Nipashe, Kulikoni , Gurdian Kulikoni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nipashe, Kulikoni , Gurdian Kulikoni?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Malaria Sugu, Jul 9, 2009.

 1. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #1
  Jul 9, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wengi Tunaufatilia Mjadala wa mahakama ya kadhi kupitia magazeti yetu na redio zetu.
  Tz Daima, Mwanahalisi, Mwananchi,Majira,Habarileo, Raiamwema na redio kama vile tbc1 na nyengine nyingi. Lakini hadi leo tangu sakata hili lianze tena Bungeni sijasikia wala kuona habari hiyo katika nipashe na kulikoni. sababu za msingi bado sijazijua lkn waandishi na watangazaji wa vyombo hivyo wakifuatilia karibu habari hizo katika conference pale kinondoni Bakwata na Bungeni na hata katika vyanzo vyengine. Jee kulikoni ukimya huo kwani swala sensitive? Kulikoni wakuu.
  mzee wa hojanatoa hoja
   
 2. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #2
  Jul 9, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  '..Mimi niko njia panda,
  ukweli narandaranda,
  nangoja pijo kupanda,
  kunipeleka Mpanda...'
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Jul 9, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Habari za uhakika nilizopata kutoka kwa watu ninaowafahamu katika newsroom ya IPP ni kwamba huu ni msimamo uliowekwa rasmi wa uongozi wa magazeti hayo – mkwamba habari, makala za mjadala nk kuhusu issue ya Kadhi yasiandikwe kwenye magazeti hayo.

  Sijui kuhusu electronic media – yaani ITV na Radio One.
   
 4. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #4
  Jul 9, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huo ni mtizamo Finyu kwa IPP media wakati Tz hasa wasomaji wake ni pia waislam jee hawanyimi haki waislam kupata habri kama hizo?
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Jul 9, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,007
  Trophy Points: 280

  hiyo pijo itapita kwenye barabara gani??
  Nakushauri uvue matairi itembelee habu juu ya reli.
  Ila jihadhari na wafanyabiashara wa vyuma chakavu, hachelewi kufungua mataruma
   
 6. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #6
  Jul 9, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  unapokuwa na chombo cha habari kama gazeti si lazima uandike kila kitu. Mhariri anauhuru wa kuamua kutoa habari gani na kuacha ipi. So, kama msimamo wa IPP ni kuto andika habari za kadhi is okey. Well, huko nyuma, IPP imeshapata misukosuko mingi among them ni baadhi ya vikundi vya waislam kutangaza/kuwaangiza waislam wasisome au kuangalia media za IPP. Pia tunapaswa kuzingatia kwamba vyombo vya habari ni biashara pia, so, kama kunajambo linatishia biashara yako unaachana nalo.
   
 7. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #7
  Jul 9, 2009
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  sijajua unaongelea magazeti ya lini, lakini guardian liliandika vizuri suala hili sikumbuki gazeti la lini lakini nitacross check ili niweke kumbukumbu sahihi, tena mpaka nikahisi labda ni kwa sababu Mzee amekuwa anatoa sana support kwa bakwata........
   
 8. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #8
  Jul 9, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,145
  Likes Received: 1,238
  Trophy Points: 280
  Mtazamowangu.....Tatizo la hawa watu wakishakuwa na mwelekeo HASI/Kinyume na kitu fulani watajaribu kuleta hata vitu visivyokuwa na msingi ili kuhalalisha mitizamo yao. Hakika ulichosema ni kweli magazeti haya yameripoti habari ya kadhi tena sana tu. Au Huyu ndugu alitaka yaripoti kuanzia ukurasa wa 1 hadi wa mwisho? Acheni kutafuta uchochezi usiokuwa na msingi.....oh mara tususie bidhaa za IPP na visingizio kibao. Hata hivyo mhariri anaweza kuamua kuripoti ama kuacha kuiripoti habari kulingana na uzito na nafasi iliyopo kwa siku ile.

  Acheni kupandikiza chuki zisizokuwa na msingi kwa Magazeti ya IPP Media,
   
 9. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #9
  Jul 9, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,894
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Nziku and counterpunch,
  Very good observation. Naungana nanyi kuwa ni msimamo wa kampuni. Mfano hata siku moja sijawahi kuona ITV vile vipindi vya kikristo vya kakobe vya SAA YA MAAJABU, vingine vya SAA YA ..... huwezi kuviona ITV lakini channels nyingine vipo sana kama channel 10 star tv etc. So tuheshimu msimamo wa hivi vyombo. Kama unacho chako wewe ongelea kadhi au andika the whole page so long haukiuki maadili ya uandishi. So tu me no problem.
   
