Cha msingi search kwenye laptop unayotaka kununua angalia specificationa bila kujali ni dell au hp ama lenovo, Njia rahisi ni kuminya ile button ya start / window then search hili neno DXDIAG Anza kucheki ipi iko poa, Ukiona umechanganyikiwa wewe orodhesha specs ziweke humu tukudadavulue...Cha msingi nakushauri ucheki processor na ussishie tu kucheki kwamba ni core i3, i5 au i7...andika na model kabisa mfani core i5 6500u, core i5 7200u, .n.k
Mkuu naomba tafsiri ya Maelezo haya kwani kuna laptop nimeinunua juzi na bado ipo ndani ya warranty nikaambiwa kama sijaridhika nayo naweza kuirudisha. Sasa uliposema masuala ya DXDIAG nami nikafanya ila kitaalamu maana ya information hizi sijui. Maelezo ni kama ifuatavyo. Kitakachomiss utasema niongeze au kufanya marekebisho na mwisho naomba ushauri kama yafaa au laah! Nimenunua kwa ajili ya kuandika project mbali mbali za kiofisi!
1. Computer name: laptop
2. Operating system: window 7 professional 32-bit (6.1 build 7600)
3. Language: English
4. System manufacturer: Toshiba
5. Bios: ver 1.00PARTTBLO
6. System model: satellite
7. Processor: genuine Intel (R) CPU T 2250@1.73ghz(2cpus)~1.7ghz
8. Memory: 4096mb
9. Page file: 744used; 5378mb available
10. Direction version:direct X 11
Name: mobile Intel(R) 945 express chipset family
11. Manufacturer: Intel corporation
Note: ltk window system ilikuwa 8 nikaomba installation ifanywe ya window 7!!!
Hayo no Maelezo ya ukurasa Wa kwanza baada ya kugonga DXDIAG
cc: wataalam wa ict wote karibuni!!!