nisaidieni wana JF

Msamehe amejifunza tayari mbona wadada wengi tu wanawasaamehe vijana baada ya kutendwa sana tu?Angalia,chunguza kama kabadilika msamehe tu tuliagizwa tusamehe saba mara sabini ndugu yangu
 
Gaga wadada ni warahisi sana kusamehe sio kama wanaume. Huyo kama tayari yuko kwenye uhusiano mwingine atamuumiza bure huyo mdada mwingine.
 
Samehe 2 mara 1. Kwasababu kashajua kosa lake we msamehe tu atajirekebisha.
Huyo amedanganyika tu kidogo..
 
waungwana! nilikuwa na mchumba,toka mwaka 2004,nikamtoa form four na sasa anamalizia degree ya education mwezi wa sita mwaka huu,mwaka jana mara tu baada ya kumlipia ada ya mwaka wa mwisho,kesho yake akani sms kuwa alikuwa hanipendi na alikuwa anataka tu asome! kijana nikaamua kuwa cool kwa kuwa nshapoteza pesa nyingi vibaya kwa huyu she,lakini katika masiku ya karibuni baada ya kupigika vibaya kwa mwanaume alokuwa nae eti sasa anataka kurudi kwangu na wakati hata pate yangu ya uchumba alishaitupa,na kamwe siwezi kumuamini tena,nifanyeje ndugu zangu

Kimbia usiangalie nyuma! Ndo zake huyo,,, hata mimi alinifanya hivyohivyo.........kwangu nishamtimua,,,,
 
mkuu
pole sana. kweli dunia ina mambo??

Nakushauri umsamehe, umepoteza vingi juu yake, na zaidi anakujali sana tu. Inawezekana alipata mtu wa kumdanganya, ndio maana akafanya jambo la kijinga.

Mpe nafasi nyingine. hakuna binadamu aliye sawa (perfect). wengine wanayafanya haya wakiwa ndani ya ndoa.. Lakini give her a chance..
Ukimsamehe toka moyoni, Mungu ni mwema, atarekebisha uhusiano wenu..Kwenye mahusiano kuna mambo mengi sana, ukitaka kuchukua hatua kwa kila tukio, utakufa mapema.

Wanadamu tuko hoi siku zote, pamoja na Mungu kutuma hata Mwanaye, lakini mambo bado sio mazuri kote misikitini na makanisani. MSAMEHE.

Siafiki wala kuunga mkono ujinga wake huyo dada, isipokuwa wanadamu tunateleza sana, kama sio leo basi ni kesho. She is yours, unamjua vizuri sana na yeye vivyo.. Nakuhakikishia kuwa atakuwa na heshima kuliko wakati mwingine wowote..Mshirikishe Mungu katika uamuzi wake.

thanks

Ubarikiwe.
 
Dah, labda ni mimi tu au..lakini sijawahi ku-imagine kumlipia demu ada ya shule au kitu chochote cha dizaini hiyo. Ukifanya mambo kama hayo mambo yakienda kombo ndio inakuaga kama hivi. Cha kufanya tafuta kitu cha nguvu achana na huyo sunguramatope.
 
"imeandikwa mke mwema mtu hupewa na Bwana bali fedha na dhahabu hupewa na babaye" kwa upande wangu huyo si mke mwema!!
 
Dah, labda ni mimi tu au..lakini sijawahi ku-imagine kumlipia demu ada ya shule au kitu chochote cha dizaini hiyo. Ukifanya mambo kama hayo mambo yakienda kombo ndio inakuaga kama hivi. Cha kufanya tafuta kitu cha nguvu achana na huyo sunguramatope.
well said sijui wakaka munaingiaje kwenye mtego huu wa kutusomesha.Mimi nilishawaambia kaka zangu wafanye yote ila sio kumsomesha mwanamke university.
 
...follow your heart, msamehe lakini usirudiane nae.
good point, follow your haert.
but one more point, if you real want to start new chapter, make sure, you close all other pages, acha everything about her, especailly mawasiliano, cause, kama utamasamhe ,( na unapaswa kufayna hiyo), ila ukalegea na kuwa na mwasiliana ya hapa na pale, friend i'm telling you ( u seem to still love her) atakuteka, na kukurudihsa nyuma.

check out.
God bless you
 
well said sijui wakaka munaingiaje kwenye mtego huu wa kutusomesha.Mimi nilishawaambia kaka zangu wafanye yote ila sio kumsomesha mwanamke university.

Kumsomesha mtu ambaye una uhakika naye sio kitu kibaya..mathalan mke au mchumbako anayeelekeaelekea, maana kwa namna moja au nyingine unakua una uhakika na unapowekeza bi mkubwa.
 
well said sijui wakaka munaingiaje kwenye mtego huu wa kutusomesha.Mimi nilishawaambia kaka zangu wafanye yote ila sio kumsomesha mwanamke university.

Jamani si wanawaendeleza watarajiwa wao!!Ndivyo wanavyoamini anyway..mpako mambo yanapogeuka ndo wanajua walikua mtaji tu na faida haiwahusu!
 
waungwana! nilikuwa na mchumba,toka mwaka 2004,nikamtoa form four na sasa anamalizia degree ya education mwezi wa sita mwaka huu,mwaka jana mara tu baada ya kumlipia ada ya mwaka wa mwisho,kesho yake akani sms kuwa alikuwa hanipendi na alikuwa anataka tu asome! kijana nikaamua kuwa cool kwa kuwa nshapoteza pesa nyingi vibaya kwa huyu she,lakini katika masiku ya karibuni baada ya kupigika vibaya kwa mwanaume alokuwa nae eti sasa anataka kurudi kwangu na wakati hata pate yangu ya uchumba alishaitupa,na kamwe siwezi kumuamini tena,nifanyeje ndugu zangu
kama ulifanikiwa kumuacha na kumsahau shukuru mungu kaka mana kumuacha umpendae hata kama hujamlipia chochote ni kazi nguvu yenye maumivu, nakushauri muepuke tu ili ubaki na aman moyoni.
 
Mpigie mahesabu ya gharama yote uliyotoa kumsomesha na mara apatapo kazi aanze kurejesha kidogo kidogo kwa kumkata ktk mshahara wake.Vinginevyo utakuwa umeliwa.Nanyi wanaume wengine mnapenda kuingia kichwa kichwa unaingia migharama yote hivyo kwani uko peke yako au uko akilini mwa m dada.Wajifanya unatupa hela wakati labda ndugu zako hata chumvi hawana.any way umepata funzo
 
duuuh ananikumbusha wimbo wa 20% tamaa mbaya... Mkuu jiweke pembeni bana ya nini malumbano? Muulize anahitaji kuwa na wewe au anahitaji msaada amalizie masomo yake.. Hilo la kuwa na wewe sikushauri hata kidogo, hilo ni dege lisiloliwa ila kama uko njema endelea kumsapoti amalize masomo yake
 
Back
Top Bottom