Nisikilize: Mkeo si ndugu yako

Nisikilize: Mkeo si ndugu yako

Walikuwaga ndugu wa zamani sio hawa wa leo wanaotamani wote tuwe masikini nikipata basi visirani huanza.

Nitampenda nitamjali nitamthamini nitamuamini nitakayemuweka ndani ila sio ndugu hivyo itoshe kusema niko tayari kusalitiwa na kutengwa na mtoto wa mama mkwe ila sio ndugu sababu hawanipi changamoto za kusonga mbele ila wivu majungu na unafiki tu.

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Kweli mkuu, sisi majobless tunachekwa mpaka na ndugu wa damu kabisa. Nikioa nitamfanya kama ndugu yangu, tukitengana maana hili lipo nitaoa tena naye nitampenda kama ndugu yangu maana nikizeeka nitakuwa na mke wangu. Ndugu wa sahvi hamna kitu hasa kama unapitia shida.
 
Mke sio Ndugu yako Kwa sababu ni zaidi ya Ndugu.
Mkeo ndiye Mwanadamu pekee ambaye alikuwa kiapo kukupenda japo sio Ndugu yako.

Wakati Ndugu zako wakisimama na familia zao. Mkeo ndiye atasimama na wewe.

Wakati Ndugu zako wakiwatelekeza Watoto wako. Mkeo ndiye atakayewatunza.

Kuhusu kukengeuka Kwa mke hata Ndugu zako wanaweza kukengeuka.
Huwezi mpima MKE Kwa mzani wa kukengeuka.

Ndugu zako haohao ndio wanauwezo WA kuwadhulumu Watoto wako Mali pale utakapokufa.

Ndugu zako haohao ndio wanaweza kukuloga au kuloga Watoto wako ili wabaki kuwa na Maisha Duni.

Mkeo sio Ndugu yako, Ila ni zaidi ya Ndugu.

Mkigombana na Ndugu au na mzazi unaweza ukalala na Kupata usingizi kabisa, na chakula ukala ukashiba.
Lakini gombana na Mkeo uone hicho chakula au usingizi kama utaupata.

Hapa unazungumzia Mapenzi na upendo wa Mume na Mke.
nje ya mada kidogo naomba kuchombeza;KUONDOKEWA YANI KUFIWA NA MWENZI WA MAISHA ULIEMPENDA INAUMA SANA KULIKO MZAZI?
 
Ungeanza kwa kutoa sababu kwa nini tukusikilize wewe na sio Mwenyezi Mungu. Una hekima ipi kumzidi Mungu?

Kiwani nani alikudanganya mkeo ni ndugu yako? Kwa kuwa umerejea habari za maombi nani nitakujibu kwa maandiko:

Mathayo 19 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁵ ..... Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?

Maandiko hayajawahi kesema mke ni ndugu, bali mke wako ni WEWE!! Ninyi ni mtu mmoja, hivyo upoamini ndugu kuluko mkeo ni sawa na kujichukia na kujidharau mwenyewe. Ka hiyo hao ndugu hawabadiliki? Unamdharau mwenza wako anayeitunza afya yako ili upate nguvu za kutafutaahizo mali? Unambeza mkeo ambaye huyo ndiye anayekuzaliwa watoto na kukutengenezea familia? Ni heri basi ungezaa na hao ndugu zako ujenge nao ukoo.

Badilika sasa, vinginevyo ndoa itakushinda. Acha kabosa akili mbovu ya kumuona mkeo ni adui, kwqni unalolitamani ndilo hilo hilo litakuwa sehemu ya maosha yako. Be a man, a true husband.
Kama mwili mmoja kwa maana uliyotaka tuiamini. Mbona mmoja akifa mwingine hafi? Au hazikwi na mwenzake?
 
Eti hivi ndio vichwa vya familia🙆🙆🙆🙆
Nyie mafurushi mko busy kusambaza chuki then mambo yakibackfire mnamtafuta mchawi!!

Wanawake eeeh mume sio ndugu yako.
 
Back
Top Bottom