Wataalamu wa Lithium nawaomba kidogo

Wataalamu wa Lithium nawaomba kidogo

Engneeer

Member
Joined
Dec 30, 2021
Posts
90
Reaction score
119
Wakuu habari ya muda huu, poleni na majukumu

Nina changamoto yangu moja naomba msaada, nina taa yangu moja ni Watts 5 Dc nataka ikae inawaka kwa masaa 12 na kuchaji simu pia.

Hivyo nilikuwa nawaomba wataalamu wa betri za (Li-ion) Lithium mnisaidie naweza kutumia betri ngapi na za mAh ngapi na bms gani na nataka nikawekee na screen ndogo ya kuwa inaonesha flow ya charge ipo kiasi gani au inacharge nk na pia kuhusu kuzichaji naweza kuchaji kupitia umeme au solar kulingana na mtakavonishauri.

Nawaombeni msaada wenu

Asanteni.
 
Attachments

  • Screenshot_20260226_152730_Chrome.jpg
    Screenshot_20260226_152730_Chrome.jpg
    20.3 KB · Views: 21
Sio mtaalam wa hizo battery ila unaweza Tumia powerbank ama power station kama budget inaruhusu.

5W masaa 12 ni 60Wh, powerbank za 20,000mah ni roughly 74Wh so inatosha masaa 12, na kuhusu kioo tayari powerbank inakua built in.

Kwa battery kama uliyoweka kwenye picha 3000mah kwa 3.7V ni watts 11 so roughly masaa 2 kwa taa yako so utahitaji battery nyingi kufanikisha, zipo kubwa zake hizo battery Hadi 7800mah.
 
kama hiyo taa ni 5W, 12V
tafuta zile mini UPS za airtel router, zina BMS kwa ndani
zinaingiza 12V zinatoa 12V
upande wa kutoka weka buck converter kushusha 12V kwenda 5V kuchaji simu

huwa zinakaa masaa 5 (kutegemea na joto) iki deliver 12W
 
Mkuu asante sana kwa elim yako ila sitak moja nataka nitengeneze betri nyingi kwa ajili ya masoko ndo maaana nkaomba mbinu za ziada
 
Mkuu asante sana kwa elim yako ila sitak moja nataka nitengeneze betri nyingi kwa ajili ya masoko ndo maaana nkaomba mbinu za ziada
chukua 3S BMS , ziko off-shelf kibao kama hii
tafuta cells zako tatu za 5000mAh 3.7V, 18650 (Li-ion au LiPo)
utahitaji wall wart charger ya 12V 2A+ au uunge PV panel moja kwa moja

kuchaji , utahitaji buck converter(off-the-shelf) kama hii zinatoa 5V 3A unapachika kama ni USB-C/micro port uchaji simu
 
Asante sana mkuu naomba unisaidie namba yako mkuu kuna mengi ntaomb unishauri
0769444542 au nitext ahsante
 
chukua 3S BMS , ziko off-shelf kibao kama hii
tafuta cells zako tatu za 5000mAh 3.7V, 18650 (Li-ion au LiPo)
utahitaji wall wart charger ya 12V 2A+ au uunge PV panel moja kwa moja

kuchaji , utahitaji buck converter(off-the-shelf) kama hii zinatoa 5V 3A unapachika kama ni USB-C/micro port uchaji simu
Kwaiyo hizo betri naunga kwa series au parallel na je Naweza pata wapi maduka wanapouza hizo lithium nataka hata za 8000mah zikiwepo
 
Kwaiyo hizo betri naunga kwa series au parallel na je Naweza pata wapi maduka wanapouza hizo lithium nataka hata za 8000mah zikiwepo
unaziunga in series, link niliyoweka ina maelekezo na sakiti
duka lipo ubungo njia panda UD, kuna lingine lipo magomeni HAPA
anza na 5000mAh kwanza
 
chukua 3S BMS , ziko off-shelf kibao kama hii
tafuta cells zako tatu za 5000mAh 3.7V, 18650 (Li-ion au LiPo)
utahitaji wall wart charger ya 12V 2A+ au uunge PV panel moja kwa moja

kuchaji , utahitaji buck converter(off-the-shelf) kama hii zinatoa 5V 3A unapachika kama ni USB-C/micro port uchaji simu
Hakuna 18650 yenye 5000mah
 
Hakuna yà 8000mah hata 5000mah hakuna Kwa 18650 kama unataka zenye 4000+ tafuta 21700 au 26650 battery kumbuka hizo code
Kwaiyo hizo betri naunga kwa series au parallel na je Naweza pata wapi maduka wanapouza hizo lithium nataka hata za 8000mah zikiwepo
 
Tafuta battery original za 18650 capacity Huwa 2200mah mpaka 3500mah max

Let's assume umepata za 3000mah ukiweka in series battery tatu itakupa 11.1v na 3Ah
Sawa na watts 33.3 je inatosha Kwa matumizi Yako hapana itabdi tuongeze zingine tatu in parallel Kila battery Yani iwe 3S3P

Jumla battery 9 ambazo jumla itakuwa watts 100

Itabdi utafute BMS 3S unaweza agiza mtandaoni kama AliExpress ni bei rahisi ama ununue Kwa wauzaji walioko karibu na wewe

Hapo itabdi utafute chaja ya volt 12.6 kama hauna tumia adapter ya PC inatoa volt 19 ila utaweka step down converter Kisha utazungusha Ile scruu isome volt unazotaka ambazo ndo hizo 12.6 ambazo ukigawa Kwa 3 unapata volt 4.2v ambazo ndo ikijaa inapaswa soma hivo

Kingine hio converter unaweza connect na solar mfano solar za volt 12 Huwa zinatoa mpaka volt 18 au zaidi kidogo hivo umeme huo hata volt zikipanda converter Ile ya step down itaset volt ziwe 12.6 TU hata kama zitafika 30v hivo battery ya BMS zitakuwa salama

Hapo solar ya watts 30 itafanya kazi vizuri

Kuhusu kuchaji simu zipo module nyingi ambazo Zina ingiza from 6v to 32v Kisha Zina USB ama type c out ambazo Zina weza negotiate power Zina mfumo WA power delivery PD, QC 3.0 nk simu yoyote inakuwa compatible na hio module
 
Attachments

  • Screenshot_20260909-190035.png
    Screenshot_20260909-190035.png
    256 KB · Views: 1
Back
Top Bottom