Nisikilize: Mkeo si ndugu yako

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Jun 23, 2022
227
333
Wanaume nisikilize mimi, ukikutana na mwanamke mzuri muoe zaa nae watoto jenga familia pamoja naye.
Anaweza kuwa rafiki yako bora, msiri wako, mfanya biashara wako mshirika.

Na Unaweza kumuona kama mshirika wako wa karibu kwenye maombi pindi utakapomua kwani wanandoa huanza kufanana wakidumu pamoja.

Lakini usisahau nguvu iliyowaunganisha inaweza kuingia kutu kulingana na muda na kubadilika kwa moyo.
Mke wako sio ndugu yako wa damu na upendo wake unaweza kubadilika kuwa chuki ndani ya usiku mmoja.

Nisikilize mimi mpendwa kaka yangu, kwenye Wakati wa mahaba, kwenye kilele cha mafanikio yako, mkumbuke kaka yako aliesimama na wewe wakati haupo imara na umkumbuke dada yako aliekusafisha wakati ukiumwa sana.

Wakumbuke pia waliotumia muda wao kukuambia usitupe maji ya baridi kwenye mgongo wako, mikono yako na kukuandalia maji moto yaliyoilea ngozi yako.

Usiwafungie milango watoto wanapokuja mbele ya uzio wako wakiwa na miguu yenye vumbi na nguo zilizochanika wakitaka msaada wako.

Usizibe pua yako ikiwa wananuka harufu mbaya, usizibe masikio yako ili usisikie matumbo yao yakiunguruma kutokana na kukosa shibe.

Wakaribishe kwa mikono mikunjufu fungua milango yako waite wale juu ya meza yako na watendee kadri ungependa utendewe.

Yajayo ni kama upepo yanaweza kuwa hayatabiriki kabisa unaweza ukajikuta upo kama ayubu wa kwenye biblia ukiwa mtupu mwenyewe kwenye kisiwa cha matatizo.

Dada yako aliyekuokota ukiwa unaumwa hujiwezi Kama mtoto asiye na matumaini atakutafuta akusaidie tena.

Ndugu yako katakushika mkono katika mapito yako yote kwakuwa nguvu iliyowaunganisha kwenye damu itazongwa na upepo lakini kamwe haiwezi kutenganishwa.

Peter Mwaihola
Elvinah Obuya, The Standard Kenya.

Photo_1692630897041.jpg
 
Walikuwaga ndugu wa zamani sio hawa wa leo wanaotamani wote tuwe masikini nikipata basi visirani huanza.

Nitampenda nitamjali nitamthamini nitamuamini nitakayemuweka ndani ila sio ndugu hivyo itoshe kusema niko tayari kusalitiwa na kutengwa na mtoto wa mama mkwe ila sio ndugu sababu hawanipi changamoto za kusonga mbele ila wivu majungu na unafiki tu.

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Hakuna aijuae kesho, maisha ya mwanadamu ni fumbo. Hakuna ajuae roho ya mwanadamu.. Mke na Mume ni mwili mmoja ili kuanzisha kizazi chao.. kama tukijua maana pana ya kuwa mwili mmoja.. kuna mawazo na hisia hatutoweza ziruhusu kuzunguka kichwani mwetu.. Maamuzi ya mwanadamu hutokana na taarifa ya aina gani iliyomo ndani mwake..
 
Ungeanza kwa kutoa sababu kwa nini tukusikilize wewe na sio Mwenyezi Mungu. Una hekima ipi kumzidi Mungu?

Kiwani nani alikudanganya mkeo ni ndugu yako? Kwa kuwa umerejea habari za maombi nani nitakujibu kwa maandiko:

Mathayo 19 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁵ ..... Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?

Maandiko hayajawahi kesema mke ni ndugu, bali mke wako ni WEWE!! Ninyi ni mtu mmoja, hivyo upoamini ndugu kuluko mkeo ni sawa na kujichukia na kujidharau mwenyewe. Ka hiyo hao ndugu hawabadiliki? Unamdharau mwenza wako anayeitunza afya yako ili upate nguvu za kutafutaahizo mali? Unambeza mkeo ambaye huyo ndiye anayekuzaliwa watoto na kukutengenezea familia? Ni heri basi ungezaa na hao ndugu zako ujenge nao ukoo.

Badilika sasa, vinginevyo ndoa itakushinda. Acha kabosa akili mbovu ya kumuona mkeo ni adui, kwqni unalolitamani ndilo hilo hilo litakuwa sehemu ya maosha yako. Be a man, a true husband.
 
Walikuwaga ndugu wa zamani sio hawa wa leo wanaotamani wote tuwe masikini nikipata basi visirani uanza .

Nitampenda nitamjali nitamthamini nitamuamini nitakayemuweka ndani ila sio ndugu hivyo itoshe kusema niko tayari kusalitiwa na kutengwa na mtoto wa mama mkwe ila sio ndugu sababu hawanipi changamoto za kusonga mbele ila wivu majungu na unafiki tu .

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Tena hao ndugu wa zamani walikuwa n busara sana, wasingekubali wao ndio uwaweke mbele badala ya mkeo. Ndugu anayeshabikia haya hana akili kabisa.
 
Mke sio Ndugu yako Kwa sababu ni zaidi ya Ndugu.
Mkeo ndiye Mwanadamu pekee ambaye alikuwa kiapo kukupenda japo sio Ndugu yako.

Wakati Ndugu zako wakisimama na familia zao. Mkeo ndiye atasimama na wewe.

Wakati Ndugu zako wakiwatelekeza Watoto wako. Mkeo ndiye atakayewatunza.

Kuhusu kukengeuka Kwa mke hata Ndugu zako wanaweza kukengeuka.
Huwezi mpima MKE Kwa mzani wa kukengeuka.

Ndugu zako haohao ndio wanauwezo WA kuwadhulumu Watoto wako Mali pale utakapokufa.

Ndugu zako haohao ndio wanaweza kukuloga au kuloga Watoto wako ili wabaki kuwa na Maisha Duni.

Mkeo sio Ndugu yako, Ila ni zaidi ya Ndugu.

Mkigombana na Ndugu au na mzazi unaweza ukalala na Kupata usingizi kabisa, na chakula ukala ukashiba.
Lakini gombana na Mkeo uone hicho chakula au usingizi kama utaupata.

Hapa unazungumzia Mapenzi na upendo wa Mume na Mke.
 
Back
Top Bottom