Nisikilize: Mkeo si ndugu yako

Nisikilize: Mkeo si ndugu yako

Baada ya Mama yako aliyekuzaa ndugu wanaofatia ni Watoto zako.

Hao watoto wanapatikana kupitia Mke utakayemuoa.

Kama Mke amekuzalia Watoto kwanini usimuamini.

Ni mara mia kumwamini Mkeo kuliko ndugu.

Wakina Marehemu Mengi walitafuta pamoja na Mkewe hadi kufikia utajiri waliokuwa nao.

Kuna watu wengi wamekuwa -disappointed na ndugu zao kuliko Wake.

Tusisahau kumshirikisha Mungu kwenye kila hatua.
 
tena hao ndugu wa zamani walikuwa n busara sana, wasingekubali wao ndio uwaweke mbele badala ya mkeo. Ndugu anayeshabikia haya hana akiki kabisa.
Ungeanza kwa kutoa sababu kwa nini tukusikilize wewe na sio Mwenyezi Mungu. Una hekima ipi kumzidi Mungu?

Kiwani nani alikudanganya mkeo ni ndugu yako? Kwa kuwa umerejea habari za maombi nani nitakujibu kwa maandiko:

Mathayo 19 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁵ ..... Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?

Maandiko hayajawahi kesema mke ni ndugu, bali mke wako ni WEWE!! Ninyi ni mtu mmoja, hivyo upoamini ndugu kuluko mkeo ni sawa na kujichukia na kujidharau mwenyewe. Ka hiyo hao ndugu hawabadiliki? Unamdharau mwenza wako anayeitunza afya yako ili upate nguvu za kutafutaahizo mali? Unambeza mkeo ambaye huyo ndiye anayekuzaliwa watoto na kukutengenezea familia? Ni heri basi ungezaa na hao ndugu zako ujenge nao ukoo.

Badilika sasa, vinginevyo ndoa itakushinda. Acha kabosa akili mbovu ya kumuona mkeo ni adui, kwqni unalolitamani ndilo hilo hilo litakuwa sehemu ya maosha yako. Be a man, a true husband.
nakubaliana na wewe 100%, lakini hoja mada kama izi za kumwona mke sio sehemu mwili wako mume na msaidizi wako, zinaibuka kwa kasi sababu ya yanayoendelea na tuyaonayo kwenye ndoa za siku izi.
 
🤣🤣 Kwahiyo ngoma droo
Hakuna kuamini asiye damu yako
Kila munu Ave na kwao🤣🤣🤣
Mume na Mke ni zaidi ya damu. Ndoa ambayo ina baraka ya Mungu hufanya mume na mke kuwa mwili mmoja.. mke anakuwa ndani ya mume na mume anakuwa ndani ya mume.. Isipokuwa wengi hatuna elimu ya ndoa ya ndani kabisa.. kama ukiwa na elimu ya ndoa kwa kina chako.. hutoweza sema mke au mume sio ndugu yako.. mkisha kuwa mke na mume nyie ni zaidi ya ndugu..
 
Ungeanza kwa kutoa sababu kwa nini tukusikilize wewe na sio Mwenyezi Mungu. Una hekima ipi kumzidi Mungu?

Kiwani nani alikudanganya mkeo ni ndugu yako? Kwa kuwa umerejea habari za maombi nani nitakujibu kwa maandiko:

Mathayo 19 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁵ ..... Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?

Maandiko hayajawahi kesema mke ni ndugu, bali mke wako ni WEWE!! Ninyi ni mtu mmoja, hivyo upoamini ndugu kuluko mkeo ni sawa na kujichukia na kujidharau mwenyewe. Ka hiyo hao ndugu hawabadiliki? Unamdharau mwenza wako anayeitunza afya yako ili upate nguvu za kutafutaahizo mali? Unambeza mkeo ambaye huyo ndiye anayekuzaliwa watoto na kukutengenezea familia? Ni heri basi ungezaa na hao ndugu zako ujenge nao ukoo.

Badilika sasa, vinginevyo ndoa itakushinda. Acha kabosa akili mbovu ya kumuona mkeo ni adui, kwqni unalolitamani ndilo hilo hilo litakuwa sehemu ya maosha yako. Be a man, a true husband.
This is madini sana.

Unajua kuna siku nikajiuliza hivi ni kwa nini waislamu wanasema ndoa ni nusu ya dini?

Nikagundua asee ni kweli kabisa maana onaa huu ukweli: Hao ndugu wa damu ulio nao hata ukiwapenda unatimiza wajibu wako kama ndugu. Watoto wako ukifanikiwa kuwapenda basi unatimiza wajibu kama mzazi. Wazazi wako ukiwatunza pia unatimiza wajibu kama mtoto. Watoto wa mtaani ukiwalea basi unatimiza wajibu kama mwananchi labda etc etc

Lakini...