 10. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #10
  Jul 9, 2009
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Nimewaheshimu IPP the way wanavyo iandika ishu hii. Mwananchi sasa hivi ndo habari yao tu!! Kwa hiyo hao wanaolalamika kuikosa IPP wanunue tu Mwananchi na magazeti dada yake. Si lazima kila siku IPP waandike juu ya ishu hii. Hapa wameonesha profesionalism ya hali ya juu.
   
 11. idumu

  idumu Member

  #11
  Jul 9, 2009
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  SI lazima watoe habari kama hiyo, Ni upuuzi maana HIKI kitu hakipo kwenye katiba labda wafanye ammendments
   
 12. M

  Masatu JF-Expert Member

  #12
  Jul 9, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  This is classic! nimecheka hata!
   
 13. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #13
  Jul 9, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Je, vipi kuhusu ile habari ya klabu chetu cha Yanga siku kilipoingia mkataba wa udhamini na mfanyibiashara Yusuf Manji, ilikuwaje vyombo vya habari vya IPP havikuandika, kutangaza wala kuonesha habari ile?
   
 14. E

  Endaku's JF-Expert Member

  #14
  Jul 9, 2009
  Joined: May 25, 2007
  Messages: 322
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Upeo na uelewa wa mambo ni tatizo Binafsi !! Kazi kweli kweli ,./.
   
 15. S

  Sir Leem JF-Expert Member

  #15
  Jul 9, 2009
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 564
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Ni kweli ITV huwa hawana sana vipindi vya maajabu sana sana wao wanaleta nyimbo za Injili kila siku asubuhi kwenye chanel 5!
   
 16. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #16
  Jul 9, 2009
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hoja hii inalenga kujenga uhasama kati ya wanajamii ya Kiislamu na vyombo vya IPP. Hakuna ukweli wowote katika jambo hili. Muda mfupi uliopita nimenunua gazeti la KULIKONI na kusoma tahariri nzuri kuhusu suala la Mahakama ya Kadhi, yenye kichwa kisemacho: 'Mahakama ya Kadhi isitutenganishe'. Unataka nini zaidi wewe unayejiita MzeewaHoja? Kama alivyosema mchangiaji mwingine hapo juu, magazeti hayo yaliyotajwa yamekuwa yakiandika habari za Mahakama ya Kadhi kama magazeti mengine. Ulipaswa kufanya research kwanza kabla ya kuja na hoja hii isiyo na tija na yenye lengo la kupandikiza chuki. Tuwe waangalifu sana na masuala haya sensitive yanahohusu dini. Usiwe kama yule mbunge aliyemwaga sumu bungeni wakati akichangia kwa jazba za ki-mujahedeen kulishambulia Kanisa Katoliki bila hoja ya maana.
   
 17. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #17
  Jul 9, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kumbe mchangiaji wa Juu hapo unachuki? unajua mujahidina ni cheo kwa Mungu na ataingia peponi. ungalisema mnafiki ingalikuwa kosa. Hongera Msambya. mbona husemi Vertican Imepitishwa Bungeni jee waliopiisha Bungeni walikuwa nao nani?
   
 18. k

  kisarawe New Member

  #18
  Jul 9, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nafikiri huyo alietuma hii meseji ana tatizo lake binafsi, kwani Ipp kama IPP ina uhuru wa kuandika kile inachofikiria ni sawa,
  Ipp ina waislamu na wakristu wengi, pia wapagani

  kwa hio nafikiri tuwe serious wakati tunaleta hoja, si utoto.
   
 19. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #19
  Jul 9, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  ebwana wee yaaani magazeti yote yawe yanaandika habari moja? na tv & redio zitangaze habari mamoja? tembea uone nchi zingine magazeti/media zinavyofanya kazi.
   
 20. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #20
  Jul 9, 2009
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Haya masuala ya imani za Kidini tusipende sana kuyajadili humu. Historia ya nchi zilizoingia kwenye migogoro ya kidini inaonyesha ilianza mijadala ya aina hii na baadaye kulipuka. Tunafahamu baadhi ya wanajamii wenzetu wana jazba sana. Haifai!
   
Loading...