Nisikilize: Mkeo si ndugu yako

Nisikilize: Mkeo si ndugu yako

Mke sio Ndugu yako Kwa sababu ni zaidi ya Ndugu.
Mkeo ndiye Mwanadamu pekee ambaye alikuwa kiapo kukupenda japo sio Ndugu yako.

Wakati Ndugu zako wakisimama na familia zao. Mkeo ndiye atasimama na wewe.

Wakati Ndugu zako wakiwatelekeza Watoto wako. Mkeo ndiye atakayewatunza.

Kuhusu kukengeuka Kwa mke hata Ndugu zako wanaweza kukengeuka.
Huwezi mpima MKE Kwa mzani wa kukengeuka.

Ndugu zako haohao ndio wanauwezo WA kuwadhulumu Watoto wako Mali pale utakapokufa.

Ndugu zako haohao ndio wanaweza kukuloga au kuloga Watoto wako ili wabaki kuwa na Maisha Duni.

Mkeo sio Ndugu yako, Ila ni zaidi ya Ndugu.

Mkigombana na Ndugu au na mzazi unaweza ukalala na Kupata usingizi kabisa, na chakula ukala ukashiba.
Lakini gombana na Mkeo uone hicho chakula au usingizi kama utaupata.

Hapa unazungumzia Mapenzi na upendo wa Mume na Mke.
Ulipaswa kusema, wanaume tujue kecheza na "checks and balances" za ndoa na undugu kwa maana wote ni muhimu.
 
Walikuwaga ndugu wa zamani sio hawa wa leo wanaotamani wote tuwe masikini nikipata basi visirani uanza .

Nitampenda nitamjali nitamthamini nitamuamini nitakayemuweka ndani ila sio ndugu hivyo itoshe kusema niko tayari kusalitiwa na kutengwa na mtoto wa mama mkwe ila sio ndugu sababu hawanipi changamoto za kusonga mbele ila wivu majungu na unafiki tu .

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
We subiri siku upigwee Tukio.
 
Baada ya Mama yako aliyekuzaa ndugu wanaofatia ni Watoto zako.

Hao watoto wanapatikana kupitia Mke utakayemuoa.

Kama Mke amekuzalia Watoto kwanini usimuamini.

Ni mara mia kumwamini Mkeo kuliko ndugu.

Wakina Marehemu Mengi walitafuta pamoja na Mkewe hadi kufikia utajiri waliokuwa nao.

Kuna watu wengi wamekuwa -disappointed na ndugu zao kuliko Wake.

Tusisahau kumshirikisha Mungu kwenye kila hatua.

“Tusisahau kumshirikisha Mungu katika kila hatua.” Sahihi sana!


Imani dhaifu inawatesa sana binaadam wa sasa.
 
nakubaliana na wewe 100%, lakini hoja mada kama izi za kumwona mke sio sehemu mwili wako mume na msaidizi wako, zinaibuka kwa kasi sababu ya yanayoendelea na tuyaonayo kwenye ndoa za siku izi.

Hayo yanayoendelea kwenye ndoa siku hizi hayatoacha kutokea na yatazidi ubaya zaidi kama vijana wanaoingia ndoani wataendelea kuwa na akili kama za mleta mada.
 
Kweli kabisa, pamoja na maagano ya kuwa mwili mmoja bado sio ndugu. Ni watu mmekutana tena wa tamaduni tofauti kwa kusudi la kuanzisha familia. Watoto ndio wanaanzisha undugu.

Mnachekesha mnavyojikanyaga!


Mkeo sio ndugu ila watoto uliotengeneza na huyo mkeo ndio ndugu zako?


Baniani mbaya ila kiatu chake Dawa?
 
Undugu upo kwenye DNA. Huo haufutiki. Urafiki unafutika. Mke ni rafiki tu.

Hakuna rafiki atakaejitolea maisha yake kwa ajili yako.

Mkeo anajitolea maisha yake kwa ajili yako kwa kukuzalia watoto na kuendeleza kizazi chako.

Kutokufutika kwa undugu na ndugu zako hakuondoi ukubwa wa mke juu ya ndugu zako.

Mkeo ni wewe na Wewe ni Mkeo.
 
