Brigedia Chan-ocha
JF-Expert Member
- Mar 7, 2014
- 1,353
- 2,842
Natarajia kufungua kesi mahakama kuu dhidi ya jeshi la polisi, naitaka mahakama kuu itoe tafasiri na/ muongozo wa je Jeshi la polisi linaruhusiwa kuteka raia au kukamata raia? Na Je kukamata ni sawa sawa na kuteka? Na je utaratibu wa kuteka raia unatakiwa uweje? Yaani kabla raia hajatekwa ni hatua zipi za kufuata kabla ya tukio hilo? Na je ni haki zipi za mtu anayetekwa na polisi?
Utaratibu wa kukamata Raia unajulikana ila utaratibu wa kuteka raia haujulikani, kwa hiyo nitaiomba mahakama kuu itoe utaratibu mzima, na kama ni halali au haramu kwa polisi kuteka raia itamke waziwazi, na nitaiomba mahakama kama kuteka ni kitendo haramu basi itoe adhabu kali kwa polisi yeyote atakayejihusisha na utekaji raia.
Naiomba mahakama kuu isiogope kupokea na kusikiliza shauri hili, iige wenzao wa kenya wanavyotoa maamuzi bila kuangalia sura ya mtu.
Nawasilisha.