Tatizo hapa ni uongozi ikiwa hii ndio njia pekee ya kumfikisha mgonjwa hospital maana kiongozi anashindwa hata kuwahamasisha wananchi wakaona umuhimu wa kuchangishana na kununua ambulance hata kama itachukua miaka miwili ama mitatu hili ni tatizo.viongozi haohao wanaongoza kuuza mashamba na viwanja vya wazi na kwa manufaa yao.,,,think twice.
SAHIBA.
kutembelea au kutotembelea nchi za nje wala sio hoja. if you got "it" then you got "it", if you don't then you don't, hence Ndivyo Tulivyo
Kwani wao watu wa nchi za nje walienda kwenye nchi gani ya nje?
Suala hapa sio kuhamasisha wananchi na kununua ambulance. Suala hapa ni kupatikana gari a aina yoyote. Mwananchi anapotumia mkokoteni wa kuvutwa na ng'ombe au punda ni udhibitisho kwamba hana uwezo wa kukodi gari au hakuna gari kabisa katika mazingira yanayomzunguka. Mimi nimebahatika kufanya utafiti flani na kampuni moja katika mkoa wa Shinyanga, na hasa katika wilaya ya Kahama. Hali ya huko vijijini ni mbaya kwa kweli. Na suala hapa sio tu kuhamasisha kununua ambulance, bali ni kuweka miundo mbinu ya kuiwezesha hiyo ambulance kupita. Barabara ni mbovu, na kwenye mito hakuna madaraja. Kipindi cha masika hali ni mbaya sana huko. Hakupitiki kwa magari kwa kifupi.
Kama hoja ya Mwanakijiji inavyosema, nadhani tunahitaji miundo mbinu bora kwanza. Dar es Salaam inahitaji kupanguliwa na kupangwa upya. Issue ya mifereji na mitaro ya kupitisha maji ni ya siku nyingi mno. Ujenzi usio na mpangilio maalumu ni sehemu tu ya kero za jiji hili.
You are politically incorrect.
Ambulance ya nini jamii. Nimeshaona mkuu wa kitengo amechukua Ambulance kufuata majani ya kulisha ng'ombe wake wa maziwa.
kwa nini sisi hatukuwa wa kwanza kwenda kwao? kwikwikwiiiiii
Sasa unaleta utani....but knowing us (Miafrika), I wouldn't put that past anybody...
Mabadiliko Tz yataletwa na wananchi....na siyo viongozi!
Wananchi mpo????i
Ambulance ya nini jamii. Nimeshaona mkuu wa kitengo amechukua Ambulance kufuata majani ya kulisha ng'ombe wake wa maziwa.
Je viongozi ni nani ??? Si wanachaguliwa kutoka miongoni mwa wananchi.
Dar Es Salaam,
Please, Hivi wewe kweli unafikiria hayo maendeleo unayoyaona kwa watu nyumbani bila ndugu/marafiki zao nje tungefika hapo tulipo..
Trust me mkuu, kila kitu unachokiona madukani, mitaani na kwingineko kuna Mtanzania aliyeko/ anaishi nje anahusika...
Kama nilivyosema, ambulance hapa sio suluhisho. Suluhisho ni kuwa na zahanati ya karibu yenye madaktari na madawa ya kutosha. Nimewahi kushuhudia mgonjwa kwenye mkokoteni wa punda akisafirishwa for 65kms kwenda kwenye zahanati (sio hospitali). You can just imagine the pain mtu anapitia katika hali kama hiyo. Unajiuliza, maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi? Ahadi za Rais vipi? Kuna vitu ni basic human needs, lakini wenzetu hawazipati. Watu wanashangaa kuhusu mauaji ya vikongwe katika mkoa wa Shinyanga. Lakini sababu inasingiziwa ni imani za kishirikina. But what is the root cause? Hakuna vituo vya afya vijijini. Mtu akiugua, wanakwenda kupiga ramli badala ya kumpeleka hospitali. Huko anaambiwa kalogwa na kikongwe fulani. Baada ya hapo ni mauaji ya kikongwe huyo. Hii ndio hali halisi ya vijiji vingi huko Shinyanga.
Zakumi taabu wananchi wanawaamini mno viongozi kuwa ni jawabu ktk matatizo yao....yet viongozi wako ktk direction tofauti..wizi ..uongo..kujilimbikizia mali n.k
pesa hizi2 wanazoiba wanawahonga wananchi maskini wali na kanga kubaki madarakani..na wananchi wanawachagua!
Ndo nikasema taabu ni wananchi na sii viongozi!
Sasa kama wananchi hawataki kubadilika ...je tufanyeje?
Angalia Mzindakaya amekuwa mbunge Sumbawanga miaka 30 na 2010 watamchagua tena!
If you can make it nje, kwa nini usiweze hapa?