Ulipaswa kusema, wanaume tujue kecheza na "checks and balances" za ndoa na undugu kwa maana wote ni muhimu.

Hiyo alipaswa kusema Mtoa mada.

Kwenye huu Ulimwengu unapozungumzia Maisha ya viumbe unazungumzia Baba, Mama na watoto. Yaani Mume, MKE na watoto.

Mungu aliumba Mume na Mke. Ndugu walikuja baadaye.

Ndugu ni muhimu lakini hawawezi kuuzidi umuhimu wa Mume na Mke.
 
Ungeanza kwa kutoa sababu kwa nini tukusikilize wewe na sio Mwenyezi Mungu. Una hekima ipi kumzidi Mungu?

Kiwani nani alikudanganya mkeo ni ndugu yako? Kwa kuwa umerejea habari za maombi nani nitakujibu kwa maandiko:

Mathayo 19 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁵ ..... Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?

Maandiko hayajawahi kesema mke ni ndugu, bali mke wako ni WEWE!! Ninyi ni mtu mmoja, hivyo upoamini ndugu kuluko mkeo ni sawa na kujichukia na kujidharau mwenyewe. Ka hiyo hao ndugu hawabadiliki? Unamdharau mwenza wako anayeitunza afya yako ili upate nguvu za kutafutaahizo mali? Unambeza mkeo ambaye huyo ndiye anayekuzaliwa watoto na kukutengenezea familia? Ni heri basi ungezaa na hao ndugu zako ujenge nao ukoo.

Badilika sasa, vinginevyo ndoa itakushinda. Acha kabosa akili mbovu ya kumuona mkeo ni adui, kwqni unalolitamani ndilo hilo hilo litakuwa sehemu ya maosha yako. Be a man, a true husband.

Umeua bro,mwisho wa mjadara.
 
Wanaume nisikilize mimi, ukikutana na mwanamke mzuri muoe zaa nae watoto jenga familia pamoja naye.
Anaweza kuwa rafiki yako bora, msiri wako, mfanya biashara wako mshirika.

Na Unaweza kumuona kama mshirika wako wa karibu kwenye maombi pindi utakapomua kwani wanandoa huanza kufanana wakidumu pamoja.

Lakini usisahau nguvu iliyowaunganisha inaweza kuingia kutu kulingana na muda na kubadilika kwa moyo.
Mke wako sio ndugu yako wa damu na upendo wake unaweza kubadilika kuwa chuki ndani ya usiku mmoja.

Nisikilize mimi mpendwa kaka yangu, kwenye Wakati wa mahaba, kwenye kilele cha mafanikio yako, mkumbuke kaka yako aliesimama na wewe wakati haupo imara na umkumbuke dada yako aliekusafisha wakati ukiumwa sana.

Wakumbuke pia waliotumia muda wao kukuambia usitupe maji ya baridi kwenye mgongo wako, mikono yako na kukuandalia maji moto yaliyoilea ngozi yako.

Usiwafungie milango watoto wanapokuja mbele ya uzio wako wakiwa na miguu yenye vumbi na nguo zilizochanika wakitaka msaada wako.

Usizibe pua yako ikiwa wananuka harufu mbaya, usizibe masikio yako ili usisikie matumbo yao yakiunguruma kutokana na kukosa shibe.

Wakaribishe kwa mikono mikunjufu fungua milango yako waite wale juu ya meza yako na watendee kadri ungependa utendewe.

Yajayo ni kama upepo yanaweza kuwa hayatabiriki kabisa unaweza ukajikuta upo kama ayubu wa kwenye biblia ukiwa mtupu mwenyewe kwenye kisiwa cha matatizo.

Dada yako aliyekuokota ukiwa unaumwa hujiwezi Kama mtoto asiye na matumaini atakutafuta akusaidie tena.

Ndugu yako katakushika mkono katika mapito yako yote kwakuwa nguvu iliyowaunganisha kwenye damu itazongwa na upepo lakini kamwe haiwezi kutenganishwa.

Peter Mwaihola
Elvinah Obuya, The Standard Kenya.

View attachment 2724940
Bango lako halina faida kwa sababu ndoa ni kampuni ambayo kila mtu ana namna yake ya kuendesha punguza hasira,mihemko na chuki
 
Back
Top Bottom