nisaidieni wana JF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

nisaidieni wana JF

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kalunguine, Mar 26, 2011.

 1. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  waungwana! nilikuwa na mchumba,toka mwaka 2004,nikamtoa form four na sasa anamalizia degree ya education mwezi wa sita mwaka huu,mwaka jana mara tu baada ya kumlipia ada ya mwaka wa mwisho,kesho yake akani sms kuwa alikuwa hanipendi na alikuwa anataka tu asome! kijana nikaamua kuwa cool kwa kuwa nshapoteza pesa nyingi vibaya kwa huyu she,lakini katika masiku ya karibuni baada ya kupigika vibaya kwa mwanaume alokuwa nae eti sasa anataka kurudi kwangu na wakati hata pate yangu ya uchumba alishaitupa,na kamwe siwezi kumuamini tena,nifanyeje ndugu zangu
   
 2. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Duh,.
  Umewahi sikia wimbo unaitwa "stell" sina uhakika lakini?

  Jamaa kauza ng'ombe zake zote akampeleka mchumba wake kusomea udaktari Japan,siku anaenda kumpokea karudi na mtoto na pande la Mjapani!

  Anyway,msaidie tu!
  Usilipize kisasi,atleast kwa Mungu utakuwa umetenda jambo kubwa sana ila usimsaidie kama mke mtarajiwa maana hafai kuwa mke,...
  Fanya tu kama ulikuwa una msaidia mtu usiye mjua!

  Pole kaka
   
 3. donlucchese

  donlucchese JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 9,397
  Likes Received: 3,528
  Trophy Points: 280
  C alijifanya katema Big G kwa utamu wa karanga za kuonjeshwa? Wala ckushauri urudiane nae coz hana mapenz ya dhati alitaka aku2mie 2. Mpotezee
   
 4. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,807
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  mpige chini kama mwizi huyoo...
  kama unamsaidia msaidie kama rafiki...ila usiweke malengo naye hakufai huyo.
   
 5. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...follow your heart, msamehe lakini usirudiane nae.
   
 6. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #6
  Mar 26, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  dah .. pole saana! achana naye, tafuta mwengine
   
 7. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #7
  Mar 26, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ushauri mzuri Mbu

  Juzi alikuwa na wewe kwa sababu alijua ungemtimizia mahitaji yake

  Kaenda kapigika na mahitaji yameisha anarudi tena...ukishamtimizia keshokutwa anatimka tena....Kwa nini ujuimize na kujipa Pressure ya moyo...

  mwache atimke baba na muite tu vizuri kirafiki na umshauri kuwa maisha hayaendeshwi namna hiyo
   
 8. Kaka Mpendwa

  Kaka Mpendwa JF-Expert Member

  #8
  Mar 26, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 771
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  mkuu
  pole sana. kweli dunia ina mambo??

  Nakushauri umsamehe, umepoteza vingi juu yake, na zaidi anakujali sana tu. Inawezekana alipata mtu wa kumdanganya, ndio maana akafanya jambo la kijinga.

  Mpe nafasi nyingine. hakuna binadamu aliye sawa (perfect). wengine wanayafanya haya wakiwa ndani ya ndoa.. Lakini give her a chance..
  Ukimsamehe toka moyoni, Mungu ni mwema, atarekebisha uhusiano wenu..Kwenye mahusiano kuna mambo mengi sana, ukitaka kuchukua hatua kwa kila tukio, utakufa mapema.

  Wanadamu tuko hoi siku zote, pamoja na Mungu kutuma hata Mwanaye, lakini mambo bado sio mazuri kote misikitini na makanisani. MSAMEHE.

  Siafiki wala kuunga mkono ujinga wake huyo dada, isipokuwa wanadamu tunateleza sana, kama sio leo basi ni kesho. She is yours, unamjua vizuri sana na yeye vivyo.. Nakuhakikishia kuwa atakuwa na heshima kuliko wakati mwingine wowote..Mshirikishe Mungu katika uamuzi wake.

  thanks
   
 9. Esperance

  Esperance JF-Expert Member

  #9
  Mar 26, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 364
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole sana mkaka, je baada ya hapo ulianzisha mahusiano mengine? Unampenda kutoka moyoni huyo bibie wa zamani? Naweza kuchangia nikipata majibu ya hayo.
   