Huyo mwenza wako mahsusi huyo kumpenda kwa namna hiyo ni maamuzi umefanya. Ndoa ni muungano wa hiyari baina ya wawili walioamua kupendana wao wenyewe.

Kwa hiyo ukifanikiwa kuiishi ndoa kikamilifu unakuwa umejifunza kwa vitendo mambo mawili (au zaidi) makubwa nayo ni HIYARI na UPENDO. Pia wajibu, huduma, haki na huruma, kuwa na uwezo na kuutumia uwezo huo kwa faida ya mwenza pia. Asee ni nusu ya dini kwa kweli.

Wanaoelewa vizuri ndoa wanaendesha vizuri hata taasisi nyingine za kijamii na kiraia na mwishowe kimbingu.
 
Wanaume nisikilize mimi, ukikutana na mwanamke mzuri muoe zaa nae watoto jenga familia pamoja naye.
Anaweza kuwa rafiki yako bora, msiri wako, mfanya biashara wako mshirika.

Na Unaweza kumuona kama mshirika wako wa karibu kwenye maombi pindi utakapomua kwani wanandoa huanza kufanana wakidumu pamoja.

Lakini usisahau nguvu iliyowaunganisha inaweza kuingia kutu kulingana na muda na kubadilika kwa moyo.
Mke wako sio ndugu yako wa damu na upendo wake unaweza kubadilika kuwa chuki ndani ya usiku mmoja.

Nisikilize mimi mpendwa kaka yangu, kwenye Wakati wa mahaba, kwenye kilele cha mafanikio yako, mkumbuke kaka yako aliesimama na wewe wakati haupo imara na umkumbuke dada yako aliekusafisha wakati ukiumwa sana.

Wakumbuke pia waliotumia muda wao kukuambia usitupe maji ya baridi kwenye mgongo wako, mikono yako na kukuandalia maji moto yaliyoilea ngozi yako.

Usiwafungie milango watoto wanapokuja mbele ya uzio wako wakiwa na miguu yenye vumbi na nguo zilizochanika wakitaka msaada wako.

Usizibe pua yako ikiwa wananuka harufu mbaya, usizibe masikio yako ili usisikie matumbo yao yakiunguruma kutokana na kukosa shibe.

Wakaribishe kwa mikono mikunjufu fungua milango yako waite wale juu ya meza yako na watendee kadri ungependa utendewe.

Yajayo ni kama upepo yanaweza kuwa hayatabiriki kabisa unaweza ukajikuta upo kama ayubu wa kwenye biblia ukiwa mtupu mwenyewe kwenye kisiwa cha matatizo.

Dada yako aliyekuokota ukiwa unaumwa hujiwezi Kama mtoto asiye na matumaini atakutafuta akusaidie tena.

Ndugu yako katakushika mkono katika mapito yako yote kwakuwa nguvu iliyowaunganisha kwenye damu itazongwa na upepo lakini kamwe haiwezi kutenganishwa.

Peter Mwaihola
Elvinah Obuya, The Standard Kenya.

View attachment 2724940
Mume ataambatana na mke wake, pia mke ataambatana na mume wake.
Nani aliyekwambia Ndugu ndiyo wana gurantee?
Mkiamua kuoana hakikisheni mnatoshana.
 
Wanaume wengi wamepoteza dira kwenye ndoa zao sababu ya the so called ndugu. Mke ni zaidi ya ndugu. Mafanikio ya wanaume wengi yamekua reflected na wake zao zaidi ya ndugu unaowasema. So mke anabakia kua muhimu zaidi ya huo undugu ambao umetumia maneno mengi kuelezea
 
Walikuwaga ndugu wa zamani sio hawa wa leo wanaotamani wote tuwe masikini nikipata basi visirani uanza .

Nitampenda nitamjali nitamthamini nitamuamini nitakayemuweka ndani ila sio ndugu hivyo itoshe kusema niko tayari kusalitiwa na kutengwa na mtoto wa mama mkwe ila sio ndugu sababu hawanipi changamoto za kusonga mbele ila wivu majungu na unafiki tu .

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Undugu upo kwenye DNA. Huo haufutiki. Urafiki unafutika. Mke ni rafiki tu.
 
Wanaume nisikilize mimi, ukikutana na mwanamke mzuri muoe zaa nae watoto jenga familia pamoja naye.
Anaweza kuwa rafiki yako bora, msiri wako, mfanya biashara wako mshirika.
Na Unaweza kumuona kama mshirika wako wa karibu kwenye maombi pindi utakapomua kwani wanandoa huanza kufanana wakidumu pamoja.

