vitu vingi ndani ya laptop vinadumu miaka 10 na zaidi.
-cpu miaka 20 hadi 30
-ram nayo 20+
-HDD miaka kama 4 na kuendelea
-same kwenye motherboard zinakaa miaka na miaka
nenda maduka used zile laptop baadhi ni za miaka 10 na kuendelea, mfano angalia core 2 duo
-cpu ya mwisho ya core 2 imetoka 2010.
-cpu ya mwanzo imetoka 2006
hivyo unapoona laptop ya core 2 duo au quad inamaana ina miaka 7 hadi 11, hivi ni vitu vya kawaida kwenye computer kudumu hivyo.
kitu cha kuogopa kwenye laptop ni power supply aka adapter, ikizingua tu hio au ukitumia ambayo ni mbaya na umeme wetu huu wa bongo ujue una risk ya kuunguza vilivyomo ndani,
pia usipofuata maelekezo mengine vizuri kama vile kuziba feni hewa isiingie vizuri, kuacha iingie maji au hali ya hewa pia inaweza sababisha isidumu muda mrefu.