bless on
JF-Expert Member
- May 22, 2026
- 705
- 1,659
Zamani, mafuta yote ya Iran yalikuwa mikononi mwa kampuni ya Waingereza Leo inaitwa BP. Waingereza walikuwa wanachukua faida kubwa, huku Wairani wenyewe wakiambulia patashika na umaskini.
Mwaka 1951, akatokea mshua mmoja anaitwa Mohammad Mossadegh, akachaguliwa kuwa Waziri Mkuu. Huyu mzee alikuwa na msimamo kinoma; akasema, Haiwezekani dhahabu hii nyeusi iwanufaishe wageni huku wanangu wanakufa njaa. Akapitisha sheria ya kutaifisha mafuta yote yawe mali ya serikali ya Iran.
Waingereza waliumia roho vibaya sana. Walijaribu kumwekea vikwazo vya kiuchumi ili asiuze mafuta, lakini mzee akakaza fuvu. Walipoona mzee hageuki, wakaenda kumlilia mdogo wao, Marekani.
Wakati huo kulikuwa na ile Cold War kati ya Marekani na Urusi. Waingereza wakawadanganya Wamarekani Oya, huyu Mossadegh anataka kuwa mshikaji wa Warusi, tusipomtoa, Iran itakuwa upande wa Urusi. Wamarekani wakashtuka, wakasema, Hapana, huyu mzee lazima tumpige chini.
CIA wakamtuma mnyama mmoja anaitwa Kermit Roosevelt aingie Tehran. Jamaa aliingia na mabunda ya dola.
Alilipa magazeti yaandike habari za uongo kwamba Mossadegh ni dikteta na anachukia Uislamu.
Walikodisha Wahuni, magenge ya mtaani yafanye vurugu, yachome misikiti na majengo, halafu wasingizie kuwa ni wafuasi wa Mossadegh ndio wanafanya hivyo.
Walimshawishi Shah wa Iran amfukuze Mossadegh, ingawa kisheria Shah hakuwa na hiyo nguvu.
Mara ya kwanza mchongo ulikwama, Mossadegh akashtukia. Shah akakimbia nchi kwa uoga. Lakini Kermit hakukata tamaa; alimwaga mpunga mwingine mtaani. Siku chache baadaye, kukatokea maandamano makubwa yaliyojaa watu waliohongwa na wanajeshi walionunuliwa.
Wakaivamia nyumba ya Mossadegh kwa vifaru. Mzee akaona isiwe tabu, akajisalimisha ili kuzuia damu kumwagika zaidi.
Shah akarudi nchini kwa mbwembwe na akawa "kibaraka" wa Marekani kwa miaka 25 iliyofuata. Aliongoza kwa mkono wa chuma, huku CIA wakimsaidia kuunda shirika la kijasusi la kikatili liitwalo SAVAK la kutesa wapinzani.
Wairani hawakusahau hili dharau. Hasira ilizidi kupanda moyoni mwao kwa miaka yote hiyo. Mwaka 1979, zile hasira zikalipuka kwenye Mapinduzi ya Kiislamu Wakamtimua Shah.
Marekani na Uingereza waliharibu demokrasia ya Iran kwa ajili ya mafuta, na hiyo ndiyo sababu mpaka leo Iran haiamini nchi za Magharibi hata kidogo.