Tunza mahusiano yako hivi kama utaweza lakini

Man Middo tz

Senior Member
Sep 9, 2020
154
230
MAZUNGUMZO:

Ongea kuhusu mambo tofauti tofauti yanayohusu mahusiano yenu (Mazuri na mabaya, yanayo jenga na yanayo bomoa, yatakayo imarisha afya ya mahusino yanu au yatakayo dhofisha afya ya mahusiano yenu, kwa vyovyote vile ongea).

Jenga ukweli juu yenu, kuwa muwazi kwa mwenza wako na kuwa muamifu kwake.
Jitahidi usisahahu kuwa hapo kwajili yako na mwenza wako, Achana na yaliyopita yapite (ikihusisha historia ya mapenzi na mahusiano yako yaliyopita, huna haja ya kumtajataja mpenzi wako wa zamani mbele ya mpenz wako wa sasa, unadhoofu afya ya mapenzi yenu).

Jua kuwa mikwaruzanio na migangano ni kawaida na huwezi kuiepuka (pakaapo majembe mawili lazima yagongane lakini sio sababu ya kuyatoa yalipo).

Jua kuwa huwezi kuwa na furaha muda wote, usitaraji mabadiliko katika tabia au jambo bila msingi wa mabadiliko (Usijisemee kuwa atakuja kubadilika tukifunga ndoa au tukishapata mtoto, hapana kama unaweza kumbadilisha sasahivi basi fanya hivyo)

Ikubali hali yako na mazingira yaliyopo, mkubali mwenza wako jinsi alivyo na jengeni msingi wa kuwa marafiki (Mfanye mwenza wako kuwa rafiki) pendaneni, onyeshaneni mapenzi yasiyo na kikomo, chukua time yako mshike mkono mwenza wako na umwambie.

“Nitakushika mkono wako katika magumu na furaha katika maisha yetu” na mwingine ajibu hivi.

“Ndio maana nakupenda na sihitaji nikupoteze kwasababu maisha yangu yamekuwa bora tangu nilipokupata”

Fanya kadri ya uwezo wako juu ya mahusiano yako kama uliyenae ni sahihi au kama uliyenae anakubali ushauri na anaweza kubadilika.

Kuna wakati unajikuta unamwambia mpenzi wako maneno ambayo hujui yametoka wapi kama hivi.

“Mpenzi wangu (jina lake) unajua sijui kiukweli kipi nilichokua nasubiri lakini kila sekunde, kila dakika , kila saa na kila wakati nikiwa na wewe NAHISI KILA KITU NILICHOKUA NAKISUBIRI”

Mungu akubariki wewe unaesoma mahusiano yako yawe japo kwa 70% kama hivi, kama hujampata basi umpate mwenye kujua thamani yako na yake katika mapenzi.

kama upo kwenye mahusiano lakini hakuana viashiria vya mabadiliko na huna furaha basi Mungu akubariki na akuruzuku furaha na kuifungua milango ya ufahamu ya mwenza wako aje kutambua kipi afanye na kipi asifanye.

Nukuu na Man Middo “Moja ya kosa kubwa tufanyalo wanaume ni kumpa mwanaume mwenzako nafasi ya kumfanya mwanamke wako atabasamu.”

Kheri ya Christmas na mwaka mpya.

Imeandikwa na Man Middo Tz
1671883567711.jpg
 
Now hakuna mapenzi hicho ndo kitu nnachoamini mimi tafuta hela ukiwa na hamu nunua huduma siku zipite nimegundua mpenzi wangu anajiuza wakati niko nae ndan
 
Back
Top Bottom