Kisa cha Nabii Mzee na Nabii Kijana jinsi kinavyoweza kuimarisha Imani yako

Shemasi Jimmy

Member
Apr 23, 2021
93
104
KISA CHA NABII MZEE NA NABII KIJANA JINSI KINAVYOWEZA KUIMARISHA IMANI YAKO

Na Shemasi Jimmy 0659611 252

Awali ya yote nawasalimu kwa Jina kuu kupita majina yote; Bwana Yesu apewe sifa.

Ungana nami shemasi wako katika simulizi hii nzuri inayopatikana katika kitabu cha 1fal 13:1-34, huku tukitazama jinsi simulizi hii inavyoweza kuimarisha imani na tumaini tulionalo ndani ya mioyo yetu.

Ikiwa baada ya mgawanyiko wa makabila 12 ya wana wa Israeli(Israeli na yuda), mfalme Yerobohamu wa Israeli ya kaskazini alianza kufanya chukizo mbele za Mungu. Na hivyo Mungu akaamua kumtuma mjumbe wake(nabii kijana) kwa lengo la kumuonya mfalme ili aache uovu. Baada ya kufika na kumuonya mfalme Yerobohamu ambae alikua kwenye madhabahu ya miungu akitoa dhabihu na kufukiza uvumba, mfalme Yerobohamu alinyoosha mkono wake akiamuru walinzi wamkamate mara moja nabii huyo, mara ghafla mkono wa mfalme Yerobohamu ukakatika na kudondoka chini. Mfalme yerobohamu akamuomba nabii kijana akimsihi amuombe Mungu wake ili amrudishie tena mkono wake. Yule nabii akaomba na mkono ukarejea tena kama awali.

Mfalme Yerobohamu akamwalika nabii Yule ili wapate kula na kunywa pamoja kama sehemu ya shukurani yake kwa mtu huyo wa Mungu. Nabii kijana akakataa mwaliko ule akimueleza kua Bwana amemuamuru asile wala kunywa tena asirudi kwa njia aliotumia kufika mahali pale. Nabii Yule akaondoka na njia nyingine kama alivyoagizwa na Bwana.

Kumbe wakati nabii Yule kijana akinena kufanya yote yale mbele ya mfalme,kulikuepo watoto waliosikia na kuona yote yaliotendeka kwa mfalme. Watoto hao walipeleka habari kwa baba yao(nabii mzee). Yule nabii mzee akamfuata na kumlaghai mtu wa Mungu, akimkaribisha chakula na vinywaji nyumbani kwake lakini mtu Yule wa Mungu(nabii kijana) akamweleza ukweli jinsi neno Mungu alivyomzuia kula wala kunywa tena asirudi kwa njia aliyopita awali.

Nabii mzee akamlaghai kwa kumwambia kua mimi ni nabii wa Bwana kama wewe, Bwana ameniambia nikwambie tuambatane pamoja hadi nyumbani kwangu, ule na kunywa pamoja name. walakini nabii huyo alikua muongo. Nabii kijana akamwamini nabii mzee akafanya kama alivyoambiwa na nabii huyo, kinyume na neno la Bwana. Akala na kunywa nyumbani kwa nabii mzee, akarudi kwa njia aliyopita awali kinyume na agizo la Bwana. Ndipo neno la Bwana likamjia nabii mzee, akamwambia nabii kijana huku akilia kua Bwana amesema hakika atakufa kwa kua amekiuka agizo la Bwana.

TUNAPATA FUNZO GANI
1)USIAMINI KILA ROHO INAYOKUJIA BALI ICHUNGUZE KWANZA.(1 YOH 4:1, MIT 14:15). Nabii kijana ni mfano wa wakristo wengi tunaoamini kila roho pasipo kuichunguza. Nabii kijana alikua na nafasi ya kumuuliza Mungu yale aliyoambiwa na nabii mzee akini hakufanya hivyo. Tujenge tabia ya kusoma neon la Mungu ili tupata uwezo wa kupima roho zote zituijiazo. Mfano huu hauna tofauti na jinsi shetani alivyomlaghai Hawa katika mwanzo3:4 kinyume na agizo la Mungu katika mwanzo 2:17. Mkristo kua makini tupo katika nyakati za mwisho.

Je, wewe umejifunza nini kupitia simulizi hii.
 
