Nitafungua kesi dhidi ya Jeshi la Polisi

neno "kutekwa" limetumiwa vibaya na Adamoo, amelitumia neno hilo kwa maksudi kwa nia ya kupotosha.

Hata Mbowe alivyo kamatwa kule mwanza wafuasi na viongozi wa CDM walizusha kwa maksudi kuwa eti mbowe "Katekwa"!! huku wakifahamu fika kuwa kakamatwa na Jeshi la Polosi.

Wafuasi wa Mbowe na baadhi ya viongozi wenzake wamekuwa na tabia ya kuzusha na kupotosha habari kwa maksudi na kwa nia ya kuihadaa jamii kwa nia ya kuhalalisha maovu yao.
Jamii iwaelewe hivyo lkn pia vyombo vyetu vya ulinzi na usalama wanapaswa wajue tabia na nia ovu ya watu hao.
Mkuu

Nakumbuka wakati tuko sekondari tuliambiwa... mwalimu akikupiga ngumi, huo ni ugomvi sio adhabu ya kishule i.e unaruhusiwa kujilinda na wewe ukarusha ngumi.

Inapotokea Polisi wanakamata mtu bila kufuata taratibu za kikatiba, sheria na miongozo yao kama polisi, huo ni UTEKAJI.

Tito Magoti amekamatwa na "polisi" wakiwa na nguo za kiraia, hawakujitambulisha, walikuja na gari isiyotambulika, hawakumwambia kosa lake, wamempeleka polisi bila kumpa nafasi ya kuwasiliana na jamaa zake na huko polisi hakumwandika jina lake etc. Hebu piga picha kwa mfano angekuwa ana maradhi fulani, katika purukushani akafariki, unadhani polisi wangekuja kusema ilikuwa ni sisi?

Kwa ufupi kama taratibu hazijafuatwa, huo ni utekaji. Ndio maana Zakaria wa Tarime alipowatwanga risasi wale wasiojulikana, walishindwa kumpa kesi ya kuwapiga jamaa risasi; kwa sababu sheria iliyorasimisha idara ya usalama haiwaruhusu kukamata, alikuwa na haki kabisa ya kujitetea. Ila wale wangekuwa askari wa kawaida pengine angekuwa na kesi kubwa zaidi.
 
Natarajia kufungua kesi mahakama kuu dhidi ya jeshi la polisi, naitaka mahakama kuu itoe tafasiri na/ muongozo wa je Jeshi la polisi linaruhusiwa kuteka raia au kukamata raia? Na Je kukamata ni sawa sawa na kuteka? Na je utaratibu wa kuteka raia unatakiwa uweje? Yaani kabla raia hajatekwa ni hatua zipi za kufuata kabla ya tukio hilo? Na je ni haki zipi za mtu anayetekwa na polisi?

Utaratibu wa kukamata Raia unajulikana ila utaratibu wa kuteka raia haujulikani, kwa hiyo nitaiomba mahakama kuu itoe utaratibu mzima, na kama ni halali au haramu kwa polisi kuteka raia itamke waziwazi, na nitaiomba mahakama kama kuteka ni kitendo haramu basi itoe adhabu kali kwa polisi yeyote atakayejihusisha na utekaji raia.

Naiomba mahakama kuu isiogope kupokea na kusikiliza shauri hili, iige wenzao wa kenya wanavyotoa maamuzi bila kuangalia sura ya mtu.

Nawasilisha.
R.I.P HAMZA
 
Back
Top Bottom