Nisipost chakula na nisile mbele yako kisa jirani umefunga? Ni wazi unajilazimisha kushinda njaa wala hujafunga kwa imani

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,080
Hizi tabia za kulazimisha jambo la watu fulani liwe la wote nazichukia sana, Sio wote ila ni wale wanaofunga kwa kushinda njaa, wale wanaofunga kwa imani wala sina shida nao.

Nashangaa nikiweka status za vyakula kuna baadhi ya njemba zinakuja inbox eti huu mwezi mtukufu sio vizuri kupost chakula wengine tumefunga 😂 Huo mwezi mtukufu ni kwa wote? yaani nile biriani nisipost kisa umefunga ?

1711130847827.png


Ofisini tuna kawaida ya kuagiza chai na lunchi, Kwaresma ilipoanza sisi ambao hatukufunga tuliendelea kula hapo ofisni. yani tunakula kuku, pilau, juice, n.k. mbele ya waliofunga bila tatizo, ni wazi kabisa nguvu ya imani kwenye funga zao zilishinda matamanio ya kimwili (njaa). ila sasa hivi karibuni kwenye mfungo mpya kuna baadhi ya wahusika wenye imani finyu wameanza kauli za ajabu kwamba tunaokula ofisini tuwe tunaenda kulia kantini kwa kisingizio cha sisi tusiwaingiz tamaa, ni jambo linaloshangaza maana inaonekana funga yao ipo kimwili zaidi kuliko kiimani.

Nilishawaambia wao kama wanaona wanatamani tunavyokula ni wazi wanashinda njaa wala hawafungi kwa imani ni vema watujoin ama kama vipi wawe wanatoka nje kula upepo wakiona imani zao ni nyepesi kuzidi tumbo, Sio sisi tubadili utaratibu ila ni wao ndio wabadili utaratibu, nashukuru wengi wapo nyuma yangu kwenye hili.

Huwa nawaambia live bila chenga wanajilazimisha kushinda njaa wala hawajafunga kwa imani.

Mtu aliefunga kwa imani funga yake haiwezi kuharibiwa hata umweke jikoni.
 
Lakini hata kula chakula mbele ya aliyefunga kwa makusudi ni dhambi sana...,,majaribu siyo mazuri
 
Back
Top Bottom