Nabii mzee akamlaghai kwa kumwambia kua mimi ni nabii wa Bwana kama wewe, Bwana ameniambia nikwambie tuambatane pamoja hadi nyumbani kwangu, ule na kunywa pamoja name. walakini nabii huyo alikua muongo. Nabii kijana akamwamini nabii mzee akafanya kama alivyoambiwa na nabii huyo, kinyume na neno la Bwana. Akala na kunywa nyumbani kwa nabii mzee, akarudi kwa njia aliyopita awali kinyume na agizo la Bwana. Ndipo neno la Bwana likamjia nabii mzee, akamwambia nabii kijana huku akilia kua Bwana amesema hakika atakufa kwa kua amekiuka agizo la Bwana.
20Wakati walipokuwa wameketi mezani, neno la Bwana likamjia yule nabii mzee aliyemrudisha huyo mtu wa Mungu. 21 Akampazia sauti yule mtu wa Mungu aliyekuwa ametoka Yuda, “Hivi ndivyo asemavyo Bwana: ‘Umeasi neno la Bwana na hukushika amri uliyopewa na Bwana Mungu wako, 22bali ulirudi na ukala mkate na kunywa maji mahali ambapo alikuambia usile wala usinywe. Kwa hiyo maiti yako haitazikwa katika kaburi la baba zako.’ ”
23Wakati huyo mtu wa Mungu alipomaliza kula na kunywa, nabii aliyekuwa amemrudisha akamtandikia punda wake. 24 Alipokuwa akienda akakutana na simba njiani, akamuua na maiti yake ikabwagwa barabarani, yule punda wake na simba wakiwa wamesimama karibu yake. 25Baadhi ya watu waliopita pale waliona maiti imebwagwa pale chini, simba akiwa amesimama kando ya maiti, wakaenda na kutoa habari katika mji ambao nabii mzee aliishi.
26 Yule nabii aliyekuwa amemrudisha kutoka safari yake aliposikia habari hii akasema, “Ni yule mtu wa Mungu ambaye aliasi neno la Bwana. Bwana amemtoa kwa simba, ambaye amemrarua na kumuua, sawasawa na neno la Bwana lilivyokuwa limemwonya.”
27Nabii akawaambia wanawe, “Nitandikieni punda,” nao wakafanya hivyo. 28Kisha akatoka akaenda akakuta maiti imebwagwa chini barabarani, punda na simba wakiwa wamesimama kando yake. Simba hakuwa amekula ile maiti wala kumrarua punda. 29Basi yule nabii mzee akachukua maiti ya mtu wa Mungu, akailaza juu ya punda na akairudisha katika mji wake, ili amwombolezee na kumzika. 30 Kisha akailaza ile maiti katika kaburi lake huyo nabii mzee, nao wakaomboleza juu yake na kusema, “Ee ndugu yangu!”
31 Baada ya kumzika, akawaambia wanawe, “Wakati nitakapokufa, mnizike kwenye kaburi alimozikwa huyu mtu wa Mungu; lazeni mifupa yangu kando ya mifupa yake.
32 Kwa maana ujumbe alioutangaza kwa neno la Bwana dhidi ya madhabahu huko Betheli na dhidi ya madhabahu yote katika mahali pa juu pa kuabudia miungu katika miji ya Samaria, hakika yatatokea kweli.”
 
Hiki kisa mbona kina maswali mengi sana?

Kwanini Nabii wa Mungu mzee amlaghai nabii kijana,lengo lake lilikuwa nini?

Kwanini Mungu akamtumia tena Nabii huyo laghai kufikisha ujumbe wa adhabu kwa Nabii kijana?

Kwanini Nabii mzee hakupewa adhabu kwa kudanganya?
 
Yale Yale Ya Sauli Kutotii Sauti ya Bwana Mungu

Samweli Muonaji Akamwambia tu hivi SAULI

INGAWA ULIKUWA MDOGO MACHONI PAKO MWENYEWE JE HUKUFANYWA KUWA KICHWA CHA KABILA ZA ISRAEL

Nisamehe Zikawa Nyingi Kutoka Kwa Sauli Lakini Ilikuwa It's Too late TOKA PALE KIFO KILIANZA KUMTAFUTA SAULI

1 Samweli 15:31
 
..... ., mfalme Yerobohamu alinyoosha mkono wake akiamuru walinzi wamkamate mara moja nabii huyo, mara ghafla mkono wa mfalme Yerobohamu ukakatika na kudondoka chini. Mfalme yerobohamu akamuomba nabii kijana akimsihi amuombe Mungu wake ili amrudishie tena mkono wake. Yule nabii akaomba na mkono ukarejea tena kama awali....
Je, wewe umejifunza nini kupitia simulizi hii.
Ufunuo wa Yohana 22:18
Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.
 
Back
Top Bottom