Tatizo ni moja :
Watu wema wameamua kuwa chini ya waovu.
Bado bara la Afrika halijakombolewa.
Waafrika wanajazana Makanisani na Misikitini kutetea nafsi zao huku wakishiriki au wakitumika au wakinyamazia nafsi za Waafrika wenzao zikiwa zinaangamizwa na binadamu wenzao waliolewa madaraka na Mali.
Yaani Kikundi cha watu wachache waovu kimewakalia watu wema kwa nguvu ya pesa na Madaraka.
Kwa sasa CCM kwa kulitumia Jeshi la Polisi haina habari tena na kitu kinachoitwa siasa safi ya ushawishi na kuwaheshimu wapiga kura kwa kuwa wapende wasipende watashinda Kwa nguvu ya Polisi.
Hata hivyo Mleta mada kuna tatizo kwa wananchi bado hawajawaelewa wale wanaolalamika kuwa wanatekwa au kuteswa au ndugu zao kupotea.
Magereza yamejaa maskini huku wahalifu dhidi ya binadam na mali za umma wakiwa wanaheshimika na kukalia ofisi za umma kwa mitutu ya Bunduki.
Ni vyema sasa watu wema wanaojua wazi kuwa hawana hatia lakini wanashitakiwa kwa uongo wakaungana kwa pamoja na kutafuta watu waaminifu sana ,wakachanga fedha kwa ajili ya kugharamikia kesi dhidi ya watawala wanaotumia vibaya madaraka yao kuumiza na kupoteza watu.
Hata mitaani unakuta kibaka mmoja anawanyima watu zaidi ya 100 usingizi na kupora watu bila aibu . Yani kibaka mmoja anatoa vitisho na watu wote wanajifungia kwenye mageti kila mmoja na mlango wake. Badala ya watu 100 wema kuungana na kumdhibiti kibaka mmoja wao ndio wanadhibituwa na kibaka kwa hofu.
Afrika tumependa hivyo ndio maana watu wastarabu wanasema achana na siasa ni mchezo mchafu. Matokeo yake waovu wenye michezo michafu wanawahonga wenye mamlaka ya kidola ili waingie kwanye siasa na wao wanakula Mali za umma kama wanavyotaka . Wanakula bata tu.
Mwaka Jana watumishi wa umma zaidi ya 43000 wakiwemo Polisi walichukua fomu za kugombea Ubunge kupitia CCM. Ni Jeshi la wananchi pekee ndio ambao hawakuchanganya siasa na Jeshi kama Katiba inavyosema. Wengine wote walikimbilia CCM na kugombea kinyume cha katiba.
Wavunja sheria ndio wanaotangulia na kuwakamata watu wema.
Sent from my TECNO L8 Lite using
JamiiForums mobile app