Lakini usisahau nguvu iliyowaunganisha inaweza kuingia kutu kulingana na muda na kubadilika kwa moyo.
Mke wako sio ndugu yako wa damu na upendo wake unaweza kubadilika kuwa chuki ndani ya usiku mmoja.

Nisikilize mimi mpendwa kaka yangu, kwenye Wakati wa mahaba, kwenye kilele cha mafanikio yako, mkumbuke kaka yako aliesimama na wewe wakati haupo imara na umkumbuke dada yako aliekusafisha wakati ukiumwa sana.

Wakumbuke pia waliotumia muda wao kukuambia usitupe maji ya baridi kwenye mgongo wako, mikono yako na kukuandalia maji moto yaliyoilea ngozi yako.

Usiwafungie milango watoto wanapokuja mbele ya uzio wako wakiwa na miguu yenye vumbi na nguo zilizochanika wakitaka msaada wako.

Usizibe pua yako ikiwa wananuka harufu mbaya, usizibe masikio yako ili usisikie matumbo yao yakiunguruma kutokana na kukosa shibe.
Wakaribishe kwa mikono mikunjufu fungua milango yako waite wale juu ya meza yako na watendee kadri ungependa utendewe.

Yajayo ni kama upepo yanaweza kuwa hayatabiriki kabisa unaweza ukajikuta upo kama ayubu wa kwenye biblia ukiwa mtupu mwenyewe kwenye kisiwa cha matatizo.
Dada yako aliyekuokota ukiwa unaumwa hujiwezi Kama mtoto asiye na matumaini atakutafuta akusaidie tena.

Ndugu yako katakushika mkono katika mapito yako yote kwakuwa nguvu iliyowaunganisha kwenye damu itazongwa na upepo lakini kamwe haiwezi kutenganishwa.

Peter Mwaihola
Elvinah Obuya, The Standard Kenya.View attachment 2724940
Maisha hayana kanuni kwa hiyo itategemea na wanandoa au wanafamilia, wapo ambao wenzi wao ndo waliowatoa kwenye utumwa wa fikra na uchumi toka kwa ndugu zao na kuwafanya wajiamini na kujiyegemea na mwisho na hivyo kuwa na uchumi na maamuzi binafsi kwake mke ni kila kitu. Wapo ndugu lawama wao hawaoni jema kulalamika na kutaka kukushikia chini wamejaa chuki wao hawatataka ufanikiwe watataka uwe wa kuwasujudu na kuwatumia ,lakini mke mara zote anapambana bega kwa bega ili mfanikiwe na muwe na familia bora.

Shida ya hii kauli hasi inatokana na tabia au hulka za baadhi ya wanandoa ,kwa mfano baadhi ya wanaume wanajengwa na wake zao mpaka kuwa na mafanikio na wakifikia hapo wanaanza kuwadharau na kuwatendea ndivyo sivyo, mwanamke hawezi vumilia kuona kile alichopambania kinatapanywa na hapo atachukua hatua na kwa kuwa jamii hupenda kunyooshea vidole na mfumo dume mwanamke ataonekana ana makosa.

Wapo pia wanawake ambao wamejengwa na wanaume lakini wakifikia mafanikio wanabadilika na kuwaona wanaume zao washamba ,nk hapo mwanaume huenda alijinyima au kunyima wanandugu ili kujenga mwenza ambaye alifikiri atakuwa msaada katika familia yake lakini kumbe alimsaidia mpita njia.

Cha msingi, tuache kukurupuka wakati wa kutafuta wenza, unaweza fikiri umepata mtu wa kujenga nae maisha kumbe na yeye anafikiri kapata sponsor, mwisho wa siku akifikia malengo anatembea, na kwa wanaume siku zote tutambue wanawake wa nje ni wazuri, watamu, romantic kwa sababu hatuishi nao wala hawashiriki changamoto zetu za kila siku. Na tukiharibikiwa hawatakuwepo kushiriki anguko letu.
Tuwapende wenzi wetu, tuwaamini na kuwashirilisha katika masuala yale muhimu ya mustakabali wa maisha yetu, zaidi tuwe na mipaka ya kifamilia, dada, kaka, baba na mama nao wana familia zao na mipango yao, tushirikiane na kushirikisha yale ya jumla sio kuingilia katika maamuiz.
Wanaume nisikilize mimi, ukikutana na mwanamke mzuri muoe zaa nae watoto jenga familia pamoja naye.
Anaweza kuwa rafiki yako bora, msiri wako, mfanya biashara wako mshirika.
.

View attachment 2724940
 
Back
Top Bottom