi.
Mkuu nilikuwa nahofu kama atakuwa bado na uwezo wa kupata mtoto,Pia na bi mkubwa atalichukuliaje suala hili.Kuumiza hisia za mwanamke ni noma sana,na hilo tatizo la umri ni sababu ya wazazi wako au ni mtazao wako tu mwenyewe?
Mkuu nahitaji ushauli ndio maana nipo hapa.Na sio vinginevyo.Mi naona kaja kutamba tu!
Ha ha ha utoto unakusumbua na wewe.....
Mkuu nimekuelewa sana tena zaidi ya sana.BAK utoto unamsumbua kijana huyu...anachezea shillingi chooni...muhimu mwanamke ana kizazi 34 bado anaweza amzalie watoto aache mirathi...hata mtume Muhammad (S.A.W) alimuoa bi khadija alomzidi umri sana.Umri sio kikwazo kwa kijana.Kikwazo ni yeye mwenyewe na vizingiti vyote anavieka yeye.
Duu mkuu mbona unanitisha na kunikatisha tamaa!.Mkuu KALINZI NYUMBANI usithubutu kamwe kuoa mwanamke mwenye mtoto hata mmoja, mwenzako yaliyonikuta siwezi sahau japokuwa bado sijaoa.
BAK utoto unamsumbua kijana huyu...anachezea shillingi chooni...muhimu mwanamke ana kizazi 34 bado anaweza amzalie watoto aache mirathi...hata mtume Muhammad (S.A.W) alimuoa bi khadija alomzidi umri sana.Umri sio kikwazo kwa kijana.Kikwazo ni yeye mwenyewe na vizingiti vyote anavieka yeye.
Msichana yoyote alobalehe anaweza kuolewa ndivyo dini inavyosema!Kama mhusika ni muislam atanielewa sana tu!!Na waislam wanashauriwa waoe wanawake wajane ka hivo unapata thwawabu kubwa sana kwasababu atamstiri huyo mwanamke na hao mayatima....Mkuu muhamad sio mfano mzuri kwa upande wa masuala ya mahusiano, maana kuna sehemu alioa mtoto wa miaka 9 ambaye kwa sasa angekuwa darasa la 2, sina maana kwamba hakuwa na mazuri ya kuigwa bali yapo lakini sio kwa upande wa mambo ya ndoa.