 10. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #10
  Mar 26, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Me naona amsamehe na amsapoti amalizie masomo yake ila hafai kuwa mke,amsaidie kiubinadamu tu
   
 11. Kaka Mpendwa

  Kaka Mpendwa JF-Expert Member

  #11
  Mar 26, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 771
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  karibu Kibiritingoma..

  natumaini ulipata msaada kwenye msaada wa kuacha ***o..

  all the best
   
 12. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #12
  Mar 26, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Rudia kusoma..amesema "baada ya kupigika kwa mwanaume aliyekua nae...."
  Nwyz unaweza kumsamehe ila kurudiana nae sikushauri!Alikutumia kusoma sasa anataka kukutumia kuweka maisha yake sawa!Ukijitosa uwe tayari kuambiwa tena ulikua hupendwi alitaka tu umwekee maisha yake sawa!
   
 13. Wazo Langu

  Wazo Langu JF-Expert Member

  #13
  Mar 26, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 1,344
  Likes Received: 519
  Trophy Points: 280
  Blue
  alichokuambia alimaanisha na hata ukiangalia alikuambia wakati ambao haitaji tena msaada wako.
  Ni wazi hakukupenda na baada ya kutimiza malengo akaondoka.
  HAKUPENDI!

  Red
  Ni ngumu kuishi na mtu ambaye mwenyewe unakiri huwezi kumuamini na pia aliwahi kukwambia hakupendi kwa dhati anafuata msaada wako tu.
  Sasa unapata ugumu gani kufanya maamuzi?
   
 14. Kaka Mpendwa

  Kaka Mpendwa JF-Expert Member

  #14
  Mar 26, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 771
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  maisha wakati mwingine hayaendi kwa formula kama hivyo..
  wote tunazifahamu akili za wanafunzi wakiwa vyuoni..kuna peer pressure, na mengine kama mob-psychology!

  Simtetei huyo dada, ila kama huyo binti ameona kosa lake na anaomba msamaha, mie ninaona AMPE nafasi nyingine.
   
 15. Kaka Mpendwa

  Kaka Mpendwa JF-Expert Member

  #15
  Mar 26, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 771
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  nadhani mleta thread hajatamka kama ni binti alimuomba amlipie ada, au aliamua kuwekeza tu kwa kufikiri mambo yatakuwa mazuri mbeleni..kwa hiyo huwezi kusema kama binti alikuwa anamtumia..inabidi mleta mada aje aweke sawa kuhusu hili..

  mambo ya mapenzi ni magumu, ni muhimu yajengwe katika misingi ya kusameheana.. wametoka mbali since 2004, sio mchezo
   
 16. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #16
  Mar 26, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,276
  Trophy Points: 280
  Atakuumiza mimi nishayaona na kunikuta mwambie ukweli mimi nina gf wangu ajanikosea hivyo sitopenda kumuumiza mtu asiyenitendea kosa lazima itamtachi zaidi kama unamtu mwingine unhisi unampenda naye anakupenda mwambie tukio zima hii itakusaidia wewe kujikuta umekabwa na penzi la ulaghai!!
   
 17. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #17
  Mar 26, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  "akanitumia sms kwamba ALIKUA ANATAKA TU ASOME" umeona hayo maneno?Yana maana gani?Sijakurupuka kujibu!Na kutoka kwao mbali hamna aliyesema ni mchezo.
   
 18. Kaka Mpendwa

  Kaka Mpendwa JF-Expert Member

  #18
  Mar 26, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 771
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  ok, nimekupata..

  lakini nilitamani kujua makubaliano yao ya kulipiana ada yaliaanzaje??
  Kumbuka walishavishana hadi pete ya uchumba.
   
 19. Esperance

  Esperance JF-Expert Member

  #19
  Mar 26, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 364
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  swali ni kwa mkaka baada ya hayo alianzisha uhusiano mwingine?? Yeye mkaka.
   
 20. Esperance

  Esperance JF-Expert Member

  #20
  Mar 26, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 364
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asante, jana nitoa thread ya shukran naona imehamishiwa sijui jukwaa la wazee. Its almost half done, tunamsubiri mume wangu arudi tu.
   
Loading...